#COVID19 Chanjo ya korona ni salama. Wazungu wangetaka kutuua wangetuua kwenye chanjo za surua, polio na pepopunda

Madam chopra

Member
Joined
Jul 27, 2021
Posts
5
Reaction score
48
CHANJO YA KORONA NI SALAMA, UKIDHARAU YATAKUPATA MADHARA, TUSIAMINI UZUSHI, TUSIKILIZE WATAALAMU WA AFYA. WAZUNGU WANGETAKA KUTUUA WANGETUUA KWENYE CHANJO ZA SURUA,POLIO NA PEPOPUNDA.

Ni siku ya jumapili tulivu, Mimi na mdogo wangu aitwae Maria tumekaa barazani tunapunga upepo mwanana. Ghafla tunasikia sauti ya kipaza sauti kikitangaza ugonjwa mbaya ulioingia nchini umepatiwa chanjo. Nilimtazama Maria kwa hofu na kumuambia tuingie ndani haraka kwa sababu wazazi wetu walikua hawajarejea nyumbani kwasababu siku ya jumapili wanapendelea kushinda kanisani mpaka jioni. Tulipoingia ndani, tukawasha luninga(TV) taarifa tuliyokutana nayo Ni ileile CHANJO YA KORONA YAINGIA NCHINI.

Saa moja usiku wazazi walirejea wakiwa na nyuso zisizoonesha dalili ya furaha tofauti na siku nyingine. Mama akaita Neema nikaitika (Abee!) Akaniambia tuandae chakula mezani ili tupate mlo wa usiku. Nikiwa naandaa chakula nikamsikia baba na mama wakisema " Hawa wazungu wanataka kutuua" Muda mchache baadae tulikula na kufanyia maombi kisha tukalala. Siku ilyofuata tuliamka asubuhi na mapema tukaelekea shule pamoja na mama yetu ambaye ni mwalimu shule tunayosoma. Tulisoma na baadae tulirudi nyumbani.

Wiki moja baadae tukiwa darasani kengele ili gongwa na wote tukatoka na kukusanyika, kila mmoja alikaa attention kusikiliza matangazo kwani sio jambo la kawaida kukusanyika saa tatu asubuhi tena muda mchache tu baada ya morning parade. Mwalimu mkuu akatangaza Kama ifuatavyo:
Mwalimu mkuu: Habari zenu wanafunzi?

Wanafunzi: Nzuri sir!
Mwl/mkuu: Nadhani Kila mmoja anataarifa juu ya huu ugonjwa ulioingia nchini na chanjo iliyopatikana?
Wanafunzi: Ndio mwalimu!

Mwl/mkuu: Sasa kutokana na kuwa unaenezwa kwa njia ya hewa pale ambapo mtu mwenye ugonjwa huo anapokohoa au kupiga chafya, kupeana mikono, kugusana na kugusa kitu au sehemu yenye virusi vya ugonjwa huo, inatubidi kuchukua tahadhari mapema.

Mwl/mkuu: Mnanielewa wanafunzi?
Wanafunzi: Ndio mwalimu
Mwl/mkuu: Ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo yatupasa kuzingatia mambo kadhaa
Kwanza; Osha mikono mara kwa mara angalau kwa sekunde ishirini (20). Pili; funika mdomo na pua kwa kiwiko cha mkono, kitambaa au tishu wakati unakohoa au kupiga chafya. Tatu; Epuka kupeana mikono na watu. Nne; Epuka safari zisizo za lazima. Tano; Epuka kugusa mdomo,pua na macho kabla ya kunawa mikono. Sita; Safisha mara kwa mara vitu unavyo vigusa. Saba; Tumia barakoa (mask) na takasa mikono kwa kutumia kieuzi (sanitaiza). Nane; Epuka mikusanyiko. Maelezo niliyo wapatia mzingatie na kuelimisha jamii zenu, mmeelewa?

