Changamoto za kumiliki gari "unique"

Changamoto za kumiliki gari "unique"

Kuna mwamba mmoja mzee wa mashauzi classic sana yupo mji kasoro Meli alinunua ka-ford focus kake miaka kama 5 iliyopita hivi, kanafanana fanana na Nissani xtrail hivi, kakaja kufa sensa ya kwenye switch, akiiwasha gari inawaka kidogo halafu inazima.

Mwamba kazungurukaaaaaaaaaaaaaaaaaa weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee, mwisho akaambiwa atachongeshewa kwa laki 9 kwani maduka ya spea ya Dar, Moro na Chuga kote alikosa.

Ikabidi afuate ushauri wa kuchongesha kwa vishoka wa mjini, alivyochongesha sasa kuijaribu kagari kanawaka halafu hakadumu hata dakika moja kanazimika, laki kweli si pesa, laki 9 ndio ikawa ndio imekwenda hiyo.

Akampata muhindi mmoja akamwambia waifungue hiyo switch orijino waitume kiwandani China wakaifyatue nyingine, gharama yake akatajiwa Mil3, amesanda amelifunika na turubai gari lake akiwaza hiyo mil 3 anaweza kabisa kununua kavitz OLD model cha kitaa na akavimba vizuri tu.

UNIQUENESS ni NZURI ILA UWE NA MAPENEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
Beforward wanauza spare original kutoka Japana kwa bei nafuu sana. Sema alikosa maarifa tu.

Ila kwa dunia ya leo. Ukikosa spare Dar es Salaam unasogea Kenya. Hapo ukikosa Japan Moja kwa Moja
 
Mimi Nilipo Gari Niliyonayo Zinahesabika Sasa Changamoto yake ni Kuwa Inachemsha.

Gari ni BMW 320i ya Mwaka 2002.

Hii Gari Ina Changamoto ya Kuchemsha yaani unatoka vizuri asubuhi utaona inaanzakupoteza nguvu na mvuke unatoka.

Gari ipo mkoani nyanda za Juu Kusini, Kwasasa Nimeiacha Garage Fundi anashauri nibadilishe Engine.

Kwa mwenye Uzoefu na haya magari na Aliyewahi Kupata Hii Changamoto kwa Haya magari.

Msaada Hata wa mawazo.
Kuna garage ya waturuku Dar. All European cars ndio kazi zao na wapo vizuri.
 
Nairobi wako mbele sana.
Kuna jamaa zangu wa Congo huwa wakikwama spare suluhu huwa nawalekeza Nairobi...huko wajanja wengi na wana kila aina za gari za kifahari.
Watu wengi mnaizungumzia Nairobi lakini hamfahamu uhalisia wake kwa mfano hili la Magari, mnaaminishwa mambo ambayo hayapo kabisa. Ngoja nifafanue hapa.

Ukiwa Arusha, jiji la karibu, uhakika na la haraka la kukimbilia ili kupata chochote unachokikosa ni Nairobi, hili lipo kwa wajanja wengi, na utamaduni wa muda mrefu wa Arusha. Hivyo spare ya gari ukiuliza Arusha na wakasema ni ngumu sana kupatikana basi hata ukienda Nairobi unaweza usiipate kabisa. Kwanini? Wajanja wa Arusha wanaijua Nairobi, ingekuwepo hiyo spare kirahisi Nairobi haraka sana wangekwambia njoo kesho wakupe na kukufungia chap. Kwa mjanja wa Arusha, ni rahisi zaidi na haraka kuitafuta bidhaa Nairobi na kuipata kuliko kwenda Dar.

Kwa sasa utamaduni wa wakazi wa Arusha umeanza kubadilika, badala ya kukimbilia Nairobi kwa sasa wanakimbilia Dar, kwanini? Sababu ni hizi:
1. Wajanja wa Dar wanajua kona zote za kupata bidhaa. Kuanzia Genuine, Fake na Used. Iwe kutoka mkononi kwa mtu, dukani, karakana, wizi nk.

