Mr. Miela
JF-Expert Member
- Aug 2, 2007
- 1,254
- 2,121
Kuna kuchemsha na kurusha maji/coolant. Gari inatakiwa i-operate kwenye normal operating temperature mostly 80 to 90c. Iwapo gari itaendeshwa uku temperature yake ikizidi 100c itachemsha na baada ya hapo itasizi (seized) Wakati gari inaoperate kwenye joto zaidi ya 100c husababisha expansion ya metal na kuungua kwa gasket na ikiwa kutatokea kupoozwa kwa ghafla (kuongeza maji/coolant ya baridi) utasababisha kusinyaa/kujikunja kwa zile metal zilizoexpand na hapa cylinderhead hupata madhara. Gari iliyounguza gasket na kupindisha cylinderhead huwa na tabia zifuatazoHivyo Vyote nimefanya, Mara ya mwisho Tuliitoa Kabisa thermostat Gari Ikakaa Sawa, Haikuwa na Shida.
Kwakuwa Ilikaa Muda Mrefu Kidogo Garage, Fundi Aliiosha na akaipiga pressure kwenye Engine ikiwa imewaka kuna wakati Nahisi Shida ilianzia Hapa maana Baada ya Kulichukua sijalitumia Sana Ukiliwasha Tu linachemsha muda Huo huo.
1. Gari kuheat(kupata moto haraka) milipuko inayotokea kwenye cylinder ikipata nafasi na kuingia kwenye mfumo wa coolant husababisha joto la coolant kuongezea haraka isivyo kawaida
2. Kurusha maji/coolant kunakofanana na maji yanayochemka (hii husababishwa na engine compresion kuingia kwenye mfumo wa coolant kupitia kwenye head gasket iliyoungua)
3. Kuchomoka au kupasuka kwa radiator hoses au kupasuka kwa radiator. Hii inatokana na hiyo copresion kwenye mfumo wa coolant
4. Coolant kumwagika kwenye coolant expansion tank. Iwapo mfuniko wa rejeta umechoka na kukawa na compresion kwenye mfumo wa coolant basi coolant itamwagika kupitia expansion tank
5. Gari kukosa nguvu. Hii husababishwa na compresion inayopotelea. Gari litawaka lakini halitakua na uwezo wa kutembea au litatembea kwa shida.
Iwapo gari itapata moto hadi kuzima lenyewe kitaalam inaitwa engine saized. Hii ni hali ya piston kupata moto na kutanuka(metal expansion) hadi kupoteza ule uwezo wake wa kutembea ndani ya sleeve au block. Iwapo itaachwa ipoe kabisa gari inaweza kuwaka tena ila itakua na kelele na kupoteza nguvu. Tiba ya kusizi ni kufanya engine overhaul ikiambatana kurepea engine block na cylinder head au kununua engine nyingine.
Kiujumla gari inayopata moto mara kwa mara mbali na kuharibu mfumo wa wake upoozaji pia huharibu sehemu nyingine kama vile oil seal orings na plastic parts zilizo kwenye engine. Na kwa engine za magari madogo ni bora kununua engine nyingine kuliko kuifanyia overhaul hasa kama imekua na tatizo la kupata moto.