Wanafunzi: Ndio mwalimu
Mwl/mkuu: Nina zawadi nataka kumpa mwanafunzi mmoja anaejiamini, mpo tayari?
Wanafunzi: Ndio tupo tayari
Mwl/mkuu:wanaojiamini waje mbele niwaulize swali, atakayejibu vizuri nitampa hii zawadi…

Walijitokeza wanafunzi waatano na wakaulizwa swali hili “je katikati yetu tunazingatia njia za kujikinga na gonjwa hili”? Wanafunzi watatu wakajibu ndio tunazingatia lakini wale wawili wakajibu hapana. Mwalimu mkuu akawauliza kwanini mmesema hapana? Wakajibu hivi;

Mwanafunzi wa Kwanza (Omondi): Hapana hatuzingatii hizo kanuni za kujikinga kwa sababu nchini tumeshaombea huo ugonjwa hivyo hakuna haja ya kuogopa.
Mwanafunzi wa pili (Wamboi): Hapana hatuzingatii kwa sababu hatukuwa na elimu ya kujikinga na mwalimu umetuelimisha ila bado tumekuasanyika hapa, hatujavaa barakoa, kama kuna aliye na ugonjwa kati yetu tutaambukizwa kwa wingi.
Mwl/mkuu: Vizuri Sana Wamboi umejibu vizuri unastahili zawadi hii.
Mwalimu mkuu akampa zawadi kisha akatutangazia alichotuitia:

Mwl/mkuu: Ninaomba niwape elimu ambayo nanyi mtaitoa kwa familia na jamii zenu juu ya umuhimu wa chanjo hii iliyoletwa nchini. Kwanza, niwatoe hofu, chanjo hii haijaletwa nchini kwa madhumuni ya kuua raia wake, hakuna nchi ambayo viongozi watakua mfano wa kuchanjwa alafu waue raia wake. Hayo ni maneno ya uzushi myapuuze.

Vilevile, Msiamini wanaopotosha kwa kusema Wazungu hawatupendi wanataka kutuua, kila mmoja amechanjwa chango mbalimbali kama vile chanjo ya polio, surua, pepopunda, n.k wangetaka kutuua wangeweza kupitia chanjo hizo wala wasingepoteza muda kusubiri korona. Pia vifaa tiba na madawa mbalimbali yanatoka kwa hao tunaowaita mabeberu na zimekua zikitusaidia hivyo basi niwatoe hofu.

Pia msihofu kuhusu madhara yanayokomaliwa na wapinzani wa chanjo hii, kila dawa ina maudhi madogomadogo lakini ufanisi na faida ni kubwa kuliko hayo maudhi yake na madhara yanayojitokeza.

Muda uliotumika kupata chanjo ni mchache ndio, miaka miwili, lakini muda wa kupatikana chanjo sio kipimo cha ubora kwasababu wataalamu wapo na wanataka kuokoa maisha lazima wapambane kuharakisha upatikanaji wa chanjo na sio kusubiri miaka ipite, watu wapoteze maisha ndio wazitoe ili kuridhisha wanaoamini kutumia muda mwingi katika maandalizi ndio ubora wa kitu.

Chanjo za Africa sio za ulaya, wanafunzi wangu wazuri tusichunguze sana mambo wakati hatujiwezi ata kama zikiwa na utofauti kidogo cha muhimu ni ufanisi katika kazi. Na kwanini watupe feki? Ili iweje, tofauti labda ni package tu, msiwe na hofu.
Chanjo ni hiyari ya mtu sio lazima. Kwa upendo kabisa chanjo hailazimishwi inatolewa kwa hiyari tena ni bure kabisa. Kwa awamu ya kwanza zimekuja chanjo kiasi na zitatolewa kwa makundi yaliyoainishwa (watumishi sekta ya afya, wenye maradhi, wenye umri mkubwa n.k) hao ndio kipaumbele wengine tukiendelea kusubiri chanjo zinazokuja. Kama ilivyo ARVs zinatolewa bure na chanjo ya koviko ni bure kabisa, tusiwe na mawazo potofu. Baada ya kusema haya naomba mkawe mabalozi wazuri katika kutoa elimu kwenye familia zenu, kwa sababu chanjo ni muhimu kwa usalama wa afya zetu.

Hata Raisi ameonesha uzalendo kwa Taifa na afya yake kwa kuchanjwa hadharani kabisa japo wazushi hawakosekani wanaodai amechomwa chanjo tofauti. Maneno ata kwenye kanga yapo! Tushukuru Mungu chanjo zimeletwa bure nchini maana zingekua za kufata nje ya nchi maskini wangeangamia. Tuendelee kumuomba Mungu lakini tusiache kuchukua tahadhari. Tuna imani na Mungu lakini majumbani kwetu tunatumia chandarua kujikinga na mbu waenezao malaria vivyohivyo kwenye korona tujikinge pamoja na imani zetu.

