Chanzo halisi cha binadamu (Origins of mankind)

Chanzo halisi cha binadamu (Origins of mankind)

Hivi hawa Neanderthals, sio kwamba walipochangamana na homo sapiens ndio kukapatikana hizi race za wazungu wenye akili?? Mbona sisi Africa bado sana hata kiuwezo wa kufikiria?🤣🤣
Tunawaza ngono tu
Hahaha...hiyo labda uanzishe theory yako.
Lakini Neanderthals walikuwa primitive.wala hawakuwa na akili kama homo sapiens.
 
Usifuate hadithi...fuata ushahidi unapokupeleka. Hizi sio hadithi by the way kama za kwenye biblia.
Mh! Mm ni mfuatiliaji sana wa hizi mambo ila sijawahi amini hizi hadithi za ngedere mara chipanzee mara nyani, mbona hao nyani wa leo hawabadiliki!!?
 
Mh! Mm ni mfuatiliaji sana wa hizi mambo ila sijawahi amini hizi hadithi za ngedere mara chipanzee mara nyani, mbona hao nyani wa leo hawabadiliki!!?
Aah wewe sio mfuatiliaji. Kwa hilo swali ulilouliza tu inaonesha sio mfuatiliaji.

Chukulia huu mfano.
Baba azae watoto wawili wenye sifa tofauti, mmoja mkubwa wa kiume ana mandevu mwingine mtoto mdogo wa kike hajavunja hata ungo.
Sasa assume wewe ni nzi wa kwanza wa kipekee umepewa akili ya utambuzi wa kibinadamu (lifespan ya nzi ni siku 10).
Halafu uambiwe kuwa huyo mtoto mkubwa mwenye ndevu na huyo mdogo wake wa kike asiye nazo, pamoja na tofauti zao zote, wote wametoka kwa baba mmoja.
Halafu uambiwe pia kuwa hata huyo mkubwa mwenye ndevu alikuwaga mdogo pia zamani huko na hakuwa na ndevu.

Sasa wewe uanze kuwaangalia kwa hizo siku 10 za maisha yako kama huyo mtoto atabadilika na kuwa mkubwa mwenye ndevu kwa hizo siku.
Halafu baada ya kuona hizo siku zote hujaona mabadiliko yeyote kwa hao watoto, uhitimishe kuwa hawa ndivyo walivyo hawajatoka kwa baba mmoja na pia hawawezi kubadilika. Maana hujaona hata nywele moja inaota.

Swali lako la kwanini Nyani hawageuki kuwa watu, ni sawa na kuuliza kwanini yule mtoto mdogo hageuki kuwa mkubwa. Halimake sense.

Sisi hatujatokana na nyani..ila sisi na nyani tumetokana na baba mmoja ambae hiko kiumbe kilishapotea.
Wewe unaishi around miaka 60,Elimu na historia yote unayoijua haizidi miaka 6000 tu iliyopita. lakini evolution kutoka ndugu wetu wa karibu nyani (chimpanzee,) imechukua miaka zaidi ya millioni 7 iliyopita.

Kwahyo usitegemee hawa nyani kuwa watu, watabadilika kuwa kiumbe kingine kisichojulikana na sisi binadamu tunabadilika kuwa viumbe wengine haijulikani.... ila tunabadilika kwa kasi ndogo sana huwezi kuiona wewe. Kama jinsi nzi hawezi kuona binadamu wanavyokua.

Hata saivi ukiangalia binadamu wa miaka ya zamani na sasa tumeshabadilika kidogo. Sikuizi hata rangi tu kwa hapa Tz. mabinti weupe ni wengi kuliko zamani. Mabadiliko yapo ila yanatokea slowly sana huwezi kuyaona kwa lifespan yako ya miaka 60.
Ukifa ukafufuka baada ya miaka 10, 000 utashangaa kukuta watu hapa Tz ukakataa hawa sio watanzania.
 
