Changamoto za madereva na abiria wa Uber na Bolt. Tupia yako

Changamoto za madereva na abiria wa Uber na Bolt. Tupia yako

Wengine huwa hawazingatii vigezo na masharti hivyo mara kwa mara huishia kuwapa marks zisizozidi 3/5
Sijawahi toa Marks zaidi ya 3 Yani tatu ni alama ya juu kabisa!

Saingine mara chache nawapa 2/5
 
Niliwahi kuitisha Uber maeneo ya Mbagala inipeleke maeneo ya Tandika sokoni. Wakati naita range ya nauli ilikuwa kati ya Tsh 9000 hadi Tsh 11,000; wakati wa safari niliona kwenye ramani kama route imecheza na kuonesha tuko pande za Kipawa - Gongo La Mboto tunaitafuta Temeke. Kufika Tandika nauli inasoma Tsh 23,000. Nikakumbuka siku chache zilizopita nilisoma malalamiko hapa JamiiForums kwamba kuna madereva wa Uber wameanza wizi wa kucheza na ramani/route na kufanya bei ya nauli isome kubwa, nikajua na huyu amenichezea picha la kihindi. Nikagoma kumlipa hiyo Tsh 23,000 nikakomaa hadi nikamlipa Tsh 11,000 yake na kusepa.

F@l@ sana yule dereva
Yani uwezo na ujuzi wa kubadilisha muelekeo wa Gps yenye kuonyesha gari ipo maneno gani hata sielewi inawezekanaje, wabongo hatari.
 
Sema madereva kutana na watu wa kila aina wasio na aibu, hasa mashoga, na wa ku danga, yaani stori unazisikia lakini inabidi ukae kimya maana hayakuhusu. Sema daah
 
Mara mtu kaita uber alafu ana bonge la mzigo wa kuchukua, hapo inakua kero kwa dereva, maana gari sio ya mzigo kubwa, jamaa wanataka mpaka kupakia Friji na nauli alipe eti 4,000
 
1. Madereva huwa "wema sana" kupisha magari mengine, waenda kwa miguu, na wafikapo taa za barabarani, hukawiakawia mradi kijani ikate wasubirie. Huku kujichelewesha kwani je vipi?

2. Ukiita gari, halafu dereva akapiga simu kuuliza, kwani tunaelekea wapi? Ujue huyo ni dereva mbabaishaji.
 
Mi nimeita bolt, ikaja namba, kimbembe namba ya Bajaj tofauti na namba halisi, na picha ya dereva pia tofauti na dereva halisi halaf anaendesha taratibu na hapanui hata kidogo. Kwenye barabara ya vumbi Sasa, anaendesha taratibu Kama katoka kununua gari jipya showroom. Nikamwambia tu nauli ilikuwa buku 3 ikiongezeka utaongeza wewe. Bahat nzur had nafika ikawa ile ile miksa dereva kununa kwa Nini Bei haijaongezeka. Mi nikashukuru na kumpa 3/5
 
Niliwahi kuitisha Uber maeneo ya Mbagala inipeleke maeneo ya Tandika sokoni. Wakati naita range ya nauli ilikuwa kati ya Tsh 9000 hadi Tsh 11,000; wakati wa safari niliona kwenye ramani kama route imecheza na kuonesha tuko pande za Kipawa - Gongo La Mboto tunaitafuta Temeke. Kufika Tandika nauli inasoma Tsh 23,000.

Nikakumbuka siku chache zilizopita nilisoma malalamiko hapa JamiiForums kwamba kuna madereva wa Uber wameanza wizi wa kucheza na ramani/route na kufanya bei ya nauli isome kubwa, nikajua na huyu amenichezea picha la kihindi. Nikagoma kumlipa hiyo Tsh 23,000 nikakomaa hadi nikamlipa Tsh 11,000 yake na kusepa.

F@l@ sana yule dereva
Labda bolt. Uber hauwezi kufanya hivyo vitu kaka yangu uber ipo very secure....
 
Madereva wa taxi wanalalamika sana ajili bei zimepungua sababu ya uber na bolt.
 
Kuna mmoja nilikua nawahi sehemu akanambia kuwa hapa tukifata hii barabara tutachelewa, kwahiyo tuzime uber mi nipite njia za magumashi tutawahi, ila utanilipa kama Tax. Dah! jamaa alizingua sana siku ile.
 
Back
Top Bottom