A
Anonymous
Guest
Sisi waombaji wa mikopo ya asilimia 10 kutoka Halmashauri ya Nyamagana tunakabiliwa na changamoto mbalimbali katika mchakato wa kupata na kutumia fedha hizo.
Baada ya kupitia ukaguzi wa kamati tatu (kamati ya kata, kamati ya halmashauri na kamati ya wilaya) na kikundi kupitishwa, husaini mkataba na halmashauri. Hata hivyo, inadaiwa kuwa Afisa Vijana huwalazimisha baadhi ya vikundi kusaini zabuni na mzabuni anayependekezwa na yeye. Kikundi kinapochagua mzabuni mwingine, huondolewa kwenye mfumo na kunyimwa fedha, licha ya mzabuni wa afisa huyo kuwa na bei za juu.
Vikundi vilifungua akaunti katika Benki ya NMB, lakini baadaye vilipewa maelekezo ya kuhamisha fedha moja kwa moja kwenda kwa mzabuni badala ya kutoa fedha. Benki ya NMB ilikataa utaratibu huo, ndipo vikundi vikaelekezwa kufungua akaunti katika Azania Bank.
Baada ya fedha kuingia, vikundi viligundua kuwa kwenye akaunti zao kulikuwa na ongezeko la signatory kutoka watatu waliowekwa na wanakikundi hadi wanne, bila taarifa au ridhaa yao. Inadaiwa signatory wa nne ni Afisa Vijana.
Kwa sasa, kikundi kinapowasilisha muhtasari wa kuhamisha fedha kwenda kwa mzabuni waliyechagua, Afisa Vijana hataki kusaini isipokuwa kikubali kutumia mzabuni anayependekezwa na yeye.
Tunaomba mamlaka husika zifanye uchunguzi kuhusu utaratibu huu ili kuhakikisha mikopo ya asilimia 10 inasimamiwa kwa uwazi na kwa kuzingatia haki za vikundi vilivyonufaika.