Changamoto za kumiliki gari "unique"

Changamoto za kumiliki gari "unique"

Mimi Nilipo Gari Niliyonayo Zinahesabika Sasa Changamoto yake ni Kuwa Inachemsha.

Gari ni BMW 320i ya Mwaka 2002.

Hii Gari Ina Changamoto ya Kuchemsha yaani unatoka vizuri asubuhi utaona inaanzakupoteza nguvu na mvuke unatoka.

Gari ipo mkoani nyanda za Juu Kusini, Kwasasa Nimeiacha Garage Fundi anashauri nibadilishe Engine.

Kwa mwenye Uzoefu na haya magari na Aliyewahi Kupata Hii Changamoto kwa Haya magari.

Msaada Hata wa mawazo.
Nilitakaga kuingia mtego wa kununua hizo 320i ila muonekano wa mbele sikuupenda nikasema ngoja nisubiri 320i za 2012/15 zishuke bei kidogo zina muonekano mzuri. Hizo za chini ya 2012 ni bei chee ila sijazipenda.
 
Kuna mwamba mmoja mzee wa mashauzi classic sana yupo mji kasoro Meli alinunua ka-ford focus kake miaka kama 5 iliyopita hivi, kanafanana fanana na Nissani xtrail hivi, kakaja kufa sensa ya kwenye switch, akiiwasha gari inawaka kidogo halafu inazima.

Mwamba kazungurukaaaaaaaaaaaaaaaaaa weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee, mwisho akaambiwa atachongeshewa kwa laki 9 kwani maduka ya spea ya Dar, Moro na Chuga kote alikosa.

Ikabidi afuate ushauri wa kuchongesha kwa vishoka wa mjini, alivyochongesha sasa kuijaribu kagari kanawaka halafu hakadumu hata dakika moja kanazimika, laki kweli si pesa, laki 9 ndio ikawa ndio imekwenda hiyo.

Akampata muhindi mmoja akamwambia waifungue hiyo switch orijino waitume kiwandani China wakaifyatue nyingine, gharama yake akatajiwa Mil3, amesanda amelifunika na turubai gari lake akiwaza hiyo mil 3 anaweza kabisa kununua kavitz OLD model cha kitaa na akavimba vizuri tu.

UNIQUENESS ni NZURI ILA UWE NA MAPENEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
Dah angeagiza Uingereza hiyo sensor kule hizo gari ni nyingi sana kama IST hapa Dar. Kwenye ma scrape yard huko zipo nyingi sana.
 
Gari unique ukitaka kutafuta spea yake wewe mwenyewe unajikatisha tamaaa kabla hujaanza kuzunguka. Maana unakua unayajua mazoezi mazoezi yake kuzunguka mji mzima na ilala yote.

Dunia kijiji sawa, utaagiza online lakini utaskilizia mpaka mwezi na nusu uishe spea ifike ukalipie parcel yako ya RDP kwa watu Posta wakupeleke TRA mzozane kodi mmalizane, zote hizi ni gharama ( time and money) bado mzigo haujapotea.

Niliwahi miliki gari inaitwa Opel Vita mpaka na mimi nilikuwa naujua ufundi. Gari inazingua kila ikijiskia, iliwahi nipasukiwa kioo cha nyuma nikaagiza South Africa zilinitoka laki 5 karibia 6 kwa EMS mzigo ulinifikia na nilikua roho juu juu nikiwaza kinaweza pasuka njiani maana kioo cha nyuma huwa hakipasuki kuweka crack, kile kina mwagika vipande coz ni single layer.