Mdogo wangu Maria alikuwa hapendi kuvaa barakoa na alikuwa anapenda sana kushiriki katika mikusanyiko kimichezo. Siku moja alipotea katika mazingira yasioelezeka,tulimtafuta kwa majirani lakini hatukumuona, usiku ulifika Maria hakua amerejea. Mama alipiga simu polisi station na kuwaeleza, polisi walimtafuta lakini mpaka usiku wa manane hakua amepatikana. Sikuweza kulala usingizi kutokana na kumuwaza mdogo wangu wa pekee, nilihofu sana na kujiuliza maswali, atakuwa wapi? ametekwa na magaidi? au ugonjwa umemkuta?sikupata majibu ya maswali yangu. Kwanini hakutii maagizo ya mama?? Kila mara alikua akitusihi tukitoka shule tutulie nyumbani mpaka hali itakapo kuwa shwari. Kwanini mdogo wangu amekua mkaidi? Niliumia sana moyo wangu, nililia lakini haikusaidia chochote.

Siku tatu baadae Maria alirejea nyumbani akiwa analia.Tulipomuona tulimkimbilia na kumkumbatia kwa furaha. Baba alimuhoji ni wapi alipokuwa? Akawa analia na kusema hajui alipokuwa ila alikuwa anatafuta watoto wa kuchezea nae na kila alipopita hakuona watoto wakizagaa ovyo mpaka akafika sehemu asiyoifahamu. Siku ya kwanza alilala kwenye kibanda kilichopo pembeni mwa barabara ya lami na njaa ilimuuma sana, siku ya pili alipita kwenye nyumba nzuri akaomba chakula wakampatia na kumuambia asubiri waite polisi ili arejeshwe nyumbani, alipo maliza kula akahofia polisi wangemuadhibu (kwani siku zote mama alikua akituonya endapo tutafanya kosa atatupeleka polisi kumbe jambo hili lilimuathiri mdogo wangu Maria) hivyo basi akatoroka na kuingia mtaani na leo kama bahati akajikuta maeneo ya mtaa tunaoishi ndipo akarudi nyumbani.
Tulilia kwa huzuni ilichanganyika na furaha. Maria akaomba msamaha na kisha akaoga na tukala tukalala. Siku mbili zilipita lakini Maria hakuwa mchangamfu alikua na homa wala hakuwa na hamu ya kula chakula, familia tukajua ni baridi iliyompiga ndio imesababisha awe na homa tukachukulia poa, hatukuwa na hisia yoyote juu ya ugonjwa huu mpya.

Jioni wakati tunamaliza kula tulisikia taarifa inaelezea dalili za ugonjwa huu mpya unao julikana kwa jina- Covid-19 (Corona)ni pamoja na homa inayozidi centgrade38 , kikohozi kubanwa na mbavu na kupumua kwa shida,vidonda kooni, kuchoka mwili kuumwa kichwani na maumuvu ya misuli. Ugonjwa huenea kwa njia ya majimaji yenye maambukizi yanatoka kwa njia ya hewa pale mtu anapokohoa kohoa, kupenga mafua, kupiga chafya, kugusana na mtu mwenye maambukizi au kugusa vitu venye maambukizi.
Pia habari ilieleza kuwa watu wote (wakiume kwa wa kike) wanaweza kudhurika na ugonjwa huo, wenye maradhi yanayoshusha kinga mwili huwa na hatari kubwa zaidi, wazee pia wapo katika hatari kubwa kupata huu ugonjwa ulioitwa korona (koviko) kwani wana kinga mwili hafifu.

Dalili karibu zote zilizotajwa Maria alikua nazo, mama alipata mshtuko na alimtazama baba!!! Nusu saa baadae Maria alikimbizwa hosipitali ili afanyiwe vipimo, majibu yalipotoka kwa bahati nzuri hakua na koviko bali malaria, alianzishiwa dozi na baada ya siku tati aliruhusiwa kurudi nyumbani.

