Mungu ninayemsema hapa ni Mungu aliyetuumba sisi kama alivyowaumba Adam na Hawa/Eve, mwenye uwezo wa kukufisha na kukuhuisha.
Kama nitalazimika kusema uumbaji wake wa ulimwengu ulikuaje ni lazima nihusishe vitabu vya dini, Quran imeeleza namna gani Ulimwengu uliumbwa. Wanasayansi waliokuja na hoja za uumbaji wa ulimwengu si wa kongwe kama Quran iliyoshushwa tangu Karne ya 7. Na imeeleza kwa namna gani ulimwengu uliumbwa. Kwa karne ya 7 isingekuwa rahisi kuishi mtu mwenye maarifa makubwa kama yaliyoonekana katika Quran yakieleza namna ulimwengu ulivyoumbwa. Naamini maarifa hayo ni ya Mungu peke yake alipokuwa akitanabaisha namna alivyouumba ulimwengu.
Wasio amni husema Quran ni maneno ya Mtume Muhammad (SAW), jambo ambalo sio kweli, kwani asingeweza kuwa na maarifa ya namna ulimwengu ulivyoumbwa kama hakuambiwa na Mungu mwenyewe ili awafikishie wanaadamu namna ambavyo aliumba ulimwengu.
Kuhusu Mungu alikuwa wapi wakati anaumba ulimwengu, mimi sijui (Yeye mwenyewe ndo anaejua). Baada ya wanasayansi kuanza kutafiti ulimwengu uliumbwaje, walipata kufanana na namna gani Quran ilieleza ulimwengu ulivyoumbwa. Hoja za Big Bang theory zilimezwa na hoja za kwenye Quran ya karne ya 7.
Ukipitia link hapo chini unaweza kuona mengi zaidi juu ya nilichodokeza.
Quran-Islam.org - True Islam