Safari nyingine nikapasua kioo cha mbele, Sauzi nilikosa nikakipata Nairobi naada ya kugoogle sana, kupita kwenye ebay, amazon aliexpress na website kote nilimaliza sikupata, ila nikanahatisha Kenya na cost zote ikawa ni 250,000, yakaanza mazoezi kutafuta transporter na kuhakikisha kinanifikia salama, na hapo nilikua mkoani Tabora, mda wote huo gari nimepaki huwez tembea, na kipindi natafuta kioo cha nyuma nilifunika na makaratasi kuzuia vumbi nikawa natumia gari watu wananishangaa wanacheka gari haina kioo na hakipatikani basi kioo kilifika salama nikashusha pumzi

Bado mahitaji mengine ya spea ikawa yanahitajika kwa vifaa vingine solution ikawa ni kukimbilia ebay kuchapana email na wazungu kisa natafuta CV joint, bearing, Zlink, shock ups na vingine, maana bongo nzima hakuna kila unakoenda ukitaja jina la gari jibu ni Aaaah hiyo sina ndo gari gan? Unapicha ya hiyo gari? Naomba chassis namba nikuagizie wakat na mm nakua nimechoka mambo ya kuagiza kusubiri kitu miezi af kakitu kadogo tu, na kiri nilikuwa mtumwa sana. Nilikuja uza ile gari nikamshukuru Mungu kwa kuachana na ndoa ya kikristo.

Ushauri wangu kwa mtu yoyote ntamwambia ukweli gari unique aachane nayo kabisa itampa vidonda vya tumbo na presha. Gari unatakiwa uiendeshe sio ikuendeshe inavyotaka.
Sema Opel mbona south Africa ziko nyingi sana ulikosaje huko kuna kiwanda chao kabisa upate Nairobi?
 
Tunakosa sana fursa. Kuna nchi ndogo na za kishamba tu watu wanaendesha ndinga za Europe kinyama tu. Tanzania tuna ushamba sana yaani kila mtu IST, Harrier, Rumion, Rav4, Hillux, Prado, Corolla, Mark x, Premio, Vanguard. Yaani ni kero. Ukiingia mtandaoni leo gari kali za Europe ni bei chee sana kuliko hizo za Kijapan ambazo nyingi ni mabati matupu, hazitulii barabarani, lakini tunalazimika wote kununua hizo za Japan. Hivi unajua BWM kali kabisa mtandaoni used unapata kwa bei rahisi kuliko Vanguard au Rav4 Miss Tanzania? Likewise, Audi, Volvo, VW Tiguan, VW Tuareg, Ford Escape, Benz nyingi ni bei affordable kuliko Toyota. Botswana tu hapo watu wako na ndinga kibao za Europe, kwa Tanzania utajuta, spea hakuna!
Mbona unateseka mkuu? wewe nunua tu mbona wahindi pale upanga wanazo nyingi tu European za kila aina. Unatukana wabongo eti washamba kisa mtu hataki presha za gari. Wewe nunua tu acha mihasira ya ajabu unateseka moyoni kisa wabongo wanaendesha vanguard? Its free country bwana acha kutukana watanzania.
 
Hahahaaa nimekumbuka miaka ya 2000 mwanzoni kuna vibaka walikwapua mkoba wa sista duu k/koo wakakuta Mp3& Mp4 player ya kampuni inaitwa "active" kwa bahati mbaya haikua na charger yake na haitumii betry. Ilikua na bonge la screen na mavideo na miziki kibao.

Kipindi hiko mp3 player zipo on fire kinyamaaaa, mabishoo road unakuta wameweka headphones wanaskiza mangoma tu. Nikajichanganya nikainunua. Waliniuzia 20k. Wakasepa. Nikajiaminisha ntapata charger yake madukani.

Ilipokuja kuzima charge niliitafta maduka yote hola. Na kipindi hiko haya mambo ya kuagiza vitu Kikuu na Alibaba sikua nayajua. Ilikuja kunifia tu mikononi.
Ungeweka tangazo tu dada wa watu achukue mp3 player yake huenda angekubariki utelezi.
 
Daaah mzee baba pole sana. Vipi hujataka kujua uliyemuuzia nae yupo ktk hali gani na hiyo ndinga kwa sasa?

Mimi yule mkulima niliyemuuzia alikua analiendesha kwa fujo sana lile Wingroad. Alikua mtu wa bebes na mitungi saaaana. Alikuja kupata nalo ajali usiku wa manane akiwa bwii miezi minne baada ya kumuuzia likapiga sarakasi gari ikatoka nyang'a nyang'a bahati nzuri aliambulia michubuko tu na alipona. Gearbox ilipasuka, kitu pekee kilichobaki ilikua ni engine na tairi mbili tu.

