Chanzo cha Migogoro Endelevu ya Kisiasa Nchini Tanzania

Chanzo cha Migogoro Endelevu ya Kisiasa Nchini Tanzania

Chesi20

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2020
Posts
291
Reaction score
112
Maisha baada ya matokeo ya Uchaguzi wa Tanzania 2020 yameleta gumzo na mjadala usiokua na dalii za kufika tamati. Dalili zote zinaonyesha kuwa chanzo cha marumbano na migogoro endelevu ya kisiasa ni madhara mabaya ya mfumo wa vyama vingi.

Mfumo wa vyama vingi unaleta chuki mbaya na migogoro endelevu kati yetu sisi kwa sisi isiyokua na mwisho hadi kufikia hatua ya kuuana wenyewe kwa wenyewe.
Mfumo wa vyama vingi hupandikiza chuki mbaya sana, inayoota taratibu kati ya chama tawala na baadhi ya vyama vya upinzani kama vile kipele cha cancer kinavyoota mwilini, ambacho kinaweza kuleta madhara makubwa sana mwilini endapo kisipotibiwa.

Je, mfumo wa vyama vingi wenye madhara mabaya kama hayo unatufaa sisi watanzania ??

Kama hautufai, ni mfumo gani unaofaa kutumika ili kuleta umoja, nguvu na mshikamano hapa Tanzania??
 
Ni Ulafi tu wala sio Mbaya... Roho za chuki tu ndo zinatusumbua Waafrica. Mbona wenzetu Nigeria hata jilani zetu Msumbiji Wanabadirishana tu madaraka maisha yanaendelea. Chakula kula na wenzako Ndio Kitamu. Siasa ni nzuri Mpinzani wako anapokuwa yupo karibu na wewe.. watanzania waliamua wenyewe na tumeishi kwenye Mfumo huu ( multipart system) na tumeona matunda yake na raha yake za siasa. Sasa hii ya sasa Daaah!! ngoja tuone, maana tunaweza kuwa na wasiwasi tu wakati tunaelekea kwenye nchi yenye Asali na Maziwa. Tujipe muda maana siku zote Mr.muda ni kweli.
 
Migogoro huletwa na Kiongozi wa nchi, kama huyu wa kwenu, hatuwezi kumtazama atutoboe Macho kwa mara nyingine
Unadhani kiongozi ambaye ni sahihi kwako, kwenye utawala wake hakutakuwa na mapungufu??
 
Chuki katika nchi yetu inaletwa na CCM kwakuwa inalazimisha kutawala kwa shuruti. Hata ndani ya CCM kuna chuki kwa sababu ya haki kutokutendeka.
Hata vyama vyote vifutwe iwe serikali ya kijeshi, kama hakuna haki chuki lazima itawale. Mnalazimisha kuondoa mfumo wa vyama vingi kwa ajili ya uchu wa madaraka. Lakini vyama vikiondoka ushindani utakuwa wa kikanda, kidini, kikabila nk. Na kote huko chuki itatawala maana tatizo itakuwa ni kutenda haki. Hata mrudishe mfumo wa chama kimoja kwa shuruti, bado hatuko tayari kutawaliwa na CCM.
 
Unadhani kiongozi ambaye ni sahihi kwako, kwenye utawala wake hakutakuwa na mapungufu??

Kwanini nchi hii inapotawaliwa na kiongozi wa kikristo chuki na kuumiza watu, hasa wenye mitazamo mbadala inakuwa kubwa?
 
Kwanini nchi hii inapotawaliwa na kiongozi wa kikristo chuki na kuumiza watu, hasa wenye mitazamo mbadala inakuwa kubwa?
Jibu la swali hili umeshaliandika kwenye post yako ulioyoandika kuwa, hata kama vyama vyote vya kisiasa vikifutwa, bado chuki itaendelea kuwepo kikabila, kidini, nk.
Asante sana kwa maoni yako.
 
