Chanzo cha Mafuriko Morogoro mjini ni tuta la SGR, mamlaka zishughulikie hili

Ebale

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2016
Posts
943
Reaction score
1,683
Natamani ukweli huu uwafikie wafanya maamuzi. Kampuni ya Kituruki ya Yapi imeinua tuta kubwa na refu kwa ajili ya kupitisha reli ya SGR badala ya nguzo. Kisha wakaweka outlet mbili za kupitishia maji.

Matokeo yake tuta limekuwa likiyablock maji kutoka milima ya azimio na Lukobe kusambaa kwenye njia zake za asili na kuyakusanya yote na kupita kwenye outlet mbili walizozoelekeza kwenye makazi ya watu!

Hata kama mvua hainyeshi mjini imenyesha Milimani ni mafuriko mjini hasa maeneo ya Lukobe, Azimio, Manyuki na Kihonda!

Kuna maafa makubwa yanakuja! Barabara zote za maeneo haya zimekatika. Rais tafadhali unda tume ujiridhishe na ukweli huu. Hatua zichukuliwe.

Pia soma:Serikali: Watu 33 Wamefariki Kutokana na Mafuriko na Mvua Kubwa katika Mikoa ya Morogoro na Pwani
 
Bwawa la Mindu limejaa sana, na likijaa huwa linatema maji(overflow), likiyatema hayo maji ndio yanazagaa mitaani.

Kuna mpango wa kulitanua liwe kubwa zaidi.

SSH, kabla hajazindua treni ya umeme, kwanza aangalie athari za kimazingira za mradi wa reli hiyo (environmental impact assessment).

Haya mambo jiwe alikuwa anakataa kuyafanya, watu wanamshangilia
 
Ukijaza TUTA au KIFUSI unalipwa pesa kubwa zaidi kuliko kuweka NGUZO kama unavyoshauri, hawa watu walikua wanawaza kupiga hela zaidi kuliko usalama wa watu, umesema ukweli
 

Bwawa la mindu limejengwa na Magufuli?
 
Kwa nini watumie teknolojia ya kizamani ya ujenzi wa reli? tangu mkoloni bado yanajengwa matuta tu........

Kabla ya hilo tuta, mlima lukobe ulikuwa umetengeneza mkondo mkubwa wa maji ambao ulikuwa unapita kwenye maeneo ya makazi ya watu na kusababisha maji kutuama maeneo ya chini, sasa imagine hilo tuta lizuie huo mkondo hali inakuwaje.​
 
Jamani jamn kwani uhuru wanini ninahaki ya kwenda ama nisiende tusilazimishane vitu bhn🤣
 
Kuna Maafa makubwa yanakuja au yameshakuja hasa Jumamosi kuamkia Jumapili? Waambie hao Wanaoficha kuwa tunajua wa Kawaida kama 30 na wale wenye Dege lao Bovu la Mafunzo 13 waliokuwa katika Uokoaji hatunao tena Ulimwenguni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…