SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Sina uhakika kama nitaweza kuielezea mada hii vizuri ila nianze kwa kusema kuwa nimefuatilia muundo wa jamii ya kitanzania, nimegundua unaweza kutugawanya katika makundi mawili kulingana na mitazamo yetu.
Upande mmoja ni wale watu ambao wanapenda kutafuta ukweli wa mambo, hawaogopi kukosolewa, wanapenda kutafuta maarifa, hawaridhiki na pale walipo, wanataka muda wote kupambana kuwa bora zaidi ya jana.
Halafu kuna upande wa pili. Huu ni upande wa wanafiki, wasiopenda kuambiwa ukweli, wenye wivu dhidi ya wale waliowazidi, wenye kusifia vitu vya hivyo kwa kuwa tu ni 'mtu' wao na sifa nyingine kama hizo.
Katika migawanyo hii, nimegundua CCM na Yanga wako upande huo wa pili. Hata hili suala la kuitana sijui 'timu ya wananchi' ni jambo la kisiasa tu linalotukumbusha CCM na YANGA ni pete na kidole.
Nchi hii kuna watu wanapenda sana kushinda. Wanapoona uwezo wao wa kushinda ni mdogo, watatumia njia zote hata zile ovu kufanikisha hilo. Kuna kundi kubwa la Watanzania wapo katika mitazamo hii. Hawa ndiyo wataroga ikibidi, watasambaza fitna na chuki dhidi ya wengine, nk. Haya siyo mambo yanayotakiwa kuwepo katika jamii ya wastaarabu na ya kisasa.
Nchi hii haitaendelea bila kubadilisha fikra ya Mtanzania. Imefika wakati tuanze kuambiana ukweli hata kama unauma.
Inabidi tujenge jamii mpya ya Kitanzania yenye kupenda kusema ukweli, kuchukia uongo na unafki, kupenda maarifa ya kweli, na kufuraia maendeleo ya wengine.