Concept nzuri sana hii na naifahamu vizuri tu!

- chukulia kiumbe hai kina kufa na kinaanza kuoza, baada ya siku kadhaa vinatokea vimelea kwa yule kiumbe mfu alieanza kua mzogo, na wanatokea aina nyingi za vimelea, japo vingine vinakua vingi kuliko jamii nyingine ya vimelea, na kuna ambao huwezi kuviona kirahisi, na kuna ambavyo usiweze kuviona kwa macho yako, sasa hapa nikikuambia kua sisi na viumbe hai wengine ni matokeo ya process inayo fanana na mfano huo utakubali au utakataa!!? Haya mambo ni magumu kidogo. Kuna ambao wakikuelezea kuhusu alliens kumuumba binadamu out of hao ngedere na masokwe nao wana factors ambazo wewe hunasuki humo. [emoji89] Na hua zina make sense kuliko hizi concept zingine
 
Sasa hapa nikikuambia kua sisi na viumbe hai wengine ni matokeo ya process inayo fanana na mfano huo utakubali au utakataa!!?
Process zipi??
Kuna ambao wakikuelezea kuhusu alliens kumuumba binadamu out of hao ngedere na masokwe nao wana factors ambazo wewe hunasuki humo. [emoji89] Na hua zina make sense kuliko hizi concept zingine
Hizi ni hearsay zisizo na ushahidi wowote.
I'll admit, ni theories nzuri masikioni ambazo watu walikaa wakazifikiria ili wauze vitabu kwa laymens.
 
Process zipi??

Hizi ni hearsay zisizo na ushahidi wowote.
I'll admit, ni theories nzuri masikioni ambazo watu walikaa wakazifikiria ili wauze vitabu kwa laymens.
Kama wewe huamini nani ataelewa hizo hearsay zako!!?
 
Duh, mkuu hata sijaelewa hili swali lako.
Tukubaliane kuto kukubaliana tu! Kila mtu alewe anavyo elewa! Kama wewe ulitokea kwa ngedere haya, kama mimi niliumbwa na alliens sawa, kama tumetokea kwenye muozo wa kitu flani(dunia " dunia ilikua hai ilipo kufatu sisi viumbe hai unao tuona ndio vile vimelea vinavyo toka kwenye mzoga ") sawa. Hii biashara imeishia hapa
 
Okay sawa...ila huu uzi sio kwa ajili ya conspiracy theories kama una evidence ya theory yako unaweza kuweka pia tujifunze.
 
Nilisoma theory za origin of life ila kwa uvivu nilivyomaliza mtihani nikatupa vitini.

Nimejifunza kitu cha ziada.

Asante sana
knowledge tunazofundishwa vyuoni nyingi ni za mchongo ili kutu brainwash......real knowledge na siri za ulimwengu huu zinapatikana kwenye vitabu ambavyo havipo kwenye mitaala ya shule/vyuo.

itakukubidi utoke nje ya box la yale ulivyofundishwa vyuoni na maprofesa. dedicate mda wako kujisomea vitabu na journals za waandishi/watafiti mbalimbali. kwa kufanya hivyo utakuwa umejikusanyia knowledge kubwa na hakuna ambaye atakudanganya.
 
Tsup! Leo tuzamishe kidole gumba kwenye bahari -bahari ambayo ni hii mada ihusuyo chanzo halisi cha binadamu.

Hii story (History[emoji28]) ni very complicated na ndefu ila nataka niandike kwa ufupi sana nisije nikajaza page 200, so without further'a do, let's dive into it.

Creation theory
Kabla ya 1800's watu wengi waliamini katika creation theory (special creation) ambayo waliamini kuna Mungu aliumba kila kitu ulimwenguni kama kilivyo sasa kwa siku saba tu. Yani aliumba binadamu akiwa kama binadamu wa sasa na wanyama wote wakiwa kama walivyo sasa. Pia hii imani ya uumbaji iliambatana na imani ya new Earth, yani ulimwengu ni mchanga, kwamba Mungu ameumba dunia miaka michache iliyopita (roughly 6000 yrs ago) akaumba na binadamu na viumbe wote kwa pamoja.