2. Kuna connection kubwa mnoo baina ya mfanyabiashara mmoja na mwingine, mteja mmoja na mwingine kila mmoja anajua mwenzake ana bidhaa gani ambayo yeye hana au aliipata wapi, uswahili wetu umefanya watu kushare taarifa, hivyo ni rahisi mnoo mfanyabiashara mmoja kukurufaa kwenda kwa mwingine, au mteja mmoja kukupa uzoefu wake binafsi kwa jambo linalofanana na wewe.

3. Wabongo wa Dar wamekuwa wepesi mnoo kuagiza bidhaa adimu kwa haraka na uhakika kutoka Dubai na China ikiwa mteja yupo hapo na cash mkononi.

4. Hakuna changamoto ya mipaka ya kimaeneo. (Ujio wa Magufuli na Covid uliharibu mahusiano ya Tanzania na Kenya katika mipaka, mambo yakawa magumu mipakani).

Hitimisho langu ni kuwa, ukikosa spare ya gari yako Dar na Arusha, usisumbuke sana kuisaka Nairobi hukuukiamini kuwa utaipata kirahisi.
 
Kuna mwamba mmoja mzee wa mashauzi classic sana yupo mji kasoro Meli alinunua ka-ford focus kake miaka kama 5 iliyopita hivi, kanafanana fanana na Nissani xtrail hivi, kakaja kufa sensa ya kwenye switch, akiiwasha gari inawaka kidogo halafu inazima.

Mwamba kazungurukaaaaaaaaaaaaaaaaaa weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee, mwisho akaambiwa atachongeshewa kwa laki 9 kwani maduka ya spea ya Dar, Moro na Chuga kote alikosa.

Ikabidi afuate ushauri wa kuchongesha kwa vishoka wa mjini, alivyochongesha sasa kuijaribu kagari kanawaka halafu hakadumu hata dakika moja kanazimika, laki kweli si pesa, laki 9 ndio ikawa ndio imekwenda hiyo.

Akampata muhindi mmoja akamwambia waifungue hiyo switch orijino waitume kiwandani China wakaifyatue nyingine, gharama yake akatajiwa Mil3, amesanda amelifunika na turubai gari lake akiwaza hiyo mil 3 anaweza kabisa kununua kavitz OLD model cha kitaa na akavimba vizuri tu.

UNIQUENESS ni NZURI ILA UWE NA MAPENEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
Mlete kwangu namletea hiyo parts kutoka kwa kaburu hapo sio kwa gharama hizo za kununua gari lingine...na ford ina mtihani akiipaki muda mrefu seal zitaanza kuvujisha hapo ni mtihani bora huo wa kwanza ingawaje SA zipo za kumwaga..
 
Watu wengi mnaizungumzia Nairobi lakini hamfahamu uhalisia wake kwa mfano hili la Magari, mnaaminishwa mambo ambayo hayapo kabisa. Ngoja nifafanue hapa.

Ukiwa Arusha, jiji la karibu, uhakika na la haraka la kukimbilia ili kupata chochote unachokikosa ni Nairobi, hili lipo kwa wajanja wengi, na utamaduni wa muda mrefu wa Arusha. Hivyo spare ya gari ukiuliza Arusha na wakasema ni ngumu sana kupatikana basi hata ukienda Nairobi unaweza usiipate kabisa. Kwanini? Wajanja wa Arusha wanaijua Nairobi, ingekuwepo hiyo spare kirahisi Nairobi haraka sana wangekwambia njoo kesho wakupe na kukufungia chap. Kwa mjanja wa Arusha, ni rahisi zaidi na haraka kuitafuta bidhaa Nairobi na kuipata kuliko kwenda Dar.

Kwa sasa utamaduni wa wakazi wa Arusha umeanza kubadilika, badala ya kukimbilia Nairobi kwa sasa wanakimbilia Dar, kwanini? Sababu ni hizi:
1. Wajanja wa Dar wanajua kona zote za kupata bidhaa. Kuanzia Genuine, Fake na Used. Iwe kutoka mkononi kwa mtu, dukani, karakana, wizi nk.

2. Kuna connection kubwa mnoo baina ya mfanyabiashara mmoja na mwingine, mteja mmoja na mwingine kila mmoja anajua mwenzake ana bidhaa gani ambayo yeye hana au aliipata wapi, uswahili wetu umefanya watu kushare taarifa, hivyo ni rahisi mnoo mfanyabiashara mmoja kukurufaa kwenda kwa mwingine, au mteja mmoja kukupa uzoefu wake binafsi kwa jambo linalofanana na wewe.