Baba alikuwa mpinzani mkuu wa chanjo ya korona kabla hata haijafika nchini, aliamini ni mpango wa mabeberu kutuua ata alipokuwa kanisani alikua akikemea sana hiyo roho ya korona. Mama alimsihi sana baba wajisajili ili wapate chanjo lakini hakushaurika, mama akajisajili na kupatiwa chanjo. Siku si nyingi mzee baba akaanza kuumwa sukari ilipanda sana na presha ilikuwa juu. Akaendelea kutumia dawa zake lakini jioni ya jumamosi hali yake ulikuwa mvaya zaidi, mama akashirikiana na jirani kumpeleka hospitali. Baada ya vipimo alibainika ana korona, madaktari walimuwekea oksijeni ili imsaidie aweze kupumua lakini baada ya siku mbili baba alifariki na tukabaki yatima, mama akabaki mjane. Baba alizikwa maisha yakaendelea.. Ila siku zote majuto ni mjukuu na marehemu hajuti!

Siku zinasonga na mtindo wa maisha unabadilika, wananchi wamezoea kuvaa barakoa na wengi wanaobainika kuwa na ugonjwa wanapona. Nina imani hata watakaotumia chanjo itawasaidia hivyo kuna matumaini kiasi fulani. Ninawasihi wenzangu muwe na utii na msisikilize maneno ya wazushi bali wataalamu wa afya. Ninaumia kila nikimkumbuka baba yangu.

Vilevile tuendee kumuomba mungu atusaidie hili gonjwa la kovidi naitini (covid-19) (koviko) linalosababishwa na kirusi cha korona lipotee kabisa Ila tusisahau kuchukua tahadhari. Na tusidharau chanjo kama mwalimu wetu alivyotuelimisha. Tupambane na mitishamba lakini tusidharau sayansi.
Kwa heri.
 
Attachments

Kuna wengi sana hawajachanja chanjo yoyote kuanzia pepopunda, ndui, surua sijui takataka za vitamin A na bado wanadunda mitaaani

Wengi wanaotumia ARVs wanakufa kwa matatizo ya Figo na Ini halafu kuna Jitu linasema wangetaka kutuua wangetuua, halijiulizi hizi case za Cancer, figo,Ini, chanzo chake ni nini kama sio ma dawa yao

Hata ARV zinazoletwa Africa sio zile wanazotumia wao the same to Fertilizers.

Kitisho chetu huku uswekeni ni njaa sio Corona na kama kuna chanjo walete ya ku boost mifuko yetu
 
wagonjwa wa,
1.KISUKARI
2.PRESHA
3.MOYO
4.SARATANI
5.UKIMWI
wagonjwa wa maradhi hayo wanapaswa wachue tahadhari sana maana Corona itatumaliza sana.
 
Kipindi cha nyuma dunia ilikuwa inaokoa maisha ya binadamu ili wasiangamie kwa polio, pepo punda, surua n.k., lakini kwa sasa wenye uwezo wanaangamiza wenzao kwa kigezo cha kupunguza idadi ya watu duniani; kisa hakuna chakula, maji ya kutosha kulisha watu bilioni 7+. Na walengwa zaidi ni watu weusi hata Raisi mstaafu wa Marekani Obama alituambia miaka ya hivi karibuni.
Mungu ndiye aliyetuumba na kama tumezidi anajua cha kufanya.
 
CHANJO YA KORONA NI SALAMA, UKIDHARAU YATAKUPATA MADHARA, TUSIAMINI UZUSHI, TUSIKILIZE WATAALAMU WA AFYA. WAZUNGU WANGETAKA KUTUUA WANGETUUA KWENYE CHANJO ZA SURUA,POLIO NA PEPOPUNDA.

Ni siku ya jumapili tulivu, Mimi na mdogo wangu aitwae Maria tumekaa barazani tunapunga upepo mwanana. Ghafla tunasikia sauti ya kipaza sauti kikitangaza ugonjwa mbaya ulioingia nchini umepatiwa chanjo. Nilimtazama Maria kwa hofu na kumuambia tuingie ndani haraka kwa sababu wazazi wetu walikua hawajarejea nyumbani kwasababu siku ya jumapili wanapendelea kushinda kanisani mpaka jioni. Tulipoingia ndani, tukawasha luninga(TV) taarifa tuliyokutana nayo Ni ileile CHANJO YA KORONA YAINGIA NCHINI.

Saa moja usiku wazazi walirejea wakiwa na nyuso zisizoonesha dalili ya furaha tofauti na siku nyingine. Mama akaita Neema nikaitika (Abee!) Akaniambia tuandae chakula mezani ili tupate mlo wa usiku. Nikiwa naandaa chakula nikamsikia baba na mama wakisema " Hawa wazungu wanataka kutuua" Muda mchache baadae tulikula na kufanyia maombi kisha tukalala. Siku ilyofuata tuliamka asubuhi na mapema tukaelekea shule pamoja na mama yetu ambaye ni mwalimu shule tunayosoma. Tulisoma na baadae tulirudi nyumbani.

