Chanzo cha mgogoro kati ya Rais Trump na Elon Musk

View attachment 3357372
Wiki moja baada ya bilionea wa Marekani, Elon Musk kutangaza kujiondoa katika Serikali ya Rais Donald Trump, uhusiano wao umeendelea kutetereka kiasi cha wawil hao kulumbana mitandaoni.

Musk ambaye ni mmiliki wa kampuni za Tesla, Space X na mtandao wa X (zamani Twitter) alitangaza kujiondoa kwenye Idara ya Ufanisi wa Serikali (DOGE) akieleza kukatishwa tamaa na utendaji wa Trump.

Chanzo cha mzozo

Chanzo cha mgogoro kati ya Rais Donald Trump na Elon Musk ni tofauti zao kuhusu muswada mpya wa bajeti wa chama cha Republican, unaojulikana kama "One Big Beautiful Bill."

Musk amekosoa vikali mswada huo kwa sababu unapunguza ruzuku kwa magari ya umeme—hatua inayoweza kuathiri moja kwa moja biashara ya Tesla. Aidha, amelaumu ongezeko la matumizi ya serikali na kupunguzwa kwa misaada ya kijamii, akiuona mswada huo kama mzigo mkubwa kwa deni la taifa .

Trump, kwa upande wake, ameeleza kusikitishwa na mabadiliko ya msimamo wa Musk, akidai kuwa Musk alikuwa na taarifa zote kuhusu mswada huo kabla ya kupitishwa. Pia, Trump amemshutumu Musk kwa kuwa na upinzani na msimamo wake na kutishia kufuta mikataba ya serikali na kampuni zake, ikiwa ni pamoja na SpaceX na Tesla .

Mgogoro huu pia umechochewa na hatua ya Trump ya kuondo uteuzi wa Jared Isaacman, mshirika wa karibu wa Musk, kama mkurugenzi wa Shirika la Anga la Marekani (NASA), kwa madai ya kuwa na mwelekeo wa kisiasa wa chama cha Democratic.

Musk, ambaye alikuwa mshirika mkubwa wa Trump katika uchaguzi wa 2024 na aliongoza Idara ya Ufanisi wa Serikali (DOGE), sasa amejitenga na utawala wa Trump na amependekeza kuanzisha chama kipya cha kisiasa cha wastani. Amesema kuwa bila msaada wake, Trump asingeweza kushinda uchaguzi wa 2024, akionyesha kutoridhika na kile anachokiona kama kutothaminiwa kwa mchango wake.

Kwa sasa, uhusiano kati ya Trump na Musk umeharibika kabisa, na mgogoro wao una athari kubwa kwa siasa za Marekani, hasa kwa chama cha Republican na uhusiano wake na sekta ya teknolojia.
Wauane tu kama wana CCM, tushawachoka
 
Wacha wauane!
Redneck vs Boers !
Wote roho mbaya, wote wabaguzi, wote mashetani!
Twajiuliza wale makaburi walioenda USA watarudi SA?!
USA hakuna ma servants wa bei poa, hakuna kutishiana silaha, hakuna kubaguana kama SA, kazi wanayo!
 
Wacha wauane!
Redneck vs Boear!
Wote roho mbaya, wote wabaguzi, wote mashetani!
Twajiuliza wale makaburi walioenda USA watarudi SA?!
USA hakuna ma servants wa bei poa, hakuna kutishiana silaha, hakuna kubaguana kama SA, kazi wanayo!
Wale watarudi South Africa tu.Watajuta kwenda USA na kuacha maisha mazuri South Africa.
 
View attachment 3357372
Wiki moja baada ya bilionea wa Marekani, Elon Musk kutangaza kujiondoa katika Serikali ya Rais Donald Trump, uhusiano wao umeendelea kutetereka kiasi cha wawil hao kulumbana mitandaoni.

Musk ambaye ni mmiliki wa kampuni za Tesla, Space X na mtandao wa X (zamani Twitter) alitangaza kujiondoa kwenye Idara ya Ufanisi wa Serikali (DOGE) akieleza kukatishwa tamaa na utendaji wa Trump.

Chanzo cha mzozo

Chanzo cha mgogoro kati ya Rais Donald Trump na Elon Musk ni tofauti zao kuhusu muswada mpya wa bajeti wa chama cha Republican, unaojulikana kama "One Big Beautiful Bill."