3. Wabongo wa Dar wamekuwa wepesi mnoo kuagiza bidhaa adimu kwa haraka na uhakika kutoka Dubai na China ikiwa mteja yupo hapo na cash mkononi.

4. Hakuna changamoto ya mipaka ya kimaeneo. (Ujio wa Magufuli na Covid uliharibu mahusiano ya Tanzania na Kenya katika mipaka, mambo yakawa magumu mipakani).

Hitimisho langu ni kuwa, ukikosa spare ya gari yako Dar na Arusha, usisumbuke sana kuisaka Nairobi hukuukiamini kuwa utaipata kirahisi.
Umeandika maelezo mengi ila kuhusu Nairobi ni kuwa wao wanazo gari kama Isuzu,Nissan ambao na maagent wake wapo pale ni kama jamaa mmoja aliagiza parts ya gari yake Rwanda kwa kuwa wakala yupo pale ni rahisi kuipata...Wauzaji wa parts Arusha hawawezi kuleta parts ya gari ambalo hakuna na hawana uhakika wa kuipata vitu vingi vipo Nairobi na wao wana chinja chinja za kutosha..
 
Inakaa kwa wapi kwenye wish. Mkuu nasumbuka sana asubuhi
Washa ac tu... itasolve mambo yote...

Hiyo ya kushoto👇🏾 Itafute hiyo alama.,

IMG_20221025_084904.jpg
 
Umeandika maelezo mengi ila kuhusu Nairobi ni kuwa wao wanazo gari kama Isuzu,Nissan ambao na maagent wake wapo pale ni kama jamaa mmoja aliagiza parts ya gari yake Rwanda kwa kuwa wakala yupo pale ni rahisi kuipata...Wauzaji wa parts Arusha hawawezi kuleta parts ya gari ambalo hakuna na hawana uhakika wa kuipata vitu vingi vipo Nairobi na wao wana chinja chinja za kutosha..
Mkuu hao maagent wa Nissan, Isuzu hata Dar wapo, na sio issue kubwa.

Biashara ya sasa hivi haihitaji uwe na duka lenye parts nyingi bali inataka uwe na connection mbalimbali za kupata hizo parts popote, kwa hili wafanyabiashara wa Dar wako mbele mnoo. Wewe njoo na parts yako unayohitaji tu, wako speed kuagiza mzigo Japan, Dubai, China, India, Nairobi, South Afrika nk.

Narudia tena kuandika hapa, kwa miaka hii Nairobi ingekuwa mbele sana kwenye parts kamwe usingeona machalii wa Arusha wakija Dar kufanyia services gari zao au kusaka vipuri, mambo yote yangeishia Arusha pale pale au kumalizikia Nairobi.

Nairobi ilikuwa zamani wakati wabongo hawana exposure ya kununua mzigo kwa haraka na wepesi kutoka nchi za Ulaya, America na Asia. Tena Nairobi haikuwa issue za magari tu, mpaka issue za elimu, tiba, dawa, vifaa vya Eletronics ilikuwa ndio kimbilio la waTz, lakini kwa sasa hilo limepotea sana. Nairobi na Arusha ilikuwa kama Dar na Zanzibar miaka hiyo, leo hii ni nadra kuona mtu anatoka Dar kwenda Zanzibar kutafuta bidhaa ambayo Dar haipo.
 
Mkuu huwezi kuta gari mpya imechinjwa daslm kama ambavyo utaikuta imechinjwa Nairobi au Lilongwe hizo Isuzu zilizo road kwa majiji yetu ni mangapi hapa pana mtu kaenda CMC kutaka wiper za Ford Ranger ya 2016 wanamwambia sijui 150,000 hapo Nairobi nimepiga simu naambiwa 50,000 tsh ya Kitanzania kwa zile kubwa hiyo bei sawa na rand 200 au 300 nikinunua Johannesburg niliwahi tafuta alternator ya Ford Ranger ya kwangu hapo kwa Wahindi waliishia 4m wakati Nairobi niliambiwa bei ndogo tuu ila nilipoenda SA nikanunua chini ya 1m..mimi kuhusu parts na magari yake nimetembea machaka mengi mno maana mimi nikiona gari nalipenda nanunua baadae likija swala la parts ndio naanza kutafuta ila kwa kuwa nina mtandao SA hata nikiwa Tanzania chochote kupata inakuwa rahisi kwangu...
 