Wiki moja baadae tukiwa darasani kengele ili gongwa na wote tukatoka na kukusanyika, kila mmoja alikaa attention kusikiliza matangazo kwani sio jambo la kawaida kukusanyika saa tatu asubuhi tena muda mchache tu baada ya morning parade. Mwalimu mkuu akatangaza Kama ifuatavyo:
Mwalimu mkuu: Habari zenu wanafunzi?

Wanafunzi: Nzuri sir!
Mwl/mkuu: Nadhani Kila mmoja anataarifa juu ya huu ugonjwa ulioingia nchini na chanjo iliyopatikana?
Wanafunzi: Ndio mwalimu!

Mwl/mkuu: Sasa kutokana na kuwa unaenezwa kwa njia ya hewa pale ambapo mtu mwenye ugonjwa huo anapokohoa au kupiga chafya, kupeana mikono, kugusana na kugusa kitu au sehemu yenye virusi vya ugonjwa huo, inatubidi kuchukua tahadhari mapema.

Mwl/mkuu: Mnanielewa wanafunzi?
Wanafunzi: Ndio mwalimu
Mwl/mkuu: Ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo yatupasa kuzingatia mambo kadhaa
Kwanza; Osha mikono mara kwa mara angalau kwa sekunde ishirini (20). Pili; funika mdomo na pua kwa kiwiko cha mkono, kitambaa au tishu wakati unakohoa au kupiga chafya. Tatu; Epuka kupeana mikono na watu. Nne; Epuka safari zisizo za lazima. Tano; Epuka kugusa mdomo,pua na macho kabla ya kunawa mikono. Sita; Safisha mara kwa mara vitu unavyo vigusa. Saba; Tumia barakoa (mask) na takasa mikono kwa kutumia kieuzi (sanitaiza). Nane; Epuka mikusanyiko. Maelezo niliyo wapatia mzingatie na kuelimisha jamii zenu, mmeelewa?

Wanafunzi: Ndio mwalimu
Mwl/mkuu: Nina zawadi nataka kumpa mwanafunzi mmoja anaejiamini, mpo tayari?
Wanafunzi: Ndio tupo tayari
Mwl/mkuu:wanaojiamini waje mbele niwaulize swali, atakayejibu vizuri nitampa hii zawadi…

Walijitokeza wanafunzi waatano na wakaulizwa swali hili “je katikati yetu tunazingatia njia za kujikinga na gonjwa hili”? Wanafunzi watatu wakajibu ndio tunazingatia lakini wale wawili wakajibu hapana. Mwalimu mkuu akawauliza kwanini mmesema hapana? Wakajibu hivi;

Mwanafunzi wa Kwanza (Omondi): Hapana hatuzingatii hizo kanuni za kujikinga kwa sababu nchini tumeshaombea huo ugonjwa hivyo hakuna haja ya kuogopa.
Mwanafunzi wa pili (Wamboi): Hapana hatuzingatii kwa sababu hatukuwa na elimu ya kujikinga na mwalimu umetuelimisha ila bado tumekuasanyika hapa, hatujavaa barakoa, kama kuna aliye na ugonjwa kati yetu tutaambukizwa kwa wingi.
Mwl/mkuu: Vizuri Sana Wamboi umejibu vizuri unastahili zawadi hii.
Mwalimu mkuu akampa zawadi kisha akatutangazia alichotuitia:

Mwl/mkuu: Ninaomba niwape elimu ambayo nanyi mtaitoa kwa familia na jamii zenu juu ya umuhimu wa chanjo hii iliyoletwa nchini. Kwanza, niwatoe hofu, chanjo hii haijaletwa nchini kwa madhumuni ya kuua raia wake, hakuna nchi ambayo viongozi watakua mfano wa kuchanjwa alafu waue raia wake. Hayo ni maneno ya uzushi myapuuze.

Vilevile, Msiamini wanaopotosha kwa kusema Wazungu hawatupendi wanataka kutuua, kila mmoja amechanjwa chango mbalimbali kama vile chanjo ya polio, surua, pepopunda, n.k wangetaka kutuua wangeweza kupitia chanjo hizo wala wasingepoteza muda kusubiri korona. Pia vifaa tiba na madawa mbalimbali yanatoka kwa hao tunaowaita mabeberu na zimekua zikitusaidia hivyo basi niwatoe hofu.

