#COVID19 Chanjo za corona zimehakikiwaje?

#COVID19 Chanjo za corona zimehakikiwaje?

Kivumishi Kielezi

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2019
Posts
1,028
Reaction score
2,451
Siku moja iliyopita, wazungu wametubwagia furushi la chanjo za misaada. Zinaitwa Johnson Johnson.

Furushi hilo lina chanjo milioni moja ambazo zinapaswa kudungwa chap chap. Na hivi kesho tu, Rais Samia anaenda kudungwa chanjo ya uhamasishaji.

Baada ya hofu kuwa kubwa kuhusu usalama wa hizo chanjo, wameibuka wanasiasa wakisema kwamba chanjo ni salama na zimehakikiwa na TFDA na wakemia wa serikali.

Mimi sio mkemia na sijui chochote kuhusu kemia. Kwanza hata sekondari sikusoma. Nilibangaiza bangaiza tu nikaishia shule ya msingi darasa la saba.

Ningependa kuwauliza hawa wanaoitwa "wataalamu wa UVIKO", Je, hilo furushi la chanjo limehakikiwa kwa methodolojia gani?

Kwa kuchukua sampuli chache na kuzihakiki? Au zote? Na kwa namna gani?

Kwa elimu yangu ya hii ya darasa la saba, ninaelewa kwamba, usalama wa chanjo unapimwa kwa MAJARIBIO YA UBORA (clinical trials) ambayo yanalenga kubaini athari za muda mrefu ama muda mfupi, na majaribio hayo yanaweza kuchukua angalau miaka mpaka mitano au zaidi.

Huyo mkemia anayetuambia kwamba amepima chanjo na kuona ziko salama ametumia njia gani haswa ya kisayansi?

Ghafla Bin Vuu tu ndani ya siku moja kaingia maabara na koti lake kakorokochoa test tubes, anatuambia chanjo ni salama? No trials?

Just mixing stuffs in test tubes, that's all?

Hiyo ndiyo sayansi ya Tanzania?

Mmezipimaje haswa hizo chanjo enyi wataalamu wa UVIKO?

Watanzania wana kiu ya kujua!
 
Heri Mimi Sijasema.👇👇

"Mimi sio mkemia na sijui chochote kuhusu kemia. Kwanza hata sekondari sikusomi. Nilibangaiza bangaiza tu nikaishia shule ya msingi darasa la saba".
 
Sasa mkuu unataka tukupitishe step by step au?

Na kama hukusoma nan alikuambia chanjo lazima ifanyiwa majaribio miaka 5+

Unajua technology iliyotumika ? Any way kama unataka kujua imehakikiwaje ni somo pana mana inabidi iwe step by step na hivyo either ugoogle tu au unilipe nije physically kukufundisha na kukupa michoro na baadhi ya practical zinazohusika

NB: Ni course kabisa hii
 
Muhimu ni ile form tu ukishajaza kukubali kuchanjwa basi hayo mengine ya kuwa ni salama au si salama hayana nafasi tena, na hata sielewi hao wanaosema wamehakiki na ni salama sijui ni usalama upi huo wanaouzungumzia.
 
Back
Top Bottom