Morning_star
JF-Expert Member
- Apr 21, 2018
- 6,008
- 17,480
Nakumbuka miaka ya 80s mitaa ya kariakoo kulikuwa na nyumba za tope za Wamanyema kutoka (kigoma) na wanyamwezi (kutoka tabora).
Maisha yalivyokuwa yanapanda watu wakapakimbia Kariakoo na kuja kujenga au kupanga maeneo ya Ilala hivyo hivyo wakakimbia na kuja Buguruni mpaka uzee unawadaka na kufariki na maisha yanaishia hapo na kuacha kizazi chao katika umasikini wa kutupwa.
Hao watoto nao wanaanza kukimbia Buguruni na kuhamia Kipawa au Gongo la Mboto, n.k, n.k. Point yangu ni hii hapa kwamba wewe unakimbia changamoto za maisha kwa kutafuta kuishi sehemu zenye unafuu wa maisha kumbe unakimbia fursa na utajiri unakimbilia umasikini.
Hao Wamanyema na Wanyamwezi na Wazaramo ambayo enzi hizo walikuwa wanamiliki nyumba za tope waliokomaa na changamoto za maisha wakapambana nazo mwisho wake wamekuja kuuza viwanja walipojenga hizo nyumba za tope kwa million kuanzia 200 na kuendelea (enzi hizo) na waliokuwa na akili waliingia ubia na wafanyabiashara kwa kupatiwa apartment ya biashara au katika maghorofa na sasa wanakula kuku.
Ukiona sehemu kuna changamoto zinazoendana na wingi watu jua ndo penye fursa usipakimbie eti unatafuta sehemu zenye unafuu wa maisha kwa kufanya hivyo unakimbilia umasikini labda kama unaenda kujipanga kimkakati.
Changamoto hukomaza akili na kukupa ujasiri wa kupambana na maisha. Kwa mfano kijana umebahatika kupaya mahali pa kujishikza Dar eti unakimbia unaenda mikoani? Labda kama mikoani umepata deal za kukutoa lakini unarudi kwenu kufanya nini kwa mfano?