Pia msihofu kuhusu madhara yanayokomaliwa na wapinzani wa chanjo hii, kila dawa ina maudhi madogomadogo lakini ufanisi na faida ni kubwa kuliko hayo maudhi yake na madhara yanayojitokeza.

Muda uliotumika kupata chanjo ni mchache ndio, miaka miwili, lakini muda wa kupatikana chanjo sio kipimo cha ubora kwasababu wataalamu wapo na wanataka kuokoa maisha lazima wapambane kuharakisha upatikanaji wa chanjo na sio kusubiri miaka ipite, watu wapoteze maisha ndio wazitoe ili kuridhisha wanaoamini kutumia muda mwingi katika maandalizi ndio ubora wa kitu.

Chanjo za Africa sio za ulaya, wanafunzi wangu wazuri tusichunguze sana mambo wakati hatujiwezi ata kama zikiwa na utofauti kidogo cha muhimu ni ufanisi katika kazi. Na kwanini watupe feki? Ili iweje, tofauti labda ni package tu, msiwe na hofu.
Chanjo ni hiyari ya mtu sio lazima. Kwa upendo kabisa chanjo hailazimishwi inatolewa kwa hiyari tena ni bure kabisa. Kwa awamu ya kwanza zimekuja chanjo kiasi na zitatolewa kwa makundi yaliyoainishwa (watumishi sekta ya afya, wenye maradhi, wenye umri mkubwa n.k) hao ndio kipaumbele wengine tukiendelea kusubiri chanjo zinazokuja. Kama ilivyo ARVs zinatolewa bure na chanjo ya koviko ni bure kabisa, tusiwe na mawazo potofu. Baada ya kusema haya naomba mkawe mabalozi wazuri katika kutoa elimu kwenye familia zenu, kwa sababu chanjo ni muhimu kwa usalama wa afya zetu.

Hata Raisi ameonesha uzalendo kwa Taifa na afya yake kwa kuchanjwa hadharani kabisa japo wazushi hawakosekani wanaodai amechomwa chanjo tofauti. Maneno ata kwenye kanga yapo! Tushukuru Mungu chanjo zimeletwa bure nchini maana zingekua za kufata nje ya nchi maskini wangeangamia. Tuendelee kumuomba Mungu lakini tusiache kuchukua tahadhari. Tuna imani na Mungu lakini majumbani kwetu tunatumia chandarua kujikinga na mbu waenezao malaria vivyohivyo kwenye korona tujikinge pamoja na imani zetu.

Mdogo wangu Maria alikuwa hapendi kuvaa barakoa na alikuwa anapenda sana kushiriki katika mikusanyiko kimichezo. Siku moja alipotea katika mazingira yasioelezeka,tulimtafuta kwa majirani lakini hatukumuona, usiku ulifika Maria hakua amerejea. Mama alipiga simu polisi station na kuwaeleza, polisi walimtafuta lakini mpaka usiku wa manane hakua amepatikana. Sikuweza kulala usingizi kutokana na kumuwaza mdogo wangu wa pekee, nilihofu sana na kujiuliza maswali, atakuwa wapi? ametekwa na magaidi? au ugonjwa umemkuta?sikupata majibu ya maswali yangu. Kwanini hakutii maagizo ya mama?? Kila mara alikua akitusihi tukitoka shule tutulie nyumbani mpaka hali itakapo kuwa shwari. Kwanini mdogo wangu amekua mkaidi? Niliumia sana moyo wangu, nililia lakini haikusaidia chochote.