Johann Friedrich Blumenbach
Miaka ya late 1870's to early 1880's huyu mjerumani Blumenbach ndio alikuwa mtu wa kwanza kufuatilia kisayansi chanzo cha binadamu na kupitia kazi zake anatambulika kama founder wa Zoology na anthropology.

View attachment 2417007
Blumenbach Alichukua mafuvu ya races mbalimbali na akaanza kuya'study kwa kufuatilia tofauti zake, kwa kuangalia shape ya vichwa vya mafuvu ya watu mbalimbali duniani. Aligawanya binadamu katika race 5 ambazo ni Caucasian(wazungu+ waarabu +wapersians), Mongolian(Watu wa Asia ya kati na mashariki kama wachina, Wajapan nk.), Malayan (watu wa asia ya kusini na visiwani kama philipino, indonesia, malaysia nk.)American(wale native amercans kama red indians), Ethiopian(Negroids, watu weusi, African, sisi)
Blumenbach aliamini katika story ya creation kwenye biblia, kwamba Mungu aliumba Adam na Eva wakiwa kama caucasians na waliishi pale mesopotamia( Iraq )na uzao wakwanza wa binadamu ulikuwa hapo mpaka pale ambapo waliamua kujenga mnara wa babeli wakatanywa kwenye uso wa dunia na kutengeneza hizi races zote zilizopo sasaivi(Monogenism)..Kadri walivyoenda mbali kutoka Iraq ndipo walizidi kubadilika kutokana na mazingira, magonjwa na tabia.Mfano Waafrika wakawa weusi kwasababu ya joto, mongolians wakawa na sifa zile kwasababu ya baridi nk. Nk.

Lakini ukiangalia fuvu la caucasian lipo symetrical kuliko yote, kwahyo aliamini mungu ndio aliumba binadamu akiwa caucasian.

View attachment 2416994

Samuel G. Morton
Huyu mmarekani alikuja kutumia Idea za blumenbach kupima ukubwa wa ubongo wa kila race kati ya hizo tano na akasema caucasian ndio wanaongoza kuwa na ubongo mkubwa na Ethiopians/Negros ndio wa mwisho.katika kitabu chake miaka ya 1830's Akahitimisha kuwa binadamu walitokea independently katika maeneo mbalimbali ya dunia (polygenism) na kuleta hizi races tunazoziona leo. Na wenye ubongo mkubwa ndio walio intelligent hivyo haiwezekani kubadilika.

View attachment 2416998

Kwahyo mpaka hapo ilitokea debate kati ya monogenism Vs polygenism ipi ni sahihi?
Monogenism:Imani kuwa race zote na watu wote duniani tumetokana na chanzo kimoja (in this case kwa Adam na Hawa)

Polygenism:Imani kuwa binadamu tumetokana na vyanzo mbalimbali katika maeneo mbalimbali

Darwin theory of evolution
Mwaka 1859, muingereza Charles Darwin alichapisha kitabu chake 'on the origin of species' ambapo alielezea theory yake ya evolution. Alisema viumbe wote duniani ni ndugu, wametokana na chanzo kimoja ila kutokana na mazingira na ushindani basi kukafanya viumbe wabadilike kuendana na mazingira hivyo husababisha kutokea kwa specie mbalimbali. Kwahyo Darwin aliiprove Monogenism ila sio ile ya Adam na Eva. ikatambulika kuwa binadamu wote tulikuwa na chanzo kimoja.

Lakini kwasababu evolution ni very slow process, haiwezi kuwa tumetoka kwa Adam na Eva miaka 6000 iliyopita ikabidi watabiri miaka malaki kadhaa binadamu alitokea sehemu fulani na kusambaa dunia nzima.

