Mkuu
SAYANSIKIMU,
Pongezi kwa kujitahidi kuwaza na kuleta mada. Kimsingi wengi wa wenye kuegemea mlango huu uliochukua wa kwamba (i) vitu vimejiunda vyenyewe AUTOMATICALLY/ by CHANCE mwishoni huwa wanashindwa ku-explain order tunayoikuta kwenye all matter kuanzia a tiny ATOM hadi planets na galaxies na biological systems. Kifupi ni kuwa kama matter iliyotuzunguka ingejiumba yenyewe AUTOMATICALLY, basi for sure tungeshuhudia CHAOS nyingi kwa vile kusingekuwa na kule kutulia (equilbrium) tunayoiona (ii) lengo kuu la mlengo huu ni MWISHOWE kukataa kuwa kuna MUUMBAJI. Ila sielewi jinsi ambavyo ukirudi nyumbani kwako, ukaikuta sahani ya wali kitandani katikati kama itakuwa busara kuamua kuwa hiyo sahani na huo wali vimefika chumbani na kitandani kwako BY CHANCE!!!!!
Dosari ambayo huwa naiona inajitokeza kila mara katika mada za upande huu ni kule kukosekana maelezo yanajitosheleza ya kueleza kwanini tuna ORDER kwenye kila kitu kiasi kuwa hata maisha yetu tuna desturi ya kujiwekea taratibu.
Hongera kwa mada tamu. Tuendelee kuchangia.