Changamoto za kumiliki gari "unique"

Changamoto za kumiliki gari "unique"

[emoji23][emoji23][emoji23] hongera sana mkuu. Ukimkuta mtu mwenye wenge na uhitaji ananunua kwa ela nzuri tu. Mambo ya kupeleka spare kwa wakataji ni jau sana, wanalalia sana bei. Wingroad ni gari nzuri, na ukifunga spare nzima hainaga magonjwa ya hapa na pale. Ila inahitaji uwe na discipline tu na matunzo.
Offer nilizokuwa napewa ni za laki 2 wengine laki 4 ila ukienda kuulizia bei kwao ni 900K bila gearbox yake. Ukiweka na gearbox wanaongeza laki 4.5 juu 😂😂😂 nikitazama engine ni nzima haijawahi kufunguliwa gari iliungua na moto yote ikapona engine tu. Maana moto haukufika kuiharibu kabisa mbele.

Nilikaza moyo tu ikafikia wakati nilikata tamaa njaa ilinikamata vibaya mno. Mungu si Rashidi sina hili wala lile napigiwa simu kuna mafundi wanakuja kukagua.
 
Tunakosa sana fursa. Kuna nchi ndogo na za kishamba tu watu wanaendesha ndinga za Europe kinyama tu. Tanzania tuna ushamba sana yaani kila mtu IST, Harrier, Rumion, Rav4, Hillux, Prado, Corolla, Mark x, Premio, Vanguard. Yaani ni kero. Ukiingia mtandaoni leo gari kali za Europe ni bei chee sana kuliko hizo za Kijapan ambazo nyingi ni mabati matupu, hazitulii barabarani, lakini tunalazimika wote kununua hizo za Japan. Hivi unajua BWM kali kabisa mtandaoni used unapata kwa bei rahisi kuliko Vanguard au Rav4 Miss Tanzania? Likewise, Audi, Volvo, VW Tiguan, VW Tuareg, Ford Escape, Benz nyingi ni bei affordable kuliko Toyota. Botswana tu hapo watu wako na ndinga kibao za Europe, kwa Tanzania utajuta, spea hakuna!
Wanakuuzia hizo BM bei affordable coz wanajua kwa kukukamatia, usichekelee huo msiba, jichanganye ununue hakuna rangi utaacha kuiona.
 
Mzee sisi washamba acha tukomae na mjapani tu. Hayo mambo ya sensor million 3 wakati nikienda Tandale na elfu 40 napata sensa mbili ya kufunga na ya akiba nawaachieni nyinyi mafogo.

Wajerumani hawauzi gari tu bali wanauza gari na matatizo yake. Utatuzi wako ndio faida kwao.
Sensor gani inauzwa 3M? Imekuwa Ferrari au Bentley?

Sensor is one of cheapest things to buy in any car.

Acheni kujazana upumbavu.
 
Tunakosa sana fursa. Kuna nchi ndogo na za kishamba tu watu wanaendesha ndinga za Europe kinyama tu. Tanzania tuna ushamba sana yaani kila mtu IST, Harrier, Rumion, Rav4, Hillux, Prado, Corolla, Mark x, Premio, Vanguard. Yaani ni kero. Ukiingia mtandaoni leo gari kali za Europe ni bei chee sana kuliko hizo za Kijapan ambazo nyingi ni mabati matupu, hazitulii barabarani, lakini tunalazimika wote kununua hizo za Japan. Hivi unajua BWM kali kabisa mtandaoni used unapata kwa bei rahisi kuliko Vanguard au Rav4 Miss Tanzania? Likewise, Audi, Volvo, VW Tiguan, VW Tuareg, Ford Escape, Benz nyingi ni bei affordable kuliko Toyota. Botswana tu hapo watu wako na ndinga kibao za Europe, kwa Tanzania utajuta, spea hakuna!
Choice mkuu, kwanini umpangie mtu gari la kununua wakati hela ni zake? Yaani mtu atafute yeye mwenyewe kwa jasho lake aje anunue harrier halafu wewe umuone mshamba kisa hajanunua BMW ambayo wewe unaipenda? Ukinunua wewe inatosha mkuu... asante
 
Kununua gari Kenya siyo kitu rahisi kama kununua gari Tz.

Kwanza ile rule yao tu ya kununua gari isiyozidi miaka 7.

Toyota premio tu isiyozidi miaka 7 CIF yake siyo chini ya 20M. Hapo wazee wa TRA wamekaa pembeni.

Sijajua tu kwa Kenya kodi za magari zimekaaje.
Masikini hawezi nunua gari kenya , kodi pia zipo juu
 
Mwanzo Kabisa ilikua inapasua pipe, yaani ikichemsha maji yantokea kwenye pipe ikiziba inatoboa sehemu nyingine tukabadilisha thermostat, water pump ikatulia kidogo nimeitumia kama miezi miwili Juzi Tar 18 natoka asubuhi nimeikagua kama kawaida maji yapo sawa natoka napandisha kimlima kidogo naona inakosa nguvu, nikamaliza mlima nikaweka pembeni kufungua bonet mvuke unatoka.