Alihangaika kutafta spare akakosa. Mwisho akakata tamaa akaamua kukata body na kuwauzia jamaa wa vyuma chakavu.
Gari sharti usigongee papuchi ndani hiyo ni sheria.
 
Tunakosa sana fursa. Kuna nchi ndogo na za kishamba tu watu wanaendesha ndinga za Europe kinyama tu. Tanzania tuna ushamba sana yaani kila mtu IST, Harrier, Rumion, Rav4, Hillux, Prado, Corolla, Mark x, Premio, Vanguard. Yaani ni kero. Ukiingia mtandaoni leo gari kali za Europe ni bei chee sana kuliko hizo za Kijapan ambazo nyingi ni mabati matupu, hazitulii barabarani, lakini tunalazimika wote kununua hizo za Japan. Hivi unajua BWM kali kabisa mtandaoni used unapata kwa bei rahisi kuliko Vanguard au Rav4 Miss Tanzania? Likewise, Audi, Volvo, VW Tiguan, VW Tuareg, Ford Escape, Benz nyingi ni bei affordable kuliko Toyota. Botswana tu hapo watu wako na ndinga kibao za Europe, kwa Tanzania utajuta, spea hakuna!
Hayo magari matatizo yake hata USA wanayajua BMW unatakiwa uwe na hela spea ni bei, pitia page za magari USA uone watu wanavyoponda hizo gari. Ila ukiwa wana be baller nunua tu
 
Tz ni kama tumerogwa na mjapani. Imagine juzi kati nilikua Migori hapo Kenya, vijana IST wanaziita babywalkers, ila huku ndio unakuta mabishoo wanavimba nazo bar. Na kwa namna upatikanaji wa spare unavyosumbua bado tutabaki kua watumwa wa gari za kijapani ambazo spare zimejaa bwerere madukani
Hizo gari zinasumbua hata kenya japo kwa spea wako kidogo afadhali, ila hizo gari hata marekani wananunua watu wenye hela zikianza kuchoka zinasumbua.
 
Ila mbona kenya ukiangalia unakuta wanazo Subaru Forester SG5, Subaru WRX ,Mark X GRX120(old model), Toyota Supra MK 4, najiuliza zimeingiaje huko
Kwa sababu kenya kuna uchumi mkubwa zaidi kwaiyo disposable income inakuwa niyingi zaidi wabunge wakina sonko wanalipwa hela nyingi zaidi na wana mbwembwe zaidi hivyo tegemea vigari vya ajabu ajabu vingi zaidi sababu pesa za hovyo hovyo nyingi zaidi
 
Nilitakaga kuingia mtego wa kununua hizo 320i ila muonekano wa mbele sikuupenda nikasema ngoja nisubiri 320i za 2012/15 zishuke bei kidogo zina muonekano mzuri. Hizo za chini ya 2012 ni bei chee ila sijazipenda.
Ni kweli, Mwonekano wa mbele nachopenda ni vile Ipo Chini Yaani nikipishana mwenye nayo kama hii Bhasi Nafurahi. Kingine Inavyojaa Barabarani ukiingalia.

Hii Inanikamua Haswa, Hii Ikipona ni kuuza nipate Nyingine Tu Sina Kingine.
 
Utaiuza upate nyingine tena kama hiyo au? Una muda gani nayo toka uinunue? Je ulivyoenda kuinunua uliikagua vizuri engine?
 
Mimi Nilipo Gari Niliyonayo Zinahesabika Sasa Changamoto yake ni Kuwa Inachemsha.

Gari ni BMW 320i ya Mwaka 2002.

Hii Gari Ina Changamoto ya Kuchemsha yaani unatoka vizuri asubuhi utaona inaanzakupoteza nguvu na mvuke unatoka.

Gari ipo mkoani nyanda za Juu Kusini, Kwasasa Nimeiacha Garage Fundi anashauri nibadilishe Engine.

Kwa mwenye Uzoefu na haya magari na Aliyewahi Kupata Hii Changamoto kwa Haya magari.

