Watoto wa shule ya msingi jijini Mbeya wamepata matatizo ya kiafya ikiwemo kuumwa tumbo na kutapika na wengine kufaliki baada ya kupewa chanjo ya vidonge kwa ajili ya minyoo na kichocho.
Miongoni mwa mwanafunzi aliyefaliki ni mwanafunzi wa kike mwenye miaka minne aliyekuwa anasoma Shule ya Msingi Uhuru iliyopo Kata ya Mwakibete jijini Mbeya, aliyefariki tarehe 25-04-2026 asubuhi.
Kufariki kwa mwanafunzi huyu kulitokana na uzembe wa watoa huduma hii ya chanjo kwa kutowapa elimu ya kutosha walimu waliokuwa wakitoa chanjo na kupelekea kuzidisha dozi kwa wanafunzi wengi kwa kuwa walimu walikuwa wakipima urefu pekee na sio uzito wa mwanafunzi, mwanafunzi huyu wa miaka minne alipewa vidonge viwili na nusu na wakati huo wanafunzi hawa walikuwa hawajapata chakula cha kutosha japokuwa wazazi walichangishwa shilingi 1,500 kwa ajili ya chakula cha wanafunzi wakati wa chanjo.
Wazazi wa mwanafunzi aliyefariki walikwenda tarehe 25-04-2026 kutoa taarifa kituo kikuu cha polisi pale Mjini na kutoa maelezo kwa polisi na baada ya hapo waliongozana na polisi kwenda hospitali ya binafsi ya UWATA ambapo mwanafunzi huyo wa miaka minne alifariki hapo akiwa anapatiwa matibabu, mwili wa mwanafunzi ulichukuliwa na kupelekwa hospitali ya Rufaa ya jiji la Mbeya kwa ajili ya uchunguzi ambapo sampuli zilichukuliwa kutoka kwenye mwili wa mwanafunzi na kupelekwa kwa mkemia mkuu kwa ajili ya vipimo.
Mwanafunzi huyu alikwisha pumzishwa tarehe 29-04-2026 na familia katika nyumba yake ya milele huku bado majibu kutoka kwa mkemia mkuu hayajatolewa mpaka sasa.
Kwa taarifa zinazoenea zinaeleza kuwa huyu si mwanafunzi pekee aliyefariki, inasadidika kuna wengine kutosha shule tofauti jijini Mbeya walipoteza maisha pia.