Tunakosa sana fursa. Kuna nchi ndogo na za kishamba tu watu wanaendesha ndinga za Europe kinyama tu. Tanzania tuna ushamba sana yaani kila mtu IST, Harrier, Rumion, Rav4, Hillux, Prado, Corolla, Mark x, Premio, Vanguard. Yaani ni kero. Ukiingia mtandaoni leo gari kali za Europe ni bei chee sana kuliko hizo za Kijapan ambazo nyingi ni mabati matupu, hazitulii barabarani, lakini tunalazimika wote kununua hizo za Japan. Hivi unajua BWM kali kabisa mtandaoni used unapata kwa bei rahisi kuliko Vanguard au Rav4 Miss Tanzania? Likewise, Audi, Volvo, VW Tiguan, VW Tuareg, Ford Escape, Benz nyingi ni bei affordable kuliko Toyota. Botswana tu hapo watu wako na ndinga kibao za Europe, kwa Tanzania utajuta, spea hakuna!