Mzeeba
Senior Member
- Sep 25, 2007
- 143
- 3
Was it a vaccine trial or normal immunization program (Expanded Programme on Immunization)?
Ni immunization program. imetangazwa kwa wiki nzima katika televisheni tofauti.
Kwa mkoa wa Dar es Salaam hili lilitokea wakati wa chanjo ya minyoo,watoto pia walizidiwa nguvu na dawa na kuzimia; wakasema tatizo ni watoto kutokula kabla ya chanjo.
Swali, iweje makosa hayo hayo yarudiwe na wizara hiyo hiyo, kwa chanjo hiyo hiyo? Hii itafanya watu waanze kukataa hizi program za chanjo na hivyo kuleta tatizo kubwa zaidi.
Naomba kuuliza mwalimu bila ruhusa ya mzazi ya maandishi anawezaje kuruhusu mtoto achanjwe? hili linanisumbua sana. Natambua walimu wanatusaidia sana katika kuwalea watoto wetu. Lakini hawana historia ya afya na matibabu ya watoto, sasa uamuzi huu unafikiwaje?
Na wizara nao wanachukulia kama wameshapewa ruhusa na wazazi kuchanja watoto... Hii si sawa kabisa.