Tetesi: Channel Ten hoi kifedha, mishahara yakosekana miezi miwili

Tetesi: Channel Ten hoi kifedha, mishahara yakosekana miezi miwili

Wadau hali ya kiuchumi kwa makampuni binafsi ni tete sana. Taarifa za kuaminika kutoka Channel Ten zinadai kuwa Hali ya kampuni hiyo ni mbaya na wafanyakazi wamekaa miezi miwili sasa bila mshahara.
Sababu za hali hiyo ni kushuka kwa mapato kutokana na makampuni makubwa kusitisha matangazo yao kutokana na ukata. Makampuni ya Mabango pia yanatajwa kuwa katika hali ngumu.
Hapo kwenye mabango ndo noma mkuu! anzia mjini mpaka bunju hakuna tangazo lolote kwenye bango yamebakia machuma tu
 
Channel 10 hata kama pesa ikiwepo matangazo yao ni kama kituo cha mafunzo kwa wanahabari.

Huwezi kuamini kama ni Kituo cha Runinga, yaani wana mzaha mwingi.
 
Wamekosa ubunifu mbona wenzao itv matangazo yanaongezeka mpaka inakuwa kero kwa watazamaji
 
Hii ndo channel ya ovyo kuliko zote nchi hii, Kazi kujikomba tu kila uchao. Wakaombe wanakopeleka mboga kila siku. Yaani niitwe niitwavyo lakini channel 10 kufa ni mojawapo kati ya maombi ambayo tukiambiwa tumuombee Fulani Mimi huwa naomba kifo cha channel 10.
TBC je?
 
Sasa si waongee na Humphrey POLEPOLE awatolee hela kwenye fungu la propaganda la CCM mana kipindi kile Polepole kila TV haitaki kumuona ila Channel 10 kwa uungwana wao walimchukua Polepole nasikia hadi wakampa na Chumba chake hapo Ch10
 
suala la mishahara kwa sasa sio channel ten tu,makampuni mengi sasa hivi yameyumba kimapato,sasa hivi kama unadai mshahara unaambiwa vumilia utalipwa tu,
 
unashangaa chanel 10??waulize Star tv wanadai zaidi ya Mwaka mmoja jamaa hashtakiki amashika hatamu anasubiri wajilipue.
Kwa star tv sishangai nasikia ni kawaida yao kulipwa mshahara tarehe 72....hahhahahahah
 
Katika Channel za TV za hovyo Channel Ten inaongoza yan hawapo makini kbs .. unakuta kipindi kinaendelea unasikia watu wanaongeleshana studio dah hata taarifa yao ya habari green screen yao ni ya hovyo mtu anaonekana wa kijani kbs .. wako so reckless kwa kila kitu sishangai hata DSTV wanaiachaga km free channel kifurushi kikikata coz wanajua hautagain chochote
 
Wadau hali ya kiuchumi kwa makampuni binafsi ni tete sana. Taarifa za kuaminika kutoka Channel Ten zinadai kuwa Hali ya kampuni hiyo ni mbaya na wafanyakazi wamekaa miezi miwili sasa bila mshahara.
Sababu za hali hiyo ni kushuka kwa mapato kutokana na makampuni makubwa kusitisha matangazo yao kutokana na ukata. Makampuni ya Mabango pia yanatajwa kuwa katika hali ngumu.
Lol....na ndoa zitayumba sasa vijana machinga watajibebea tu wake zetu kiulaini
 
Back
Top Bottom