Changamoto za nchi za Afrika kwenye michezo ya Olimpiki

Changamoto za nchi za Afrika kwenye michezo ya Olimpiki

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
gfdsgdsg.jpg

Kwenye michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020 iliyomalizika hivi karibuni, kumekuwa na mambo mengi mapya ya kushangaza na kufurahisha, ikiwa ni pamoja baadhi ya nchi kupata medali kwa mara ya kwanza kwenye baadhi ya vitengo, na hata uwakilishi wa baadhi ya nchi kwenye michezo hiyo kuwa wa mchanganyiko (diverse) kuliko ilivyowahi kutokea kabla. Kwenye baadhi ya michezo ukiangalia mshindi wa kwanza hadi watatu utaona bendera za nchi za magharibi, lakini sura zina asili ya Afrika. Kwenye baadhi ya timu unaweza kuona timu mpya zimejitokeza kwenye baadhi ya michezo na kupata medali, zikiwa na mchanganyiko wa wachezaji

Hali hii imepongezwa na baadhi ya watu wanaoona kuwa michezo ya Olimpiki ni uwanja wa kuonyesha uwezo wa mwili wa binadamu, na kwamba inatoa fursa kwa wanamichezo wenye uwezo ambao kutokana na sababu moja au nyingine wameshindwa kuonyesha uwezo wao kwa kuwakilisha nchi zao. Lakini pia kuna wale wenye wasiwasi kuwa hali hii inarudisha nyuma sekta ya michezo kwenye nchi zisizo na uwezo mkubwa kifedha, kwani wachezaji wao wanavutiwa na nchi ambazo zinawapa mazingira bora zaidi ya maandalizi na hata fursa ya kushiriki kwenye michezo hiyo.

Hii sio mara ya kwanza kwa sauti kama hii kusikika, kwani mwaka 2018 Ufaransa ilipochukua kombe la dunia, baadhi ya watu walikuwa wanajiuliza ingekuwaje kama wachezaji wenye asili ya Afrika wangewakilisha nchi za Afrika? Ni vigumu kupata jibu la swali hili, lakini ni rahisi kusema kutokuwepo kwao kwenye nchi za Afrika kumeacha pengo ambalo limedhoofisha uwezo wa michezo wa nchi zao. Kwa baadhi ya nchi kama Kenya na Ethiopia, ni rahisi kuelewa wachezaji wanaoamua kuchukua uraia wa nchi nyingine ambako wanapata fursa ya kushindana kwenye michezo ya kimataifa, kwani katika nchi zao kuna vigezo vya juu sana kupata nafasi hizo, tofauti na kwenye nchi wanazohamia ambako vigezo japokuwa ni vya kimataifa, viko chini kuliko nchi zao.

Tukiangalia hali kwa undani hali hii (brain drain) tunaweza kuona kuwa nchi za Afrika zimekuwa ni wahanga na zinaendelea kuwa wahanga, hasa kutokana na watu wake wengi hodari kuhamia kwenye nchi za magharibi na kuzinufaisha nchi hizo. Ni rahisi kwa hali hii kuonekana kwenye michezo ya Olimpiki kwa kuwa dunia nzima watu wanaona kwenye televisheni. Lakini kiuhalisi hali hii iko kwenye sekta mbalimbali kama vile elimu, afya, ujenzi na hata sekta ya huduma. Watu wengi ambao wamelelewa (nurtured) na kuendelezwa na nchi za Afrika, wamekuwa wakizinufaisha nchi za magharibi na nchi zao kubaki nyuma.

China imekuwa na mifano kadhaa inayoweza kufuatwa kwenye eneo hili. Tofauti na nchi za magharibi, China imekuwa ikijitahidi kuchukua watu wenye vipaji kutoka kwenye nchi za Afrika, iwe ni kweli sekta ya afya, sayansi, au elimu na kujitahidi kuwapa mafunzo kwenye vyuo vya China, na hatimaye kuwarudisha ili waweze kutoa mchango zaidi kwenye maendeleo ya nchi zao. Hata baadhi ya maofisa wa ngazi mbalimbali na sekta mbalimbali, wamekuwa wanakwenda kupata mafunzo nchini China na kurudi kwenye nchi zao wakiwa na ujuzi zaidi.

Wakati mwingine, wakiwa wanapata mafunzo nchini China, ujenzi wa sehemu wanazoweza kutumia kuonyesha wao barani Afrika, kama vile maabara, hospitali n.k. unakuwa unaendelea. Wanaporudi sio tu wanakuwa na sehemu bora zaidi za kufanyia kazi, bali pia wanakuwa na ujuzi zaidi kwenye utendaji kazi wao.
 
Kama hao wawili pembeni ya kipchoge asili yao ni Somalia ..wengi wanaoenda ulaya mostly nchi zao Zina migogoro, Vita (ukimbizi), wazamiaji kutokanana na ugumu wa maisha, wengine ni kuchanganya wazazi nchi mbili etc...Lakini nadra sanamataifa ya ulaya kuja africa kufanya recruitment direct kupata vipaji kwa ajili ya nchi zao.....hiyo ipo hasa kwenye soka na huwa Ni kwa clubs not nchi.
 
Back
Top Bottom