Channels nyingine za YouTube zinachekesha sana na kukatisha tamaa

Melki Wamatukio

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2022
Posts
6,156
Reaction score
10,974
Habari wakuu,

Inakatisha sana tamaa ndugu zanguni. Yaani unakuta channel imekuwa created miaka mitatu iliyopita, ina video kama nane hivi zenye length ya dakika 10 kila moja, contents unakuta ni nzuri tu, video ni HD 1080p, zina ng'aa sana, lakini unakuta video moja ina 276 views, iliyojitahidi sana ina 504 views, nyingine ina miezi sita lakini ina 3 views

Hii ina maana watu ndo wachawi na wanafiki? Ama YouTube hawaoni haja ya kuzifanyia recommendations? Au shida ni nini?

Mi ni YouTuber ambaye nategemea kuanzisha channel ya YouTube siku ya kesho na kuanza kutengeneza contents tofauti tofauti ili mwisho wa siku nianze kula maokoto, ila kwa hali hii, inakatisha sana tamaa

Mlioweza mliwezaje?
 
Channel ina miaka 3 alafu ina video nane unategemea nini.....! Kila kitu kinahitaji focus and Consistency
 
Dogo si ujishughulishe tu hata kabustani ka mbogamboga hapo uwani kwa dada/shemeji yako badala ya mayoutube.
Hapana mkuu, na mimi nataka nile huku nimekaa kwenye kiyoyozi kama wafanyavyo viongozi wa viti maalumu bungeni
 
Channel ina miaka 3 alafu ina video nane unategemea nini.....! Kila kitu kinahitaji focus and Consistency
Kwani mkuu, approximately ili channel iwe engaged more inahitaji videos ngapi per month?
 


Technical sana, kupost daily kuna influence kubwa
 
youtube inataka uvumilivu na consistency.
Cha kwanza wekeza kutafuta clicks. Hapo lazima uwekeze kwenye quality thumbnail na title za kibabe.

Ni kama biashara nyingine. Wanalima watu 100K matikini wanaotoboa ni 20.

Ifanye kama side hussle, usitangulize kupata pesa utakuwa frustrated.
Fanya kama hobby na fedha iwe matokeo. Tarehe 22 ndio siku ya kuokota pesa za mzungu wa Youtube. Kuna watu wanapiga pesa sana youtube.
 
Watu wamemaliza chuo 2012 hadi leo hawana kazi ili wewe halikushangazi..?
 
Watu wamemaliza chuo 2012 hadi leo hawana kazi ili wewe halikushangazi..?
Mi mwenyewe nimemaliza 2015 mpaka leo hii sijaajiriwa, kipindi hicho Rais Magu anapukutisha wafanyakazi, nilijua nafasi za kazi zitakuwa za kutosha

Kwa sasa tuachane na mambo ya kuajiriwa, twende tukajiajiri kwenye kampuni kubwa ya ulimwengu ya YouTube
 
Kwahyo unataka kila mtu ajiajiri youtube?
 
Youtube hamna maokoto kama watu wengi wanavyodhani na kuaminishwa.
 
Don't worry mkuu
Jack ma alitumia miaka 15 kuitengeneza alibaba na alikaa miaka mitatu bila kupata hata cent sio faida cent walikuwa wananunua vitu kwa wateje wanaoweka kwenye Alibaba hata kama ni scraps (stori yake ipo you tube kaangalie ).

Elon musk alitumia miaka 12 mpaka kufanikiwa kutengeneza kampuni yake ya space X mpaka wale wawekezaji walimwambia hii ndio mara ya mwisho kuweka hela kwenye kampuni yako na alifeli mara tatu mfulululizo (kaangalie ipo you tube).

Coca cola waliuza chupa 3 tu mwaka wao wakwanza kwenye biashara looks where are they today. (You tube).

Michael Jordan alikataliwa na mwalimu wake wa high school kwenye mchezo wa kikapu.

Don't give up failure is a condition not a person all successful people and companies takes time during their early stages of business from 10 to 12 years.

Even lionel messi was rejected by many clubs because of his height and physique don't worry all great things in the world takes time.

Alamsik
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…