Changamoto za kuomba ushauri mitandaoni ukilinganisha na ushauri wa kuomba unayemjua ana kwa ana

Changamoto za kuomba ushauri mitandaoni ukilinganisha na ushauri wa kuomba unayemjua ana kwa ana

Dr. Zaganza

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
1,414
Reaction score
2,181
1. Wakati unasumbuka na tatizo la ndoa, kumbe robo tatu ya watoa ushauri hawajawahi kuishi na ndoa zaidi ya kudanda danda tu hapa na pale.Kwa kifupi hawajawahi saini mkataba mbele ya mashahidi na viongozi wa dini kwamba changamoto na furaha atazikabili. Mikataba alosaini ya kisela tu. Robo tatu ya wachangiaji utaona michango yao hailengi kutatua tatizo kumbe kiuhalisia umewapeleka kina kikubwa cha maji.umewapeleka madarasa ya mbeleni mnoo, zamani wazee ndo washauri kwa kuwa washafika mwisho kiuzoefu.Unakuwa unaulizia vifaa vya ujenzi kwenye duka la vipodozi.

2. Wakati unaleta mgogoro wako na ndugu zako unavyokukosesha amani, uzito wa undugu unaoelewa wewe kumbe na uelewa wa wachangiaji ni mbingu ni ardhi. Robo tatu yao utaskia mimi nishafuta namba zao. Wengine nishaacha kuhudhuria vikao vya familia. Umetaka kingine, unapewa kingine.Tuko na kizazi hakisumbui kichwa kutafuta suluhu, akikosa kazi ,anakuwa chawa. akizidiwa na tatizo au hasira anaua au kujiua, na kila mtu ana simu janja ya kukushauri.

MUHIMU: mfahamu unayemuomba ushauri ana uzoefu gani eneo hilo
 
Baadhi ya nchi ushauri ni fani maalum inayosomewa, fani mbalimbali unapewa général knowledge ili stress ya daktari uijue ,ya askari uijue, ya jobless uijue, ya mwanandoa uijue kabla ya kushauri

Sasa kaokote ushauri kwenye page ya msanii ,uulete ndani, utajuta!!
 
Back
Top Bottom