Changua kuambatana na familia au mwanamke unayetaka kumuoa

Changua kuambatana na familia au mwanamke unayetaka kumuoa

Nashengena

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
2,913
Reaction score
5,318
Hatimaye kijana wetu amaeamua kuchangua familia dhidi ya mwanake aliyetaka kumuoa. Mwingine alikengeuka lakini kilichotokea hadi leo anajuta.

Kijana wetu huyu wa kwanza ana miaka 26, yeye alikuwa na mahusiano na mwanamke ambaye ana watoto 2 kila mmoja na baba yake. Kijana kamaliza shahada yake akapata kazi . Baada ya kupata kazi akakutana na huyo mwanamke. Kijana akawa hashikiki mpaka akawa anawadharau wazazi wake.

Akaondoka pale nyumbani akaenda kuishi na huyo mwanamke tena kwa ugomvi mwingi na familia yake. Wazazi wakalileta hilo jambo kwa familia, na kikao kikakaa naye akiwepo. Akasemwa na akaambiwa changua sisi au yeye. Hatimaye mwezi huu kaamua kubaki na familia na kuachana na yule mwanamke na kuomba msamaha wazazi wake.

Mwingine yeye alikuwa na mwanamke ambaye inasemekana kwao ni washirikina sana. Baba wa kijana wa kiume alikuwa na hela ndefu. Kijana alipokuja kumtambulisha huyo binti familia yake ikakataa. Kijana akaendelea kukomaa. Yule baba akamuambia yule mwanae na yule binti, hamtakaa mle mali zangu. Mzee akaanza kuugua, wakati yuko hospitali kijana akawa anafurahi kuwa mzee anakufa muda si mrefu tutafaidi mali. Alikuwa ni kijana pekee wa kiume na dada zake 2. Wakati mzee anakaribia kufa kijana akachukua magari na akaenda kuyaficha huko Arusha kwa rafiki zake.

Baada ya mzee kuzikwa, yule kijana akaenda na mwanamke wake kula bata na gari za marehemu baba yake, gari Gari hiyo ya baba yake akapata ajali na yule mwanamke akafia palepale. Kijana aliumia kidogo. Mpaka sasa kijana kawa kama amechanganyikiwa , anaomba familia ikae ili aombe msamaha.

Kaka yangu ambaye tunashare baba ameoa mwanamke ambaye mama yake ni mganga, hela za pension zimeliwa zote, sasa hivi yupo ndio wanamtumia kwenda kuchimba dawa huko Kilosa. Kukitokea shida nyumbani hadi anachangiwa nauli. Alikuwa mhasibu.

Nikichojifunza ni kwamba, ingawa mapenzi ni ya watu wa 2, wakati mwingine wazazi nao wanaona mbali. Sidhani kwamba kuna mzazi ambaye anamkatalia mwanae asiyekuwa mtu sahihi kwa sababu sizizo na mashiko, ingawa wako wachache ambao huwa hawana sababu za msingi.
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Anaweza akakataa mzee kumbe alikua demu wake.
 
Back
Top Bottom