Chanzo cha ugomvi wa Hasheem na TID

Chanzo cha ugomvi wa Hasheem na TID

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2009
Posts
5,471
Reaction score
752


Hasheem Vs Top in Dar

Majibizano yao katika jokes!
Inavuma kitaani, kila mmoja anajaribu kusema lake kuhusiana na ugomvi wa mastaa wawili, staa wa NBA anayekipiga kwenye Klabu ya Memphis Grizzlies, Hasheem Thabeet na icon wa Bongo Fleva, Khaleed Mohamed ‘TID’.

Mengi yamezungumzwa lakini ipo ishu ya utani ambayo inatajwa. Kuanzia walipoonana, wakaanza kujibizana na baadaye kipigo. Usisahau ishu ya yule dogo aliyekula mbata a.k.a kerbu kutoka kwa staa huyo wa NBA.

Eti ishu ilianza hivi;
TID na chombo chake, walikuwa wanakula mema ya nchi ndani ya Club Bilicanas, Dar muda fulani hivi baadaye, Hasheem akatokea, huku akiwa ameongozana na washkaji kadhaa.
Eti, demu wa TID alipomuona Hasheem akapagawa, “wooow”, hiyo Top In Dar ikamuudhi, akaweka bifu.
Akangoja Hasheem apite, akamuanzishia kama hivi;

TID: Oyaa, we’ dogo unajiona umemaliza kila kitu?
Hasheem: Kivipi bro?
TID: Unajua dogo unajiona matawi sana?
Hasheem: Sijakuelewa kaka.
TID: Mbona unapita bila kusalimia?
Hasheem: Ooh, nikupitiwa you know, samahani.
TID: You know nini? Shauri yako!
Hasheem: Nimekuomba msamaha.
TID: Msamaha wapi? Yaani sisi tushindwe kutanua na mademu zetu kisa wewe?
Hasheem: Mbona sikuelewi?
TID: Ntakufanyia kitu mbaya!
Hasheem: Huko unakokwenda siyo kabisa.
TID: Mi’ mtoto wa Kino, nitakuharibia halafu tutakomba vyote vya mwilini.
Hasheem: Basi kama vipi jaribu.
TID: Alafu wewe unajidaia urefu wako.
Hasheem: Oyaa, nitaku-dunk kama basketball?
TID: Jaribu, mimi nitakubutua kama football au nitakukumbatia kama MIC.
Hasheem: Maneno mengi ya nini? Jaribu!
TID: Unajidai una pesa, mimi nimekuwa staa wa nchi hii kabla yako.
Hasheem: Naona hauna la kuongea, naondoka!
TID: Oyaa, mbona unaondoka, hatupigani tena?

Eti baada ya hapo, jamaa akamchota mtama mmoja ambao ulikaribia kuondoa uhai wa mtu. Ila hii siyo hali halisi iliyotokea, its only jokes.

Kuhusu brothermen aliyekula kibao;
Brothermen: Duh, huyu jamaa mrefu!
Hasheem: Ndiyo kaka, mimi mrefu, unasemaje?
Brothermen: Aah, kwani nini?
Hasheem: Anyway, poa.
Brothermen: Poa nini? Naona siku hizi unajidaia vogue lako.
Hasheem: Duh!
Brothermen: Halafu sisi kitaani hatukufagilii wala nini?
Hasheem: Naomba tuheshimiane basi!
Brothermen: Akuheshimu nani? Unafikiri mimi TID, nitakupa kipondo?
Hasheem: Unaweza kunipiga?
Brothermen: Yap, sogea hapa uone.
Baada ya hapo jamaa alikula mbata moja, kisha akazimika.

USHAURI SERIOUS
Matatizo anayokumbana nayo Hasheem yanatokana na Wabongo kutotambua thamani yake. Bado tunasumbuliwa na ile tabia ya wivu usiokuwa na maana.
Hata kama wewe ulikuwa maarufu kabla ya Hasheem, muhimu ni kutambua kwamba jamaa yupo daraja lingine kwa sasa.

Tulichojifunza ni kwamba watu wengine hawataki kumheshimu Hasheem kwa sababu tu walimuona jinsi alivyokuwa, anasukumwa na makonda kwenye daladala.
Jamaa ni ‘hero’ wa taifa, Watanzania wakimchukulia ni mfano wa kuigwa, anaweza kuwa njia ya vijana wengi kuelekea kwenye mafanikio. Inawezekana, wengi wanaponzwa na jinsi ‘mchizi’ anavyojichanganya na wana wa kitaa halafu anafanana nao.
 
Inasikitisha Tanzania tusivyothamini talent zetu anyway silaumu ni tabia ya watanzania wengi kuwa na miwivu ya kijinga
 
jealous! tu zimetujaaa wabongo. Nakwambia Hata kama angekaa ndani kwao wangeenda kumchokonoa tu. Bila shaka ni Super Star wa ukweri hapa bongo. tena kwa ku-struggle kwake mwenyewe.
 
Inasikitisha Tanzania tusivyothamini talent zetu anyway silaumu ni tabia ya watanzania wengi kuwa na miwivu ya kijinga


Unakosea lazima ulaumu ili walaumiwa waamke kwenye usingizi mzito! Chukua hatua!
 
wanasema ukiona mtu ananenwa vibaya na kila mtu, basi jua ana tatizo.TID hashauriki, kijana amelewa sifa, na ujinga wake huo ndiyo uliompeleka Jela. Badilika kijana.
 
wanasema ukiona mtu ananenwa vibaya na kila mtu, basi jua ana tatizo.TID hashauriki, kijana amelewa sifa, na ujinga wake huo ndiyo uliompeleka Jela. Badilika kijana.

Hivi jamani TID anaweza kupigana kweli???majuzi nimemwona choka mbaya sana!!!!Najionelea Hasheem alikuwa anatafuta mudder case.....TID kachoka sana jamani.
 
Back
Top Bottom