View attachment 2416999

Out of Africa theory
Darwin baada ya kuwa'study apes(tumbili, sokwe, nyani) wa Africa alihitimisha kuwa binadamu tumetokea Africa, Alisema kuwa huenda miaka ya zamani binadamu na hawa apes walikuwa na baba mmoja ambapo walievolve na kutuleta sisi.

Lakini kipindi Darwin anasema hayo hakukuwa na sayansi ya archeology (ya kufukua mafuvu ya kale na kuyapima umri) wala Genetics.

Baadae archeologists Kina dr. Leakey na wengine waligundua kuwa kweli binadamu wa kale waliishi East Africa around miaka laki 2 iliyopita. Na pia kupitia genetics walithibitisha kuwa sisi na hawa apes tulikuwa kitu kimoja takibran miaka million 7 iliyopita.

Kwahyo hii out of africa theory inasema, miaka laki2 iliyopita binadamu wa sasa(homo sapiens) alianza kuwepo hapa East Africa, na miaka 60,000 iliyopita akatoka Africa na kuitawala dunia na ndipo hizi races tofauti zikatokea.

View attachment 2417003
Pan African theory
Hii ni very recent, wanasayansi wamegundua kuwa kumbe sio East Africa tu bali ni karibia Africa nzima ndipo binadamu alipotokea, maana kuna mafuvu yamepatikana North Africa, West Africa na South Africa yanayoonesha kuwa binadamu wa kale zaidi (homo habilis, Naledi nk.) walikuwepo huko na walichangamana ili kumpata huyu binadamu wa leo (homo sapiens).

Binadamu wa aina nyingine
Kupitia Archaeology, wanasayansi wamekuja kugundua kumbe kulikuwa na binadamu wa aina nyingine(hominids) ambao sio homo sapiens. Tena inaonekana hata miaka 70, 000 tu iliyopita kulikuwa na species za binadamu zaidi ya 7 hapa duniani. Ntataja za muhimu.

Neanderthals: hawa wamegundulika walikuwepo sanasana Ulaya na waliishi kati ya miaka laki 7 mpaka 60,000 iliyopita. binadamu wote (kasoro waafrika) wanaonesha kuwa na vinasaba vya DNA ya Neanderthals.View attachment 2417000
Denisovans: Hawa waligundulika huko Serbia maeneo ya Asia huko na waliishi around miaka 30,000 mpaka 14500 iliyopita.

Homo fluorensis: Hawa walikuwepo huko indonesia mpaka binadamu walipoenda huko miaka 50,000 iliyopita na kuwafanya wapoteeView attachment 2417002
Homo Naledi:Hawa wamegundulika south Africa na inaonekana waliishi miaka 335,000-230, 000 iliyopita
View attachment 2417001
Wapo homo wengine wengi.

The big picture (My conclusion)
Kupitia ushahidi mbalimbali wa mafuvu, genetics, molecular biology, Paleontology nk. Tunaweza ku'summarize hii story kwa kifupi hivi.
Binadamu tulianzia hapa Africa kwa staili hii (still debatable)

Miaka Millioni 7 iliyopita: Binadamu (Homo) na sokwe(chimpanzee) wakaachana na kukatokea homo habilis, homo erectus na homobwengine

Miaka million 2 iliyopita: Homo habilis alifanikiwa kutoka Africa na kwenda ulaya na Asia
Miaka laki 7 iliyopita: Huko ulaya akatokea Neanderthal
Miaka laki 3 iliyopita: Baada ya homo wengi kuungana(sex) kwa muda mrefu hapa Africa ndio homo sapiens (sisi) akaanza kupatikana...lakini pia homo wengine waliendelea kutoka nje ya Africa.

