Mkuu
Free ideas,
Awali ya yote mimi ni mwislamu, na wala imani yangu haina tatizo na scientific outlook unayoizungumzia. Tukizungumzia concept ya evolution ya natural systems sipati tatizo kwa vile katika imani yangu kuna concept ya Mola Mlezi. Ikimaanisha all evolutionary stages ambazo system objects (created objects) zitahitahitaji kwa ajili ya kupambana na mazingira yao zitapata kutokona na design iliyowaumba.
Hapa nitafafanua. Marekani kuna Bison. Kwa Wao ni kama buffalo. Ukimwangalia ni kama Nyumbu wa hapa ila wa kule ana manyoya mengi sana mwili mzima. Hapa utaona kuwa Bison ana manyoya kwa ajili ya kumhifadhi na baridi ya kule. Lakini huwezi kusema eti Bison walikaa wakasema sasa tutaota manyoya zaidi mwilini mwetu. Tuliopo huku Afrika hatukuitisha kikao na kuamua sasa tutaongeza melanin katika ngozi zetu.
Ama kuhusu ICE age, Iron age, Stone age hizo ni zama ambazo tunafundishwa kuwa kila jamii ilikuwa na zama zake. Wapo walioishi mapangoni nk. Lakini vitabu vyote vya dini huwa mara nyingi vinasimulia kuhusu mazingatio yanayotokana na matendo ya waliotangulia kama darsa kwa waliopo.
Kwa maana hiyo haijalishi hao waliotajwa waliishi kwa kutumia nyenzo zipi.
Mimi imani yangu inanielekeza kwenye Kurani. Na inaeleza kuwa dunia ipo katika umbile la duara. Na duara hiyo ni kama yai la mbuni kwa mtazamo wa mbali. Hayo yaliongewa 1400 years ago. Hii imethibitishwa kuwa kweli.
Hakuna anayejua Adamu na Hawa walikuwa na sura zipi. Ila neno Adam maana yake ni "nyekundu" kwa kiebrania. hapa inaelekea Adam alikuwa na features za aina hiyo. yaani rangi yake juu kidogo ya tunachoita "maji ya kunde".
Lakini ile theory ya Darwin kuwa huenda tulikuwa Gorrilas au Chimpazees, then tuka-evolve na kuwa binadamu wa leo inapingwa na scientists wengi wa siku zetu hizi
Disputing Darwin
binafsi sikubaliani na wazo kuwa Adam na Hawa walikuwa Chimpanzees, pia scientifically usichanganye viwili.
Kama sasa unaenda kwenye dini (maana ndiko kumetajwa Adam na Hawa tuuuu) basi Chimpanzees huwa hawafanyi TOBA kama Adamu na Hawa walivyojitahidi kufanya kwa Mola wao baada ya Makosa yao