Changamoto za uke wenza

Changamoto za uke wenza

Hapo tatizo ni baba yako siyo uke wenza.
Mwaka wa sita leo naishi na wanawake wawili lawama pekee ninazopataga ni kwa nini kwa mama fulani umelala siku nyingi??
Na hapo ujue upande A ulizingua nikaenda B,siku nimerudi A ni mpole na atauliza kwa lugha ya upendo maana tofauti na hapo nitarudi B,lakini kuhusu mahitaji ya familia ni 50/50 kabisa kama A watalala njaa basi na kule B hali iko vilevile maana kama A kuna chochote nitakigawa na B wapate,sasa naomba umlaumu baba yako alinogewa akili akaweka rehani.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu hebu tumegee siri yako ya mafanikio katika maelewano yao just tips tuu, zitusaidie wengine
 
Na ana uwezo sana kiuchumi huyo shemeji yako au ndo anasambaza tu umaskini na hao watoto 13? Afu maskini ndo tunapenda zaidi mitala sijui ndo tunajitutumua angalau tuonekane although hatujakosa nguvu za kiuchumi basi tuna za viunoni mweeh
Za kiunoni zenyewe watoe wapi!!! Wanajichetua tu.
 
Mkuu hebu tumegee siri yako ya mafanikio katika maelewano yao just tips tuu, zitusaidie wengine
Hakikisha wanapata haki ya ndoa to the maximum, hii inawezekana maana wote wanakuwa wamekukumbuka kwa nyakati tofauti kwa sababu unaishi nao kwa nyakati tofauti kuna kahali flani ka kukumiss.

Ukielezwa kezi za upande wa pili ziache hukohuko usihame nazo ila zipokee na kuahidi kuzifanyia kazi.NB:wake wenza kesi ndogo ndogo ni kawaida.

Hakikisha mahitaji ya msingi yapo kila familia na yakikosekana basi iwe kwa pande zote mbili.

Nguo,wanunulie kwa usawa.

Usikubali wawe marafiki,lakini kemea uadui kati yao na mkaidi muadhibu kwa kutokwenda kulala na siyo kumnyima mahitaji.

Hizo chache zinatosha mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakikisha wanapata haki ya ndoa to the maximum, hii inawezekana maana wote wanakuwa wamekukumbuka kwa nyakati tofauti kwa sababu unaishi nao kwa nyakati tofauti kuna kahali flani ka kukumiss.

Ukielezwa kezi za upande wa pili ziache hukohuko usihame nazo ila zipokee na kuahidi kuzifanyia kazi.NB:wake wenza kesi ndogo ndogo ni kawaida.

Hakikisha mahitaji ya msingi yapo kila familia na yakikosekana basi iwe kwa pande zote mbili.

Nguo,wanunulie kwa usawa.

Usikubali wawe marafiki,lakini kemea uadui kati yao na mkaidi muadhibu kwa kutokwenda kulala na siyo kumnyima mahitaji.

Hizo chache zinatosha mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Shukrani mkuu ,
Nini mantiki ya kuzuia urafiki kati yao mie , nilidhani itapendeza wao kuwa marafiki kwani hata ukaribu wa familia hz mbili utakua mkubwa.
 
Usikubali wawe marafiki,lakini kemea uadui kati yao na mkaidi muadhibu kwa kutokwenda kulala na siyo kwa kumnyima mahitaji.

“Mkaidi muadhibu kwa kutokwenda kulala kwake”.... hii ni adhabu..? [emoji848][emoji848]
 
Na ana uwezo sana kiuchumi huyo shemeji yako au ndo anasambaza tu umaskini na hao watoto 13? Afu maskini ndo tunapenda zaidi mitala sijui ndo tunajitutumua angalau tuonekane hatujakosa nguvu za kiuchumi angalau tuna za viunoni mweeh
Hana uwezo hata watoto wengine inabidi asaidiwe na ndugu kusomesha may be ndio maana wake zake wametafuta wanaume wengine
 
Unachosema ni sahihi ila pia ukiuliza watu wenye ndoa za mke 1 zenye miaka 15 na zaidi, kama angekuwa anaoa leo angemuoa mke aliyenaye, 90% wangekujibu hapana.
98% ya familia za mitala hazinaga amani wala maelewano kubali kataa lakini ndo ivo, ata wawe wanaishi mikoa tofauti hao wake wenza yaani hakunaga.....na wengi walio oa mara nyingi ukiongea nao lazima akwambie anajutia kuoa mke zaidi ya mmoja ni kwanini???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi shemeji yangu wake zake wanaelewana sana lakini ndio kila mtu ana mchepuko wake ila shemeji yetu ameshajua tunamuonea hata huruma aanaishia kunywa mipombe tu kachakaa hafai halafu wake zake wanajiremba warembo hao kufukuza anashindwa tayari ana watoto 13 yaani anatiaga huruma
anasikitisha sana, wake wakipata maumivu lazima apate mume
 
Ndoa zinachangamoto nyingi hakuna mwanamke anayelazimishwa akae mitala wengi wanakubali wenyewe, kwahyo hapo kosa si wanaume , kosa liende kwa wanawake wenyewe kwanini mtu akubali kuolewa mke wa pili?? Hata Kama wanawake wengine wakigoma Kuna wanawake hao hao wanakubali ndio maana wanasema adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzie na Wala si mwanaume.
 
Jamani jamani, kwanza kabisa happy new year na lile jina ulipendalo ntalirudisha kwa ajili yako
Same to you!

Uwe mwaka wa mafanikio makubwa sana kwako. Nitafurahi likirudi maana nalipenda lile jina. Nkikumbuka yale ya kwa waziri mkuu ndio hahahahahaah
 
Back
Top Bottom