Miaka laki 2 iliyopita: tukaanza kutumia tools mbalimbali ambazo zimegundulika Olduvai gorge na sehem zingine za Africa. (Muda huo huo kule Asia na Ulaya wale homo habilis wameevolve kutengeneza Denisovans, Homo fluorensis na wengine)

Miaka 60,000 iliyopita: Homo sapiens (sisi) tukaanza kutoka Africa na kwenda ulaya na Asia ambapo hao waliotoka walikutana na homo wengine kina Neandarthals, Denisovans na wengine na wakafanya nao ngono wakazaa wazungu, wachina na race zingine..Huku sisi waafrica tukabaki hapahapa.

Miaka 6,000 iliyopita: (kipindi hiki hawa Homo wengine wote wameshapotea duniani) Binadamu (homo sapiens) wakawa wameanza kupata akili na kutengeneza miji, Lugha,maandishi, Art, Music, agriculture na ndipo tukaanza kupata Dini (Hindu, Zorastrianism,) na ndipo ukawa mwanzo wa kumbukumbu zote tulizonazo leo kuhusu historia ya nchi, empires, tawala na falme mbalimbali kwasababu hapo ndipo tulipogundua kutunza kumbukumbu kupitia maandishi na lugha.

Miaka 4000 mpaka 1400 iliyopita: Uyahudi, ukristo na uislam ukaanza ambao ukainfluence historia yote iliyopita na kutufanya tuamini sisi tumetengenezwa juzijuzi tu (miaka 6000 iliyopita) kwa nguvu kutoka angani isiyoonekana.

(oh, by the way..zile data za Samuel Morton kuhusu ukubwa wa ubongo na akili zilikuja kugundulika kuwa zilipikwa. Huyu jamaa alikuwa racist hivyo alipika data ili ziendane na ideology yake, hivyo endeleeni kuwa na imani na Mama)
Na pia fuvu la homo neanderthalensis lina-suggest kua alikua na ubongo mkubwa kuliko sisi homo sapiens, ivo kuna inawezekana walikua na uwezo mkubwa wa akili kuliko sisi. Sasa wanasayansi bado wanaumiza kichwa kufikiria kwann walitoweka na sisi tukabaki ingawa inaonesha walikua na akili kutuzidi!
Nadharia moja wapo wanafikiri kua walitoweka kwasababu ya uhafifu wa chakula. Wao walikua na miili mipana zaidi na walipendelea nyama sana (waliwinda). Kulingana na tafiti, inaonekana waliwinda wanyama wakubwa sana (size za nyati) hivo mara nyingi walipatwa na majeraha katika mawindo yao. Fossils zao nyingi zinaonesha mifupa iliovunjika na kupona ivo kuna uwezekana walikua waliwinda kwa shida. Na pia ubongo mkubwa unahitaji mlo mkubwa alafu wao walikua na miili mipana hivo aliitaji chakula kingi zaidi. Sasa homo sapiens walivokuja katika maeneo ya Neanderthals waliwashinda katika kupata vyakula juu ya fact kwamba miili yetu imeumbika kustahimili sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hivi haiwezekani kuwa common ancestor wa sisi na Neanderthals alikuwa nje ya Afrika? Halafu baadae akarudi Africa, watoto waliobaki Ulaya wakawa Neanderthals na walionde Africa wakawa homo sapiens?
Kuna hii wanasema kwamba common ancestor alikua afrika kisha baadhi ya homo sapiens walipohama na kwenda mabara mengine wakaanza kuevolve ili kuadapt na mazingira ya kule. Sasa wale homo sapiens waliobaki huku afrika hawakuevolve au walievolve kdg sana kwasababu walikua fit na mazingira waliopo. Homo sapiens waliobak afrika wakaanza kusambaa tena duniani na ndipo wakakutana na wale homo wengine ambao walievolve kua Neanderthals etc... ndio wakaanza kujaamiana nao na mwisho wa siku wakapotezwa. Bado haiko clear nn kiliwaondoa lakin tunafkiri ni competition ya resources. Ndiomaana mpaka leo waafrika hatuna DNA za homo neanderthalensis ila wazungu wengi wanazo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hawa Neanderthals, sio kwamba walipochangamana na homo sapiens ndio kukapatikana hizi race za wazungu wenye akili?? Mbona sisi Africa bado sana hata kiuwezo wa kufikiria?[emoji1787][emoji1787]
Tunawaza ngono tu
Homo neanderthalensis walikua na mafuvu makubwa kuliko homosapiens ivo inafikiriwa kua walikua na ubongo mkubwa zaidi. Ubongo mkubwa = akili nyingi...?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mh! Mm ni mfuatiliaji sana wa hizi mambo ila sijawahi amini hizi hadithi za ngedere mara chipanzee mara nyani, mbona hao nyani wa leo hawabadiliki!!?
Eti mbona nyani wa leo hawabadiliki?[emoji23]
Umefatilia hizi mambo kweli wewe? Evolution haina final goal. Yani final goal sio kwamba nyani awe binadamu... nyani ivo alivo hakuwa ivo miaka 700,000 iliopita.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na pia fuvu la homo neanderthalensis lina-suggest kua alikua na ubongo mkubwa kuliko sisi homo sapiens, ivo kuna inawezekana walikua na uwezo mkubwa wa akili kuliko sisi. Sasa wanasayansi bado wanaumiza kichwa kufikiria kwann walitoweka na sisi tukabaki ingawa inaonesha walikua na akili kutuzidi!
Nadharia moja wapo wanafikiri kua walitoweka kwasababu ya uhafifu wa chakula. Wao walikua na miili mipana zaidi na walipendelea nyama sana (waliwinda). Kulingana na tafiti, inaonekana waliwinda wanyama wakubwa sana (size za nyati) hivo mara nyingi walipatwa na majeraha katika mawindo yao. Fossils zao nyingi zinaonesha mifupa iliovunjika na kupona ivo kuna uwezekana walikua waliwinda kwa shida. Na pia ubongo mkubwa unahitaji mlo mkubwa alafu wao walikua na miili mipana hivo aliitaji chakula kingi zaidi. Sasa homo sapiens walivokuja katika maeneo ya Neanderthals waliwashinda katika kupata vyakula juu ya fact kwamba miili yetu imeumbika kustahimili sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Interesting, shukran sana kwa mchango wako....
Sidhani kama Neanderthals walikuwa na akili kuliko homo sapiens kwasababu hiyo uliyoisema ya kuwa na mwili mkubwa.

