Wajameni (hususani wanandoa) ni kitu cha kawaida wengi kukuta watu wamenuniana hatari yaani hawasemezan hata mwezi mzima, unakuta kuna ugomvi kati yao kwa ishu ndogo tu hasa wivu, kulea watoto, kazi,ndugu na kubamba sms/email za mchepuko.
binafs nimeshaexperiece minuno kadhaa unakuta wife amefanya kosa Fulani unaamuliza kistaarabu lakini atakavyo-react balaa hakubali kama alikosea bali hutafuta KUJITETEA kwa kumbushia makosa yangu ya zamani tukiwa wachumba. Hapo mim huwa kimyaaa ili niepushe hasira za kumshushia MAKONDE. Basi unafuata MNUNO hata wiki 3. Hebu tujuzane ikitokea umekutana na mnuno kwa mwenzi wako dawa ni nini?