Beforward wanauza spare original kutoka Japana kwa bei nafuu sana. Sema alikosa maarifa tu.

Ila kwa dunia ya leo. Ukikosa spare Dar es Salaam unasogea Kenya. Hapo ukikosa Japan Moja kwa Moja
befoward gani hio ambayo kuna spea za bei rahisi namimi nikanunue?
 
Sehemu Mlizonielekeza Nimewatafuta, Ninasubiri Wanipe Mrejesho. Wengine Wamekuwa Wazito Kupokea Simu niliwapigia.
 
Nimeshindwa kuweka Video, Nime screen shot Linavyochemsha na kumwaga maji na Hapo, Ukiwasha tu hata kabla Haujaondoka.
Ila Miss Imepungua.View attachment 2399266
X5 ilikuwa inazingua kihivyo, kibuyu (tenki) kikawa kinapasuka kabisa na kumwaga maji jinsi yanavyokuwa ya moto. Tukabadili thermostat bado tatizo likaendelea, tukabadili cylinder head gasket na feni ilifungwa iwe inazunguka muda wote tatizo likapona, lakini tunakagua maji kabla na kila baada ya safari na kuangalia gauge ili kama ikianza tu kupandisha joto unaiwahi na kuliacha lipoe na kuongeza maji
 
Pole kwa changamoto.. Bimmer kwenye cooling system kuna wakati inasumbua kweli.. Kwa maelezo yako una e46 320i hiyo engine ni M54B22.. Kama hakuna leakage yoyote unaona.. Angalia water pump kama ipo sawa.. Then hamia kwenye radiator kama ni safi haina blockage..
Ila kabla ya kwenda kwenye water pump na radiator fanya bleeding ya system.. Inawezekana upepo umeingia.. Kwahiyo hata ukiongeza coolant bado ndani kuna air bubbles zinachukua space.. Fanya bleeding kwa kufungua hiyo nipple..!
 
Asante Sana Mkuu, Nashukuru Sana Kwa Maelezo yako Ngoja Nimshirikishe Fundi.
 
X5 ilikuwa inazingua kihivyo, kibuyu (tenki) kikawa kinapasuka kabisa na kumwaga maji jinsi yanavyokuwa ya moto. Tukabadili thermostat bado tatizo likaendelea, tukabadili cylinder head gasket na feni ilifungwa iwe inazunguka muda wote tatizo likapona, lakini tunakagua maji kabla na kila baada ya safari na kuangalia gauge ili kama ikianza tu kupandisha joto unaiwahi na kuliacha lipoe na kuongeza maji
Hivyo Vyote nimefanya, Mara ya mwisho Tuliitoa Kabisa thermostat Gari Ikakaa Sawa, Haikuwa na Shida.

Kwakuwa Ilikaa Muda Mrefu Kidogo Garage, Fundi Aliiosha na akaipiga pressure kwenye Engine ikiwa imewaka kuna wakati Nahisi Shida ilianzia Hapa maana Baada ya Kulichukua sijalitumia Sana Ukiliwasha Tu linachemsha muda Huo huo.
 
Hahahaaaa inaelekea mwamba alikua anawaoshea saaana na Ford yake bila kujua anatembea na chuma ulete. Mimi naona kibongo bongo bado tuna mda mrefu sana mpaka tuweze kua na variety ya spares za magari yote madukani kama ilivyo Nairobi. Gari nyingi unique upatikanaji wa spare madukani ni tatizo
Sasa si aende tu Nairobi
 
Nina simu hapa display imekufa nilidondosha.Aisee simu ni kali,ila sijui ni aina gn?

Ukiweka laini texts na calls zinaingia lakini huoni ni nani?
Nimezunguka sanaaaaaa but wapiii,ndo basi tena nimeiweka tu sijui cha kufanya
Yani simu haina jina cheki kwenye settings about phone?
 
Back
Top Bottom