Chanzo ya Manjano, haijatukuta

Chanzo ya Manjano, haijatukuta

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
Ukiishi nchi ya ujanaujana kila kitu ni ujanja ujanja

Yaani hata sindano ya manjano unahonga ugongewe muhuri tu badala ya kuchomwa

Haya.
 
Na kuna jamaa wako mpaka flani wa kilimanjaro na kenya wao wanatumia cheti fake wanaiibia serikali kabisa, bora ugongewe muhuri kwa cheti halali, unapewa cheti fake, kinagongwa muhuri wananunua karatasi cha njano kutoka stationary wanaprint, haela inakuwa yao serikali inapata ziro. Magufuli anakazi kubwa sana nchi hii.
 
mkuu nijuze huo mpaka ni sirari, horohoro au namanga?
 
Nakumbuka pale Horohoro walinikomalia mpaka nikachoma...nashukuru kupata vaccination...ni kweli wengi hawapendi kuchoma..
 
heri ulichomwa japo kwa kung'ang'aniwa
 
Hivi huo ugonjwa wa manjano upo kweli au?

upo vizuri sana. Inasababishwa na virusi vinavyoambukizwa na mbu.

Kwenye karne ya 18 huu ugonjwa ndio ulikuwa "UKIMWI" wa wakati huo.

Watu wanaoishi maeneo ya joto ndio wanakufa wengi kwa ugonjwa huu hasa Afrika.
 
Nakumbuka pale Horohoro walinikomalia mpaka nikachoma...nashukuru kupata vaccination...ni kweli wengi hawapendi kuchoma..
napita ha[o soon je ulikua na cheti chetu kile?
 
Watu wengi mnakosea kwenda kuchukulia mpakani zile kadi,ukienda hospital yoyote ya serikali unapewa bure.
 
Back
Top Bottom