Musk amekosoa vikali mswada huo kwa sababu unapunguza ruzuku kwa magari ya umeme—hatua inayoweza kuathiri moja kwa moja biashara ya Tesla. Aidha, amelaumu ongezeko la matumizi ya serikali na kupunguzwa kwa misaada ya kijamii, akiuona mswada huo kama mzigo mkubwa kwa deni la taifa .

Trump, kwa upande wake, ameeleza kusikitishwa na mabadiliko ya msimamo wa Musk, akidai kuwa Musk alikuwa na taarifa zote kuhusu mswada huo kabla ya kupitishwa. Pia, Trump amemshutumu Musk kwa kuwa na upinzani na msimamo wake na kutishia kufuta mikataba ya serikali na kampuni zake, ikiwa ni pamoja na SpaceX na Tesla .

Mgogoro huu pia umechochewa na hatua ya Trump ya kuondo uteuzi wa Jared Isaacman, mshirika wa karibu wa Musk, kama mkurugenzi wa Shirika la Anga la Marekani (NASA), kwa madai ya kuwa na mwelekeo wa kisiasa wa chama cha Democratic.

Musk, ambaye alikuwa mshirika mkubwa wa Trump katika uchaguzi wa 2024 na aliongoza Idara ya Ufanisi wa Serikali (DOGE), sasa amejitenga na utawala wa Trump na amependekeza kuanzisha chama kipya cha kisiasa cha wastani. Amesema kuwa bila msaada wake, Trump asingeweza kushinda uchaguzi wa 2024, akionyesha kutoridhika na kile anachokiona kama kutothaminiwa kwa mchango wake.

Kwa sasa, uhusiano kati ya Trump na Musk umeharibika kabisa, na mgogoro wao una athari kubwa kwa siasa za Marekani, hasa kwa chama cha Republican na uhusiano wake na sekta ya teknolojia.
Acha moto uwake,akatuletea midoli ya kufanyia mapenzi,AI, Mungu hadhihakiwi,economic barriers😆,waendelee kumwalika mzee wa Brics
 
Mwaka jana niliandika kitu kwenye ukurasa wa Twitter wa Elon juu ya uhusiama wake na Trump "Niliongea kama ndoa yenye masharti magumu isiyodumu", Mama yake Elon alinifuata In box na kuniuliza namfahamu vipi mwanaye? Nikimuamuambia kuwa mimi ni shabiki wake ila nachelea kuwa tokana na tabia na mwenendo wa Trump uhusiano wao ni wa muda mfupi sana hivyo Elon asitengeneze maadui kwa kuwa itamghalimu maisha yake yote. Na kweli imetokea.
 
Listi ya wateja waliokuwa wananunua ngono toka kwa watoto wadogo Muuzaji akiwa mtu anajulikana kwa jina la Jeffrey Epstein, ni rafiki wa P.didy,Obama, DJT, Bill Clinton na vigogo wengine, hawa wote wanatajwa kuwa moja ya wateja wakubwa wa biashara ya Epstein.
Kununua ngono unamaanisha sex au porno?
 
Kununua ngono unamaanisha sex au porno?
Ngono:intercourse
Pornograph:representation of sexual behaviour in books, pictures, statues, films, and other media that is intended to cause sexual excitement.
Hivyo ngono ni kitendo chenyewe.
 
Yaani Ramaphosa aingie oval Office asimwage vile vitu vya ki Afrika?Na kuku wa manyoya mcharuko walivyojaa Afrika? Mafaraka ya masangoma wa kusini mwa Afrika washindwe?

Ellon ndiye alikuwa mchonganishi USA na SA walielewane, akampa Trump picha feki za CongoDr.

Matajiri wakigombana masikini anapata afueni
 
Elon kaanza kutoa siri za Trump.Moja ni Trump alikuwa kwenye list ya Epstein. IMAGINE ELON KAONDOKA NA SIRI NGAPI KUTOKA KWENYE COMPUTER ZA IKULU. ELON KAMA MANGE TU.
Samahani....hivyo hiyo list ya Epstein inahusiana na nini?
 
Elon kaanza kutoa siri za Trump.Moja ni Trump alikuwa kwenye list ya Epstein. IMAGINE ELON KAONDOKA NA SIRI NGAPI KUTOKA KWENYE COMPUTER ZA IKULU. ELON KAMA MANGE TU.

Epstein ni nini? Ebu tufafanulieni, toka jana uko X naona hilo neno
 
Back
Top Bottom