Nilishawai muuliza dada mmoja ambaye alikuwa ameolewa mke wa pili na jamaa flani;
Hivi kwanini unachepuka wakati umeolewa?
Jibu alonijibu wallah niliishiwa nguvu,
Yule dada alisema hivi; Tatizo dushelele la foleni yeye hawezi,
dah niliishiwa nguvu sasa mpaka nikajiuliza kwanini akubali kama alikuwa hawezi kulisubiria mpaka litoke uko kwenye mzunguko.
Ukiachana na mfano huo hapo juu upo mwingine ambao nao pia ni dada ambaye najua makuzi na malezi yake, alikulia katika dini na alikuwa na msimamo thabiti katika dini, aliolewa na jamaa flani, ambaye waliishi vizuri wakafanikiwa kujenga na kuwa na maisha mazuri.
Baada ya kuwa na maisha mazuri jamaa aliowa mke wa pili na hapa ndipo timbwili lilipoanza, maana mwisho wa siku yule dada naye alitafta mtu wa pembeni kwa ajili ya kumtoa mawazo.
Jambo hili limekuwa likinichanganya sana, maana nikitazama wengi walokuwa na mahusiano na mke zaidi ya mmoja, wengi wanasaidiwa wake zao awe mkubwa au mdogo.
Nimejikuta naogopa hata ikifikia kuja kuoa wake wawili, maana wengi wanachapiwa na hawajui wanachapiwa.
Na sababu kubwa nimeiona wanayoijenga wanawake ni kuwa bwana wakuchangia hawawezi.
Sina lengo na kupingana naafundisho alokuja nayo bwana mtume, (Rehma na Amani zimshukie), ila nikitazama wanawake wa zama hizi ni mtihani kwakweli, maana kila ninapozungumza kwa hawa watu hali ni hiyo hiyo, yani kumi kwa mmoja ukute ndo mwenye kujiheshimu, maana haya mambo yanafanywa mpaka na wamama wa makamo yaani ukiwaangalia huwezi amini.
Angalizo kwa walioa wake wawili;
1;Jamani msijisahau sana iwe nyumba kubwa au ndogo basi kule ambapo utakuacha basi ujuwe watu wanakusaidia.
2;Pia ziara za kustukiza muhimu sana,maana wengi akiwa zamu ya bi mkubwa, huku kwa bi mdogo anamuacha free tu usiku kucha hata kupitia pita hakuna mpaka ifike zamu ya mchana, au kama atapita basi mchana,
Jamani kuweni makini mkitoa tu miguuu watu usiku wanakuja kulala na uzuri ratiba zenu wanazijua fika siku ambazo hampo.
Ebu wadau mkuje hapa tupeane maarifa maana mpaka nimekuwa muoga sana wakumiliki majiko mawili japo natamani sana hapo baadae, maana kwa sasa hali tete.