Wajameni (hususani wanandoa) ni kitu cha kawaida wengi kukuta watu wamenuniana hatari yaani hawasemezan hata mwezi mzima, unakuta kuna ugomvi kati yao kwa ishu ndogo tu hasa wivu, kulea watoto, kazi,ndugu na kubamba sms/email za mchepuko.
binafs nimeshaexperiece minuno kadhaa unakuta wife amefanya kosa Fulani unaamuliza kistaarabu lakini atakavyo-react balaa hakubali kama alikosea bali hutafuta KUJITETEA kwa kumbushia makosa yangu ya zamani tukiwa wachumba. Hapo mim huwa kimyaaa ili niepushe hasira za kumshushia MAKONDE. Basi unafuata MNUNO hata wiki 3. Hebu tujuzane ikitokea umekutana na mnuno kwa mwenzi wako dawa ni nini?
Binafsi mpemdwa nimejifunza vitu fulani kwenye mahusiano ingawaje si mwanandoa ila naomba nichangie kiroho na kama nitakosea wajuaji ninaomba mnirekebishe please. Kitu cha kwanza kama couples never ,never go to bed mkiwa mmenuniana . Nikiimanisha kwamba pamoja na Yale yote mliyokoseana hebu jaribuni kuyaongelea mkiwa kitandani na muombane msamaha hata kama kosa lilikuwa si lako hebu humble kwa kuomba Radhi then sawazisheni kwa kumake up with more romantic......stuffs.
Hakuna kitu kibaya kama kukaaa na kinyongo, kulipizana visasi, kujiweka juu katika mahusiano, na sisemi hivi uwe mjinga no but sometimes we need to be listener and less talker kuepusha Shari.
Kwa sisi wanawake kuongea na kazi yetu, seriously sometime utakuta wapenzi wetu or mume zetu wametukwaza kidogo but we take it very big thing and saa nyingine we even tried to remind wapenzi wetu mambo ambayo yaliyopita tangu mwaka arobaini na saba, you why we do this? Because either hatulusamehe completely, ile kitu ilituuma sana to the point that haiwezi kutoka kabisa mioyoni mwetu au kile kitu mume au wapenzi wetu walivyotukosea Bado wanavifanya na vinatukwaza sisi.
Things to do tukiwa katika hali kama hizi ni:
Tujitahidi or tuweke msimamo wote as couples kuwa no matter what tusiende kitandani na hasira, kununa.
Just be happy a with the moment and take things easy without backfire us .
Msamaha, msamaha , tujitahidi kuwa wepesi Wa kuomba msamaha na kujifunza kitu kutoka kwenye ule msamaha tuliwaomba wenzetu.
Forgive , tunapoamua kumsamehe MTU / wapenzi/ mume/ mke tuwe willing kusafisha mioyo yetu na kuwa safi kwa kutokuweka kinyongo.
Tupeane maneno mazuri - tujifunze kupeana maneno mazuri na kutufanya wote kuwa tunafurahia kuwa pamoja.
Tukumbushane- hebu sometimes tujikumbushe kwa nini we fell in love with the person you / we are married or be with . Hii itatusaidia kuamsha hisia zilizopotea or sometimes even to get us more closer than before na kutufanya tusahau yale mabaya ya wapenzi wetu na kukumbuka Yale mazuri .
Share things - tujitahidi kuwafanya mume/ wapenzi/ wachumba more than they are . Tuwachukulie kama marafiki, best friend. Tujitahidi hata kama kuna vitu vinatusumbua instead ya kuviweka na kuvirundika moyoni ( hii tabia wanawake wengi tunayo, uwoga) mpaka siku wenzetu wakituudhi tunajibu kihasira, kukumbusha ya mwaka 47 au kujitetea hii ni mbaya. Hebu tuwe free kwa spouses, wachumba na wapenzi Kwani hii inasaidia pia kupunguza stress tulizo nazo or mizigo tuliyo nayo. Samahani kama nimekwenda siko. Kama kuna wengine please share nasi. Thanks.