Changamoto za kijana kusaka mchumba zama hizi

Changamoto za kijana kusaka mchumba zama hizi

Kizimbuzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2013
Posts
1,569
Reaction score
749
Salaam wakuu. Kijana wa zama hizi ana changamoto nyingi, moja wapo ikiwa ni kutafuta mchumba/mke wa kuoa. Kutokana na mabadiliko katika jamii. Kutokana na utafiti wangu nimekuja na haya:

1. Baadhi ya wasichana wanapenda wawe na kazi/kipato kwanza ndiyo waolewe au kuzaa.

2. Vijana wengi haswa wasomi wa elimu ya juu ni masikini kuliko wasio soma, au walioishia la 7. Hivyo basi, wenye elimu ndogo wanayamudu maisha ikiwemo kupata wa kuoa, ukilinganisha na wasomi ambao wengine wana miaka 30 hata kitanda hana.

3. Wanawake wengi kwa sasa hawana mapenzi ya kweli, bali wanapenda pesa. Yaani, wanaamini kuwa katika ndoa, utajiri ni jambo la kwanza, ambao utaleta mafanikio, hatimae upendo baadaye.

4. Mfumo wa elimu na utamaduni, umewalemaza vijana wengi na wasichana wengi, kiasi kwamba kijana anashindwa kumudu familia kwa sababu ya kuwa na fikra tegemezi. Elimu inawaandaa wategemee kuajiriwa pekee kitu ambacho kinashindikana kwa wengi. Pia wanawake wameona kuolewa ni ajira tosha kwao.
 
Changamoto nyingine niku nganganiana... Mtu anakunganga Nia had inabdi likuowe tu yaishe
 
Kwahiyo wanawake ndio sio waaminifu!!!
Haya.[emoji124] [emoji124] [emoji124]
 
changamoto nyingine kubwa sana uliyoiacha ni UOGA, wote wanawake na wanaume siku hizi ni waoga sana kufunguka kwa wawapendao, wanaishia kula kwa macho huku wakiumia moyo...
 
Back
Top Bottom