nokwenumuya
JF-Expert Member
- Jun 29, 2019
- 820
- 2,896
Leo katika uzinduzi wa chanjo. Waziri wa Afya kaongea mambo mengi ili kuhalalisha mchakato huo.
Ameenda mbali na kushawishi watu kuwa kujaza fomu ya kuridhia kuchanjwa ambayo inasema ukipata madhara serikali haitawajibika ni jambo la kawaida kitabibu na hata ukifanyiwa operation basi wewe au ndugu zako watasaini kwa niaba yako.
Mfano aliotoa hauendani kabisa na utolewaji wa chanjo. Mathalani tumekuwa tukipata chanjo toka tukiwa watoto wadogo lakini hatujawahi jaza fomu za aina hiyo hata siku moja.
Vilevile kama serikali imejiridhisha kuwa hizo chanjo ni salama. Na wao ndio wamezipokea na kutudunga na kwa kuwa wao ndio wana wataalam na maabara kwanini wanaogopa kuwajibika na madhara yanayoweza kujitokeza?