Channel ya YouTube ya Diamond Platnumz yafutwa (Terminated)

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607


Siku mbili tangu akaunti ya YouTube ya Diamond Platnumz iliporipotiwa kudukuliwa, akaunti hiyo imeondolewa na YouTube wenyewe kwa kilichoandikwa kuwa mtumiaji amekiuka masharti ya mtandao huo.

Inadaiwa kuwa baada ya kudukuliwa uongozi wa msanii huyo wa Bongo Fleva ulifanikiwa kuirejesha mikononi mwao lakini wadukuaji walirejea na kuanza kuichezea ndipo YouTube wakaamua kuifuta.

Mkuu wa Digital wa Wasafi afung
Ackim amesema: "Kutokana na Channel ya @diamondplatnumz kudukuliwa Jumapili iliyopita na wadukuzi kuingia Live. Leo Imezuiliwa na YouTube kutokana na maudhui yale kuvunja sheria za YouTube! Tumeshafanya mawasiliano ya awali kutatua tatizo hili. Tuendelee kuwa wavumilivu kila kitu kitakuwa sawa."
 
watakuwa ni team kiba & konde boy gang...
 
Zile nyimbo na views zote zile daaah
 
Tetesi , channel ya you tube ya diamond wamarekani wameipiga chini, hata ukienda kuitafuta Sasa hivi hutaipata.

Tetesi ni kuwa diamond ameviolate na amevunja Sheria na taratibu zote za you tube. Kisa ni kuiba view au view feki Sasa sijui Kama ni kweli au
 
Hivi huyo mnaemuita Diamond, ndio yulekijana aliye wahi kutoa tamko kwamba yeye ni kama maji.... usipo yaoga utayanywa, usipo yanywa utayapikia, usipo yapikia utayafulia, usipo yafulia utayajengea, usipo yajengea utayaoshea vyombo, gari nk
 
Kiki.
 
Usifikiri kila mtu anatabia kama za harmonize
 
Reactions: Qwy
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…