Mfumo wa demokrasia una kanuni zake na kanuni ya kwanza, na ya msingi kupita zote, ni HAKI sawa kwa wadau wote, haswa vyama vya siasa.
Chama kilichopo madarakani kinatakiwa kiwezeshe mazingira ya HAKI sawa kwa wadau wote wa demokrasia nchini.
 
Ndani ya CCM kuna chuki kubwa kupita hata hizi za wapinzani na CCM. Fanya research mkuu
Nakubaliana na ww kuwa kuna chuki kati ya CCM kwa CCM.
Mtazamo wangu pia chuki ipo kati ya CHADEMA kwa CHADEMA au CUF na CUF. Mfano, kama sio chuki ndani ya chama kimoja, wale Wabunge wa CHADEMA kuhamia CCM, au yule kiongozi wa CUF kuhamia ACT wazalendo!
 
Kwa nini haya yanatokea awamu hii ?Mbona tulikotokea baada ya kukubali mfumo wa vyama vingi hatuyaona yanayotendeka leo ?Something is not right somewhere,tujitafakari kama wenye nchi.
 
Jibu la swali hili umeshaliandika kwenye post yako ulioyoandika kuwa, hata kama vyama vyote vya kisiasa vikifutwa, bado chuki itaendelea kuwepo kikabila, kidini, nk.
Asante sana kwa maoni yako.
Ila Polisi na Jeshi hawawezi kuuwa watu kama kule ZNZ
 
Chuki katika nchi yetu inaletwa na ccm kwakuwa inalazimisha kutawala kwa shuruti. Hata ndani ya ccm kuna chuki kwa sababu ya haki kutokutendeka. Hata vyama vyote vifutwe iwe serikali ya kijeshi, kama hakuna haki chuki lazima itawale. Mnalazimisha kuondoa mfumo wa vyama vingi kwa ajili ya uchu wa madaraka. Lakini vyama vikiondoka ushindani utakuwa wa kikanda, kidini, kikabila nk. Na kote huko chuki itatawala maana tatizo itakuwa ni kutenda haki. Hata mrudishe mfumo wa chama kimoja kwa shuruti, bado hatuko tayari kutawaliwa na ccm.
Agiza kinywaji, bili kwangu.
 
Ugomvi kwenye nchi zetu wala siyo mfumo wa vyama vingi tatizo ni utajiri wa raslimali zetu ambao ni kichocheo cha nchi za nje kugombanisha ili zirudi kuvuna. That is all.
 
Tatizo siyo mfumo wa vyama vingi.. Shida ni chama tawala kutotenda haki, na kutumia ubabe wazi wazi.

Kwa mfano, kwenye Uchaguzi wa mwaka huu, wananchi karibu wote, wanajua CCM imeshinda kwa wizi na unyang'anyi, na imejinyakulia madaraka kwa nguvu, na hivyo inatawala bila ridhaa yao
 
..mfumo wa demokrasia una kanuni zake.

..na kanuni ya kwanza, na ya msingi kupita zote, ni HAKI sawa kwa wadau wote, haswa vyama vya siasa.

..chama kilichopo madarakani kinatakiwa kiwezeshe mazingira ya HAKI sawa kwa wadau wote wa demokrasia nchini.
Umenena Mkuu!

Mfumo wowote ule una kanuni zake na unahitaji uadilifu katika kuzifuata kanuni zake zote ili ufanye kazi kwa ufanisi. Huwezi kuchagua baadhi na kuacha nyingine, utegemee matokeo yaleyale; Hapana! Ni kama mfumo wa mwili wa binadamu, huwezi kuondoa baadhi ya viungo ukategemea ufanisi ule ule. Lazima kutakuwa na utofauti.

Kwa kuongezea: Demokrasia inahitaji ushiriki mpana na siyo ushiriki wa wanasiasa tu! Hili kosa tunalofanya la kuachia maamuzi yote ya mwelekeo wa nchi yafanywe na wanasiasa yatatudumaza sana.
 
Back
Top Bottom