Changamoto za kumiliki gari "unique"

Kuna kuchemsha na kurusha maji/coolant. Gari inatakiwa i-operate kwenye normal operating temperature mostly 80 to 90c. Iwapo gari itaendeshwa uku temperature yake ikizidi 100c itachemsha na baada ya hapo itasizi (seized) Wakati gari inaoperate kwenye joto zaidi ya 100c husababisha expansion ya metal na kuungua kwa gasket na ikiwa kutatokea kupoozwa kwa ghafla (kuongeza maji/coolant ya baridi) utasababisha kusinyaa/kujikunja kwa zile metal zilizoexpand na hapa cylinderhead hupata madhara. Gari iliyounguza gasket na kupindisha cylinderhead huwa na tabia zifuatazo

1. Gari kuheat(kupata moto haraka) milipuko inayotokea kwenye cylinder ikipata nafasi na kuingia kwenye mfumo wa coolant husababisha joto la coolant kuongezea haraka isivyo kawaida

2. Kurusha maji/coolant kunakofanana na maji yanayochemka (hii husababishwa na engine compresion kuingia kwenye mfumo wa coolant kupitia kwenye head gasket iliyoungua)

3. Kuchomoka au kupasuka kwa radiator hoses au kupasuka kwa radiator. Hii inatokana na hiyo copresion kwenye mfumo wa coolant

4. Coolant kumwagika kwenye coolant expansion tank. Iwapo mfuniko wa rejeta umechoka na kukawa na compresion kwenye mfumo wa coolant basi coolant itamwagika kupitia expansion tank

5. Gari kukosa nguvu. Hii husababishwa na compresion inayopotelea. Gari litawaka lakini halitakua na uwezo wa kutembea au litatembea kwa shida.

Iwapo gari itapata moto hadi kuzima lenyewe kitaalam inaitwa engine saized. Hii ni hali ya piston kupata moto na kutanuka(metal expansion) hadi kupoteza ule uwezo wake wa kutembea ndani ya sleeve au block. Iwapo itaachwa ipoe kabisa gari inaweza kuwaka tena ila itakua na kelele na kupoteza nguvu. Tiba ya kusizi ni kufanya engine overhaul ikiambatana kurepea engine block na cylinder head au kununua engine nyingine.

Kiujumla gari inayopata moto mara kwa mara mbali na kuharibu mfumo wa wake upoozaji pia huharibu sehemu nyingine kama vile oil seal orings na plastic parts zilizo kwenye engine. Na kwa engine za magari madogo ni bora kununua engine nyingine kuliko kuifanyia overhaul hasa kama imekua na tatizo la kupata moto.
 
Utaiuza upate nyingine tena kama hiyo au? Una muda gani nayo toka uinunue? Je ulivyoenda kuinunua uliikagua vizuri engine?
Kwasasa Sijajua Ila Natamani Ninunue Gari La Hivi, Nimelitumia Karibu Miaka Miwili (Japo Nitajitahidi Zaidi Kuongeza Umakini katika kulikagua).

Kiukweli Nikubali Hili Lilikuwa Gari la Kwanza na sikuwa Mzoefu kabisa Wa Magari, Aliyenikagulia Alikuwa Jamaa yangu ila Na yeye Naona Hakuwa na Uzoefu wa Haya Magari.

Changamoto Kubwa ilitokea Kuna siku Nilienda, Carwash Jamaa wa Carwash akataka alisogeze ile kuingia na kutaka kuondoka haraka haraka akaweka reverse njiani Anapita Mwenye Kuluger mpya na kuna kimteremko badala akanyage brake akakanyaga mafuta. Akamvaa Mwenye Kuluger Ubavuni akaipindisha mpaka mlango Na Kuumia sana (Bahati Nzuri Kwa nje Gari Yangu haikuumia sana ilibonyea kidogo sana, na ikakwaruzika Taa ya Nyuma kidogo, Sasa ndani vitu vilivurugika sana... wakaniomba msamaha na kurekebisha vitu vichache maana pale pale wana garage hasa bumper nikaondoka, Baada ya Siku Mbili Ndipo Shida zikaanza Kujitokeza.
 
Asante MKUU, Kwasasa Nime Save Nitamtafuta Kesho.
 
Asante Nitaifuatilia Hiyo Garage, Nilipo Huyu Fundi Alikuwa Arusha Baadae akarudi akafungua Garage yake na ndiye anarekebisha Haya Magari.
 
Asante Sana Kwa Maelezo Mkuu, Asante Sana Kwa Elimu.

Hizo Sifa zote Ulizozieleza Naona Zinajitokeza.
 
