#COVID19 Chanjo ya COVID-19: Watanzania hatujawahi kuchomwa chanjo kwa kujaza fomu kuiepusha Serikali na lawama za madhara

nokwenumuya

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2019
Posts
820
Reaction score
2,896
Leo katika uzinduzi wa chanjo. Waziri wa Afya kaongea mambo mengi ili kuhalalisha mchakato huo.

Ameenda mbali na kushawishi watu kuwa kujaza fomu ya kuridhia kuchanjwa ambayo inasema ukipata madhara serikali haitawajibika ni jambo la kawaida kitabibu na hata ukifanyiwa operation basi wewe au ndugu zako watasaini kwa niaba yako.

Mfano aliotoa hauendani kabisa na utolewaji wa chanjo. Mathalani tumekuwa tukipata chanjo toka tukiwa watoto wadogo lakini hatujawahi jaza fomu za aina hiyo hata siku moja.

Vilevile kama serikali imejiridhisha kuwa hizo chanjo ni salama. Na wao ndio wamezipokea na kutudunga na kwa kuwa wao ndio wana wataalam na maabara kwanini wanaogopa kuwajibika na madhara yanayoweza kujitokeza?
 
Taja mfano wa nchi yoyote ambayo chanjo za majaribio za dharula za covid-19 zinachomwa kwa lazima?
 
Hii chanjo ipo kwenye pilot stage. No wonder Serikali haitaki kuhusika na potential consequences. Na ndio maana wamesisitiza kwamba kwenda kuchomwa ni hiari. Wanaotaka kuchoma waende tu bila kuwatisha wanaoipinga.
 
Ukiwaona sasa wanasiasa wanavyoishabikia chanjo nikama wametengeneza wao kwenye ofis zao za ccm, mbaya zaid kuna wale wakina fulan ambao hawana ujuz wowote, wala uelewa wowote kuhusu chanjo, lkn ukiwakuta wanavyozishabikia[emoji44][emoji44][emoji44]..kwa hili watanzania kama izo chanjo ztakuwa na athari basi watakao athirika ni wale bendera fuata upepo, maana ku a watu wamejazwa upepo na wanasiasa kwa kuona kila liletwalo na mzungu ni zuri, ukiwapinga wanakuita mjinga mara sukuma geng [emoji23][emoji23][emoji23].....tutaona soon
 
Zamani tulikuwa tunalazimishwa, watoto wa shule walishikwa kwa lazima ili kuchanjwa!. Zama hizo zimepitwa na wakati, sasa wananchi wana uelewe na ndiyo maana wanapewa choice
 
Zamani tulikuwa tunalazimishwa, watoto wa shule walishikwa kwa lazima ili kuchanjwa!. Zama hizo zimepitwa na wakati, sasa wananchi wana uelewe na ndiyo maana wanapewa choice
Hizo chanjo za zama hizo zilipitia hatua zote za majaribio na kupata muda wa kutosha wa kufanyiwa utafiti.....hizi za covid ni mradi wa watu wanaotafuta kutajirika kwa haraka sana!
 
 
Ipo hivi, hiyo ni experimental vaccine maana yake bado ipo kwenye majaribio. Kimsingi kama chanjo bado ipo kwenye hatua za majaribio watafiti na wale watu waliowapa mafunzo ndo watahusika na hayo majaribio. Ikiwa ni pamoja na kutafuta watu watakaohusika na majaribio, kuwaeleza kila kitu kuhusiana na hayo majaribio ikiwa ni pamoja na madhara yanayoweza kujitokeza na namna ya kukabiliana nayo au kuweza kuwapa taarifa watafiti wafuatilie na kutoa msaada wowote, hii inaitwa (informed consent) maana yake mtu anatoa ridhaa baada ya kueleweshwa kila kitu kuhusiana na majaribio bila kuficha. Kiini macho kinachoendelea kwenye hii chanjo ya majaribio ni kwamba;​

1. Serikali ndo ipo mstari wa mbele kuhamasisha huku watafiti wakiwa wamejificha nyuma ya pazia.
2. Fomu ya ridhaa (consent form) haina maelezo yoyote kuhusiana na majaribio yanayofanyika na madhara yanayoweza kujitokeza na namna watafiti watakavyohusika kusaidia endapo mtu atapata madhara.
3. Utaratibu wa kuingiza wahusika (recruitment process) haujawahi kutokea wakati wowote kuhusisha zaidi ya watu bilioni moja dunia nzima kwenye hatua za awali za majaribio ya dawa au chanjo. Hatua za awali hutakiwa kuhusisha watu wachache angalau elf 40 na kuwafuatilia kwa angalau miaka 10.
4. Majaribio kama hayo huhusisha kulipa fidia kwa waliojitolea kuhusika, lakini hapa tunaona majaribio yanafanyika bwerere bila fidia yoyote.
Kwa hiyo utaona haya majaribio yamevunja maadili ya kitafiti (Gross violation of research ethics and code of conduct in human subjects). Mwisho kabisa nasema kazi iendelee.......
 
Hii chanjo ipo kwenye pilot stage. No wonder Serikali haitaki kuhusika na potential consequences. Na ndio maana wamesisitiza kwamba kwenda kuchomwa ni hiari. Wanaotaka kuchoma waende tu bila kuwatisha wanaoipinga.
Nimekupata vema kwa lugha iliyojificha ni kwamba waliotayari kushiriki majaribio wachanjwe lol.
 
Viongozi wanajua ukweli Ila Mungu atawavua nguo tu.
 
Nimechoma chajo ya tetanus hivi karibuni lakini sikujazishwa hizo form, kwa nini hii ya corona tujaze hizo consent form?
Hapa Kuna kitu tu
 
Kama una wasiwasi acha kuchanja. Usituletee upuu wako hapa!
 
Acha uongo. Hakuna chanjo inayotelewa bila form/kadi. Hata dawa za kawaida zina kadi. Hata za Ukimwi zinatolewa kwa kadi. Clinic kama mtoto hana kadi hapewi chanjo. Ndo form hizo
 
Acha uongo. Hakuna chanjo inayotelewa bila form/kadi. Hata dawa za kawaida zina kadi. Hata za Ukimwi zinatolewa kwa kadi. Clinic kama mtoto hana kadi hapewi chanjo. Ndo form hizo
Huu ni uongo, chanjo ya tetanus hujazi form. Hata hizi tunazowapeleka Watoto wachanjwe hakuna form tunajaza. ACHA UONGO
 
WENDA lalamiko lako likawa sawa, Kutokana na serikali kufanya vitu kishamba, kumjazisha mwananchi form ya na namna hii kwenye chanjo na ukalinganisha na kiapo KWa mgonjwa kufanyiwa surgery sio sawa

KWa kifupi kila chanjo na batch ya chanjo yoyote ile huja na form ambazo hujazwa na watoa huduma pale waonapo batch flani may be unaleta madhala Kama reaction n.k , na kuwakilishwa KWa utaratibu mahalum ili kuchukua hatua , Sasa hii sarakasi ya serikali hii inaanza tia mashaka wananchi
 
Sasa wanaposema wamejiridhisha kuwa chanjo ni salama halafu hapo wameweka form ya kujitoa na lawama ukipata madhara kwenye hizo chanjo sijui hiyo inakuwa na maana gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…