Msaada Hata wa mawazo.
Mkuu fundi anakuingiza chaka. Izo gari changamoto yake kubwa uwa ni sensors tu. usibadili Engine, mafundi wake wapo Dar maybe na Arusha zaidi. Huko uliko fundi atakudanganya tu.
Hayo magari yanahitaji vipimo zaidi kwa computer ili kubaini tatizo.
Mcheki huyo dogo anaweza kukusaidia zaidi 0682 114 311
 
Hivyo Vyote nimefanya, Mara ya mwisho Tuliitoa Kabisa thermostat Gari Ikakaa Sawa, Haikuwa na Shida.

Kwakuwa Ilikaa Muda Mrefu Kidogo Garage, Fundi Aliiosha na akaipiga pressure kwenye Engine ikiwa imewaka kuna wakati Nahisi Shida ilianzia Hapa maana Baada ya Kulichukua sijalitumia Sana Ukiliwasha Tu linachemsha muda Huo huo.
Hayo madude hayataki kuosha kwenye engine kwa pressure. Yana sensor nyingi sana kama mishipa ya fahamu. Pia hayatengenezwi kwa kubahatisha. Lazima ulipime kwanza😀😀
 
Mimi Nilipo Gari Niliyonayo Zinahesabika Sasa Changamoto yake ni Kuwa Inachemsha.

Gari ni BMW 320i ya Mwaka 2002.

Hii Gari Ina Changamoto ya Kuchemsha yaani unatoka vizuri asubuhi utaona inaanzakupoteza nguvu na mvuke unatoka.

Gari ipo mkoani nyanda za Juu Kusini, Kwasasa Nimeiacha Garage Fundi anashauri nibadilishe Engine.

Kwa mwenye Uzoefu na haya magari na Aliyewahi Kupata Hii Changamoto kwa Haya magari.

Msaada Hata wa mawazo.
Umepeleka Garage gani huko nyanda za juu kusini. Kama upo Mbeya Peleka Evolution Auto Garage wana branch yao mitaa ya Mama John. Hapo Soweto kuna mafundi wa gari za Ulaya kuna Benz,BMW kibao raia wanatoka nazo South Africa miaka nenda rudi wanatengeneza huko.

Hapo Mbalizi kwa mzungu Rena, anafanya service ya gari hizo. Ukishindwa nenda Tunduma vuka upande wa Zambia maeneo ya Parking za Basi za Lusaka na Kitwe upande wa kushoto kama unaifata reli kuna njia ya rough road(barabara ya mpaka) mitaa hiyo kuna garage za gari ndogo kuna mafundi watanzania na wazambia wana deal na gari hizo za ulaya na Japan
 
Ni kweli, Mwonekano wa mbele nachopenda ni vile Ipo Chini Yaani nikipishana mwenye nayo kama hii Bhasi Nafurahi. Kingine Inavyojaa Barabarani ukiingalia.

Hii Inanikamua Haswa, Hii Ikipona ni kuuza nipate Nyingine Tu Sina Kingine.
Peleka Evolution Garage mitaa ya Mama John au zama Soweto ndani kuna mafundi wakusaidia
 
Umepeleka Garage gani huko nyanda za juu kusini. Kama upo Mbeya Peleka Evolution Auto Garage wana branch yao mitaa ya Mama John. Hapo Soweto kuna mafundi wa gari za Ulaya kuna Benz,BMW kibao raia wanatoka nazo South Africa miaka nenda rudi wanatengeneza huko.

Hapo Mbalizi kwa mzungu Rena, anafanya service ya gari hizo. Ukishindwa nenda Tunduma vuka upande wa Zambia maeneo ya Parking za Basi za Lusaka na Kitwe upande wa kushoto kama unaifata reli kuna njia ya rough road(barabara ya mpaka) mitaa hiyo kuna garage za gari ndogo kuna mafundi watanzania na wazambia wana deal na gari hizo za ulaya na Japan
Umeambiwa gari haitembei inachemsha kitwe anaendaje? Fundi wake anakuja kwenye gari ilipo
 
Back
Top Bottom