Sio apeleke gari awafate hao mafundi waje watengeneze gari
We unazani hela ya kuzunguka mipakani na gari la kuvuta ni mchezo gereji moja hadi nyingine usijue kama litapona au laa.
Ukute hao mafundi wako bize utasubiri sana hadi waje
 
Watu hao ni wapumbavu sana, mimi nilichukia sana siku nimenunua gari mpya nikaenda gereji kucheki kwanini gari nikipanda mlima nahisi kama inakwangua chini nikipiga breki nikampa fundi aingie ndani aendeshe asikie tatizo akaja mwenzake wakapanda wakaondoka dakika kumi wakarudi wanasifia jinsi walivyokimbiza gari. Yani gari mpya nilichukia sana watu wenyewe hawana mia wangegonga hata wasingenilipa kumbe gari haikuwa na tatizo lolote ila walienda tu kulikimbiza. Pole sana kwa kuwapa watu wkagonga gari lako na hawakuwa na hela ya kukulipa.
 
Kuna mambo unaweza tukana hadi tusi la mwisho, mimi nilikuwa na gari zamani nilipata ajali mbele bumber iliharibika nikapeleka gereji. Siku naenda kuichukua niwahi harusivya dadaangu kuna dogo pale gereji kaambiwa aitoe gari ailete pale nje niondoke nayo. Dogo kawasha gari karudi nyuma kakwangua gari yangu ubavuni na gari nyingine bonge la pasi. Yani nilihisi kutukana kila aina ya tusi maana mda ulikuwa umeenda na natakiwa niwahi harusi meneja wa gereji anasema brother tutarekebisha nikiangalia hiyo siyo kazi ya leo nawaza mda umeenda nihangaike na usafiri wa umma kwenda kwenye harusi na mwisho gari yangu ikapigwa rangi ubavuni na ikawa imepoteza mvuto kabisa kisa hawa madogo wa gereji. Sometimes bora tu uwaambie mkitaka kusogeza gari langu naomba mniite nije mwenyewe kugeuza.
 
Acha Kabisa, Ila Nilikuja kujifunza Carwash na Baadhi ya Garage Zenye Watu Wasio na Utaalamu ndipo sehemu tunauliwa sana magari yetu.
 
story feki ya kutunga. unamiliki gari eti spare ya 350k brand new original(maana nissan hawana clones) ikakutoa roho mpaka ukauza gari? seriously

Wewe huwezi ukamiliki hata kitoyota vitz maana wishborne tu ya vitz original moja ni zaidi ya sh 600,000. Endelea tu kuendesha baiskeli huko kijijini
 
Huyo hakuwa mjanja, ukikosa spea ya gari bongo, utaipata kwa majirani zetu, Uganda na Kenya Kule ni kama ulaya tu,maana wao wanatuzidi sana ufahamamu kwenye mambo ya magari,hizi gari mnazosema unique huku kwao zimejaa kama njugu
 
Mimi nimepata wasiwasi nilipoona eti namtumbo pale kuna punda na msitu, nikiaanza kuangulia tangu huku juu suluti mpaka kule chini lwinga mtoni sioni popote palipo na msitu wala wafuga punda... angesema mbuzi walau wapo
 

Migari ya Europe sio ya kununua kama una hela ya mawazo.
 
Acha Kabisa, Ila Nilikuja kujifunza Carwash na Baadhi ya Garage Zenye Watu Wasio na Utaalamu ndipo sehemu tunauliwa sana magari yetu.
Majuzi nilipeleka gari kuliosha ile mpaka ndani (seats) wenyewe wanaita kulifua gari. Ni Toyota Ractis, dogo akazifungua seat na kuzipiga maji na gari pia akalipiga maji kwa presha likawa safi, kuja kuliwasha, likawaka na kuleta alama ya P/S (Power Steering) kwenye dashboard, steering ikawa ngumu balaa kukata kulia na kushoto. Baada ya diagnosis kufanyika ikaonekana Power Steering Computer imekufa, kuifungua tunakuta imetengeneza kutu ya kutosha (ni kitendo cha siku 4 hivi), tayari ikawa kipengele. Ila uzuri wa Toyota ni kuwa spea ni bwerere, hela ikatoka na kuweka computer nyingine steering ikarudi mwake mwake babake.

Baada ya ku-google nikaelewa kuwa haifai kupiga pressure water kwenye engine ni hatari sana, maana yanaweza kuingia kwenye ECU na kuua kabisa mashine. Lesson learnt the hard way
 
Sijajua kuna nini kilichojificha kwenye punda..
Ukimgonga mtu anaweza kudhani umegonga mti au umegonga trailer kwa nyuma..
Ambao hawajawahi kushuhudia watakataa hili lakini kule tanga mjini nilishuhudia dala dala limegonga punda bwana bwanaaa itoshe kusema punda ndio aligonga dala dala mana iliharibika vibaya mnooo punda mzimaaaa
 
Mkuu hii gari napanga kuinunuwa mwisho wamwezi huu. Naomba unipe mawili matatu kuhusu hii gari tafathali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…