Researchers wa oxford walistudy x-stics za ubongo wa Neanderthals,- kwasababu sehemu ya ubongo inayodeal na visual processing(visual cortex) kwa mnyama huwa ina volume approximately sawa na volume ya macho yake, wakiangalia neanderthals walikuwa na Macho makubwa sana (kwasababu walievolve ulaya ambako hakuna mwanga sana) kwahyo Walikuwa na Visual cortex kubwa, hii inamaanisha sehemu kubwa ya ubongo wao ilideal na kucontrol vision na kuucontrol ule mwili mkubwa, na siyo kufikiria(higher functions)...kwahyo walikuwa na cerebrum ndogo compared to sapiens.

ila Nadhani walikuwa not so far behind, kwasababu kuna evidence za intelligence kubwa walikuwa nayo kama kutumia tools na kuzika wafu wao Lakini hawakuwa na higher intelligence kama language, agriculture, etc.

Hata gorillas wana ubongo mkubwa kuliko sisi ila hawatufikii akili kwasababu ya mwili wao mkubwa.

ila still...swali la hawa homonids wengine kupotea ni puzzle mi naona, kwasababu ukipata hypothesis ya kuwaaccount Neanderthals bado swali litakuja kwa hominid wengine...kwanini Naledis na homo Florensiesis walienda extint wakati wana umbo dogo? Gorrilas wapo hadi leo na wana umbo kubwa.

Although sidhani kama ilikuwa ni cause moja tu ilisababisha but Ice age played a huge role.
 
Back
Top Bottom