JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Siku mbili tangu akaunti ya YouTube ya Diamond Platnumz iliporipotiwa kudukuliwa, akaunti hiyo imeondolewa na YouTube wenyewe kwa kilichoandikwa kuwa mtumiaji amekiuka masharti ya mtandao huo.
Inadaiwa kuwa baada ya kudukuliwa uongozi wa msanii huyo wa Bongo Fleva ulifanikiwa kuirejesha mikononi mwao lakini wadukuaji walirejea na kuanza kuichezea ndipo YouTube wakaamua kuifuta.
Mkuu wa Digital wa Wasafi afung
Ackim amesema: "Kutokana na Channel ya @diamondplatnumz kudukuliwa Jumapili iliyopita na wadukuzi kuingia Live. Leo Imezuiliwa na YouTube kutokana na maudhui yale kuvunja sheria za YouTube! Tumeshafanya mawasiliano ya awali kutatua tatizo hili. Tuendelee kuwa wavumilivu kila kitu kitakuwa sawa."