Lucchese DeCavalcante
JF-Expert Member
- Jan 10, 2009
- 5,471
- 752

Hasheem Vs Top in Dar
Majibizano yao katika jokes!
Inavuma kitaani, kila mmoja anajaribu kusema lake kuhusiana na ugomvi wa mastaa wawili, staa wa NBA anayekipiga kwenye Klabu ya Memphis Grizzlies, Hasheem Thabeet na icon wa Bongo Fleva, Khaleed Mohamed TID.Majibizano yao katika jokes!
Mengi yamezungumzwa lakini ipo ishu ya utani ambayo inatajwa. Kuanzia walipoonana, wakaanza kujibizana na baadaye kipigo. Usisahau ishu ya yule dogo aliyekula mbata a.k.a kerbu kutoka kwa staa huyo wa NBA.
Eti ishu ilianza hivi;
TID na chombo chake, walikuwa wanakula mema ya nchi ndani ya Club Bilicanas, Dar muda fulani hivi baadaye, Hasheem akatokea, huku akiwa ameongozana na washkaji kadhaa.
Eti, demu wa TID alipomuona Hasheem akapagawa, wooow, hiyo Top In Dar ikamuudhi, akaweka bifu.
Akangoja Hasheem apite, akamuanzishia kama hivi;
TID: Oyaa, we dogo unajiona umemaliza kila kitu?
Hasheem: Kivipi bro?
TID: Unajua dogo unajiona matawi sana?
Hasheem: Sijakuelewa kaka.
TID: Mbona unapita bila kusalimia?
Hasheem: Ooh, nikupitiwa you know, samahani.
TID: You know nini? Shauri yako!
Hasheem: Nimekuomba msamaha.
TID: Msamaha wapi? Yaani sisi tushindwe kutanua na mademu zetu kisa wewe?
Hasheem: Mbona sikuelewi?
TID: Ntakufanyia kitu mbaya!
Hasheem: Huko unakokwenda siyo kabisa.
TID: Mi mtoto wa Kino, nitakuharibia halafu tutakomba vyote vya mwilini.
Hasheem: Basi kama vipi jaribu.
TID: Alafu wewe unajidaia urefu wako.
Hasheem: Oyaa, nitaku-dunk kama basketball?
TID: Jaribu, mimi nitakubutua kama football au nitakukumbatia kama MIC.
Hasheem: Maneno mengi ya nini? Jaribu!
TID: Unajidai una pesa, mimi nimekuwa staa wa nchi hii kabla yako.
Hasheem: Naona hauna la kuongea, naondoka!
TID: Oyaa, mbona unaondoka, hatupigani tena?
Eti baada ya hapo, jamaa akamchota mtama mmoja ambao ulikaribia kuondoa uhai wa mtu. Ila hii siyo hali halisi iliyotokea, its only jokes.
Kuhusu brothermen aliyekula kibao;
Brothermen: Duh, huyu jamaa mrefu!
Hasheem: Ndiyo kaka, mimi mrefu, unasemaje?
Brothermen: Aah, kwani nini?
Hasheem: Anyway, poa.
Brothermen: Poa nini? Naona siku hizi unajidaia vogue lako.
Hasheem: Duh!
Brothermen: Halafu sisi kitaani hatukufagilii wala nini?
Hasheem: Naomba tuheshimiane basi!
Brothermen: Akuheshimu nani? Unafikiri mimi TID, nitakupa kipondo?
Hasheem: Unaweza kunipiga?
Brothermen: Yap, sogea hapa uone.
Baada ya hapo jamaa alikula mbata moja, kisha akazimika.
USHAURI SERIOUS
Matatizo anayokumbana nayo Hasheem yanatokana na Wabongo kutotambua thamani yake. Bado tunasumbuliwa na ile tabia ya wivu usiokuwa na maana.
Hata kama wewe ulikuwa maarufu kabla ya Hasheem, muhimu ni kutambua kwamba jamaa yupo daraja lingine kwa sasa.
Tulichojifunza ni kwamba watu wengine hawataki kumheshimu Hasheem kwa sababu tu walimuona jinsi alivyokuwa, anasukumwa na makonda kwenye daladala.
Jamaa ni hero wa taifa, Watanzania wakimchukulia ni mfano wa kuigwa, anaweza kuwa njia ya vijana wengi kuelekea kwenye mafanikio. Inawezekana, wengi wanaponzwa na jinsi mchizi anavyojichanganya na wana wa kitaa halafu anafanana nao.