Chanzo kikuu cha matukio ya Oktoba 29 kinatokana na mkusanyiko wa malalamiko ya muda mrefu ya kijamii, kiuchumi na kisiasa ambayo yalikuwa yakijadiliwa waziwazi katika mitandao ya kijamii kwa muda mrefu kabla ya siku hiyo. Maandamano hayakuwa ya ghafla, bali yalipangwa na kujadiliwa kwa uwazi, jambo lililotoa fursa kwa viongozi wa Serikali na vyombo vya usalama kusikiliza, kuchambua, na kushughulikia madai ya wananchi mapema kwa njia ya kisheria na ya mazungumzo.
Hata hivyo, badala ya kuchukua hatua za kujenga na za kuzuia mgogoro, baadhi ya viongozi walibeza malalamiko hayo na kutoa kauli za kejeli dhidi ya vijana waliokuwa wakieleza hisia zao. Kauli hizo zilichochea hisia za kudharauliwa na kukosa kusikilizwa, hali iliyochangia vijana wengi kuona maandamano kama njia pekee ya kuwasilisha sauti zao.
Aidha, kutolewa kwa amri ya kutotoka nje (curfew) na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) kumeibua maswali makubwa ya kisheria. Kwa mujibu wa misingi ya sheria, jukumu la vyombo vya dola ni kulinda raia na kudumisha amani kwa kufuata sheria na taratibu, si kutoa amri zinazokinzana na sheria bila msingi wa kikatiba au kisheria unaoeleweka wazi. Tamko kwamba polisi na vyombo vingine “watakuwa na kazi maalumu” bila maelezo ya kisheria lilizidisha hofu na sintofahamu miongoni mwa wananchi.
Cha kusikitisha zaidi, siku chache baadaye kuliripotiwa vifo vya watu wengi vilivyosababishwa na matumizi ya risasi. Tukio hili linaashiria matumizi ya nguvu kupita kiasi na kinyume na kanuni za kimataifa na za kitaifa zinazoongoza matumizi ya silaha na nguvu kwa vyombo vya dola.
Matumizi ya risasi dhidi ya raia, hususan katika mazingira ya maandamano, ni dalili ya kushindwa kwa mifumo ya usimamizi wa amani na ulinzi wa haki ya uhai.
Kwa ujumla, chanzo cha matatizo haya si maandamano pekee, bali ni kushindwa kwa Serikali na viongozi wake kusikiliza malalamiko ya wananchi mapema, kudharau sauti za vijana, na kutumia nguvu badala ya mazungumzo. Hali hii inaonyesha mwelekeo wa ukandamizaji wa haki, ambapo malalamiko halali yanajibiwa kwa vitisho, amri tata za kisheria, na nguvu za kijeshi badala ya haki, uwajibikaji, na utawala wa sheria.
Lakini tume ilichotuletea imefanya kazi kama boss wao alivyotaka