Siku tatu baadae Maria alirejea nyumbani akiwa analia.Tulipomuona tulimkimbilia na kumkumbatia kwa furaha. Baba alimuhoji ni wapi alipokuwa? Akawa analia na kusema hajui alipokuwa ila alikuwa anatafuta watoto wa kuchezea nae na kila alipopita hakuona watoto wakizagaa ovyo mpaka akafika sehemu asiyoifahamu. Siku ya kwanza alilala kwenye kibanda kilichopo pembeni mwa barabara ya lami na njaa ilimuuma sana, siku ya pili alipita kwenye nyumba nzuri akaomba chakula wakampatia na kumuambia asubiri waite polisi ili arejeshwe nyumbani, alipo maliza kula akahofia polisi wangemuadhibu (kwani siku zote mama alikua akituonya endapo tutafanya kosa atatupeleka polisi kumbe jambo hili lilimuathiri mdogo wangu Maria) hivyo basi akatoroka na kuingia mtaani na leo kama bahati akajikuta maeneo ya mtaa tunaoishi ndipo akarudi nyumbani.
Tulilia kwa huzuni ilichanganyika na furaha. Maria akaomba msamaha na kisha akaoga na tukala tukalala. Siku mbili zilipita lakini Maria hakuwa mchangamfu alikua na homa wala hakuwa na hamu ya kula chakula, familia tukajua ni baridi iliyompiga ndio imesababisha awe na homa tukachukulia poa, hatukuwa na hisia yoyote juu ya ugonjwa huu mpya.

Jioni wakati tunamaliza kula tulisikia taarifa inaelezea dalili za ugonjwa huu mpya unao julikana kwa jina- Covid-19 (Corona)ni pamoja na homa inayozidi centgrade38 , kikohozi kubanwa na mbavu na kupumua kwa shida,vidonda kooni, kuchoka mwili kuumwa kichwani na maumuvu ya misuli. Ugonjwa huenea kwa njia ya majimaji yenye maambukizi yanatoka kwa njia ya hewa pale mtu anapokohoa kohoa, kupenga mafua, kupiga chafya, kugusana na mtu mwenye maambukizi au kugusa vitu venye maambukizi.
Pia habari ilieleza kuwa watu wote (wakiume kwa wa kike) wanaweza kudhurika na ugonjwa huo, wenye maradhi yanayoshusha kinga mwili huwa na hatari kubwa zaidi, wazee pia wapo katika hatari kubwa kupata huu ugonjwa ulioitwa korona (koviko) kwani wana kinga mwili hafifu.

Dalili karibu zote zilizotajwa Maria alikua nazo, mama alipata mshtuko na alimtazama baba!!! Nusu saa baadae Maria alikimbizwa hosipitali ili afanyiwe vipimo, majibu yalipotoka kwa bahati nzuri hakua na koviko bali malaria, alianzishiwa dozi na baada ya siku tati aliruhusiwa kurudi nyumbani.

Baba alikuwa mpinzani mkuu wa chanjo ya korona kabla hata haijafika nchini, aliamini ni mpango wa mabeberu kutuua ata alipokuwa kanisani alikua akikemea sana hiyo roho ya korona. Mama alimsihi sana baba wajisajili ili wapate chanjo lakini hakushaurika, mama akajisajili na kupatiwa chanjo. Siku si nyingi mzee baba akaanza kuumwa sukari ilipanda sana na presha ilikuwa juu. Akaendelea kutumia dawa zake lakini jioni ya jumamosi hali yake ulikuwa mvaya zaidi, mama akashirikiana na jirani kumpeleka hospitali. Baada ya vipimo alibainika ana korona, madaktari walimuwekea oksijeni ili imsaidie aweze kupumua lakini baada ya siku mbili baba alifariki na tukabaki yatima, mama akabaki mjane. Baba alizikwa maisha yakaendelea.. Ila siku zote majuto ni mjukuu na marehemu hajuti!

Siku zinasonga na mtindo wa maisha unabadilika, wananchi wamezoea kuvaa barakoa na wengi wanaobainika kuwa na ugonjwa wanapona. Nina imani hata watakaotumia chanjo itawasaidia hivyo kuna matumaini kiasi fulani. Ninawasihi wenzangu muwe na utii na msisikilize maneno ya wazushi bali wataalamu wa afya. Ninaumia kila nikimkumbuka baba yangu.

Vilevile tuendee kumuomba mungu atusaidie hili gonjwa la kovidi naitini (covid-19) (koviko) linalosababishwa na kirusi cha korona lipotee kabisa Ila tusisahau kuchukua tahadhari. Na tusidharau chanjo kama mwalimu wetu alivyotuelimisha. Tupambane na mitishamba lakini tusidharau sayansi.
Kwa heri.
Teknologies zina enda na kuongezeka. Sasa kuunda kitu uunde na atidote yake siii kazi ndogo
 
We madam umetumwa? Acha hizo mambo, kama umechanja kila la kheri kwenye safari yako
IMG-20220111-WA0004.jpg
 
Back
Top Bottom