Chanzo cha Umasikini kwa Wafanyakazi sio Mishahara midogo bali ni Ukosefu wa Elimu ya Kifedha

Chanzo cha Umasikini kwa Wafanyakazi sio Mishahara midogo bali ni Ukosefu wa Elimu ya Kifedha

Nmeongea haya sio kwa nadharia hapana mimi nmeajiriwa 2012 nmecheza kombolela kama miaka mitano hivi, yaani unalipwa mshahara hujui hata unaishia wapi😅

Na hapo sikua na familia wala nini lakini nhoma haioni giza mbili. Nikaja kupata dem akachangia kunifungua mawazo, nikajiuliza saiz nakaa na dem lakin hela naiona na inakutana na mwez ujao na nakula vizuri shida ilikua wapi????

Siku moja nmekaa na bibie tukaanza kupanga bajeti ya mwaka ndo akanieleza nunua mahitaji kwa mwaka hatutaumia, nakumbuka wakati wa watu kuvuna mahindi nikaagiza kijijin kunia moja la mahindi wakat mwanzo nlikua nanunua unga sembe, mchele tukaanza kununua wakati wa mavuno tunaagiza, nkaanza kununua mkaa wakati mwanzo nlikua na gesi pekee, mafuta,sabuni n.k tukaanza kununua maduka ya jumla.

Nikienda kazini nlikua nanunua maji ya buku na soda au maji tu lakini akaninunulia chupa akawa ananiwekea maji ya kunywa 2LT na kachupa kengine cha juice ya kusaga mara moja moja. Kazini nikawa sili anapika home anampa boda ananletea kwa buku.

Tuliweza kuishi maisha yetu japo mwanzo nlikua naona aibu wana wananicheka ila saiz ndo wanakuja niwakopeshe hela.

BILA KUPANGA BAJETI HUWEZI KUONA MIANYA YA KUPUNGUZA MATUMIZI YASIO YA LAZIMA
Aisee.
 
Back
Top Bottom