Changamoto za kupata mtoto mchanga ukiwa umri wa kustaafu, unakuwa ni Baba Babu. Dawa ni kujipanga kabla, vinginevyo ni kubebesha watu mizigo yako

Wengine watachukulia utani - lakini kuna somo kubwa ya kutosha hapo kuhusu kutokukimbilia kufanya biashara usizozizoea kwa pesa ya kiinua mgongo.

Ni bora kabisa fedha za kustaafu zikawekwa katika hatifungani za serikali za miaka 25 au 20.

Kwa vile siku hizi wengi wamezijua hatifungani, hivyo ushindani kuwa mkubwa, bado kuna utt inayofuatia kwa ukubwa wa riba- na uzuri utt haina ushindani kusema utazikosa..

Pesa zisiachwe kwenye savings account wala zisiingizwe katika biashara ya kujifunza uzeeni..
 
Kitendo cha fedha hizo kukaa Benki kwenye account ya savings, faida yake ni kiduchu Sana. Zingekaa kwenye a fixed deposit account, FDA, zingezalisha faida kubwa kidogo, lakini mpango mzima wa ukweli na wa uhakika wa uwekezaji wa mafao yako ni Kwa kuwekeza Kwa ununuzi wa dhamana za serikali, yaani Government Bonds, ambazo huuzwa na Benki Kuu ya Tanzania ambapo hutoa riba ya mpaka asilimia 16%!.

Sasa tupige hesabu ya Pamoja.
Tuseme mafao yangu ya kustaafu ya mkupuo ni milioni 100. Nikinunulia Government Bonds za miaka 25, kila mwaka nitapata shilingi milioni 16. Bonds wanalipa gawio mara 2 Kwa mwaka, kila baada ya miezi 6. Hivyo nitalipwa shilingi milioni 8 kila miezi 6.

Asante kwa elimu ya uwekezaji (investment). Tatizo linakuja, tukistaafu, ndio tunategemea mafao hayo tukajengee nyumba, je, huo uwekezaji tutauweza? Tunategemea hela hiyo tufanye mambo yote tuliyoshindwa kufanya tukiwa kwenye ajira; kujenga nyumba ya kuishi, kununua gari, shamba, nk, hapo hela ya uwekezaji itabaki? Sio kwamba hatutaki kuwekeza, la hasha, ila uhalisia wa maisha unatupeleka uelekeo mwingine!
 
Wakina Ibrahim walipata watoto wakiwa na miaka 90 lakini waliishi miaka 200+.

Umri wako haupo mbali na baba yangu.

Mama yangu ni 50+ ni biologically impossible kuconceive.

Hii inamaanisha ma mdogo umri wake ...

Anyway, nina maswali yanazunguka hapa ila basi tufuturu kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…