Baada ya Hapo Ikakosa Nguvu Kabisa, Ukiwasha Kuondoka Haiondoki. Kuipeleka Garage ilibidi kuivuta.

Ukiwasha muungurumo ukoje? Inamisi? Ukitaka kuondoka haizimi?
 
Kuna mwamba mmoja mzee wa mashauzi classic sana yupo mji kasoro Meli alinunua ka-ford focus kake miaka kama 5 iliyopita hivi, kanafanana fanana na Nissani xtrail hivi, kakaja kufa sensa ya kwenye switch, akiiwasha gari inawaka kidogo halafu inazima.

Mwamba kazungurukaaaaaaaaaaaaaaaaaa weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee, mwisho akaambiwa atachongeshewa kwa laki 9 kwani maduka ya spea ya Dar, Moro na Chuga kote alikosa.

Ikabidi afuate ushauri wa kuchongesha kwa vishoka wa mjini, alivyochongesha sasa kuijaribu kagari kanawaka halafu hakadumu hata dakika moja kanazimika, laki kweli si pesa, laki 9 ndio ikawa ndio imekwenda hiyo.

Akampata muhindi mmoja akamwambia waifungue hiyo switch orijino waitume kiwandani China wakaifyatue nyingine, gharama yake akatajiwa Mil3, amesanda amelifunika na turubai gari lake akiwaza hiyo mil 3 anaweza kabisa kununua kavitz OLD model cha kitaa na akavimba vizuri tu.

UNIQUENESS ni NZURI ILA UWE NA MAPENEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
Saa zingine ushamba hua unasumbua sasa huyo ameshindwa kugoogle hio spare akaipata used au mpya?
 
Kununua gari Kenya siyo kitu rahisi kama kununua gari Tz.

Kwanza ile rule yao tu ya kununua gari isiyozidi miaka 7.

Toyota premio tu isiyozidi miaka 7 CIF yake siyo chini ya 20M. Hapo wazee wa TRA wamekaa pembeni.

Sijajua tu kwa Kenya kodi za magari zimekaaje.
Ila mbona kenya ukiangalia unakuta wanazo Subaru Forester SG5, Subaru WRX ,Mark X GRX120(old model), Toyota Supra MK 4, najiuliza zimeingiaje huko
 
Gari unique ukitaka kutafuta spea yake wewe mwenyewe unajikatisha tamaaa kabla hujaanza kuzunguka. Maana unakua unayajua mazoezi mazoezi yake kuzunguka mji mzima na ilala yote.

Dunia kijiji sawa, utaagiza online lakini utaskilizia mpaka mwezi na nusu uishe spea ifike ukalipie parcel yako ya RDP kwa watu Posta wakupeleke TRA mzozane kodi mmalizane, zote hizi ni gharama ( time and money) bado mzigo haujapotea.

Niliwahi miliki gari inaitwa Opel Vita mpaka na mimi nilikuwa naujua ufundi. Gari inazingua kila ikijiskia, iliwahi nipasukiwa kioo cha nyuma nikaagiza South Africa zilinitoka laki 5 karibia 6 kwa EMS mzigo ulinifikia na nilikua roho juu juu nikiwaza kinaweza pasuka njiani maana kioo cha nyuma huwa hakipasuki kuweka crack, kile kina mwagika vipande coz ni single layer.

Safari nyingine nikapasua kioo cha mbele, Sauzi nilikosa nikakipata Nairobi naada ya kugoogle sana, kupita kwenye ebay, amazon aliexpress na website kote nilimaliza sikupata, ila nikanahatisha Kenya na cost zote ikawa ni 250,000, yakaanza mazoezi kutafuta transporter na kuhakikisha kinanifikia salama, na hapo nilikua mkoani Tabora, mda wote huo gari nimepaki huwez tembea, na kipindi natafuta kioo cha nyuma nilifunika na makaratasi kuzuia vumbi nikawa natumia gari watu wananishangaa wanacheka gari haina kioo na hakipatikani basi kioo kilifika salama nikashusha pumzi

Bado mahitaji mengine ya spea ikawa yanahitajika kwa vifaa vingine solution ikawa ni kukimbilia ebay kuchapana email na wazungu kisa natafuta CV joint, bearing, Zlink, shock ups na vingine, maana bongo nzima hakuna kila unakoenda ukitaja jina la gari jibu ni Aaaah hiyo sina ndo gari gan? Unapicha ya hiyo gari? Naomba chassis namba nikuagizie wakat na mm nakua nimechoka mambo ya kuagiza kusubiri kitu miezi af kakitu kadogo tu, na kiri nilikuwa mtumwa sana. Nilikuja uza ile gari nikamshukuru Mungu kwa kuachana na ndoa ya kikristo.

Ushauri wangu kwa mtu yoyote ntamwambia ukweli gari unique aachane nayo kabisa itampa vidonda vya tumbo na presha. Gari unatakiwa uiendeshe sio ikuendeshe inavyotaka.
😄😄 Motivational speaker wanajisemeaga kirahisi rahisi tu 'dunia Ni Kijiji spare utaagiza tu'
 
Back
Top Bottom