BANDOKITITA
JF-Expert Member
- Oct 4, 2022
- 1,484
- 2,852
Ajali za barabarani zinaepukika ukiachilia mbali matatizo ya kibinadamu. Kuna sababu nyingi sana zimekuwa zikitajwa, lakini mimi niseme mbali na sababu zote hizo zinazotajwa chanzo kikubwa ni abiria wenyewe.
Sijui ni ukosefu wa elimu ya kwa Watanzania au kudharau au kuona muda wote Mungu yupo upande wao tu. Maana serikali kupitia jeshi la police wamekuwa wakitoa Elimu kwa abiria juu ya madhara ya mwendo kasi, lakini mara nyingi ukiskia ajali ya basi chanzo huwa ni speed.
Tatizo huanzia kwa ujuaji kwa baadhi ya abiria. Ktk safari ya basi huwa kuna mchanyiko wa abiria tofautitofauti. Mimi nataka kuongelea wale wanaotaka kujulikana km na wao wana miliki au wamewahi kumiliki magari. Mkiwa safarini ikatokea abiria mmoja au kadhaa kulalamikia speed ya dereva hawa wajuaji utaskia wanasema "hiyo speed ya kawaida sna labda hujawahi kuendesha gar" au watasema "labda wewe ni mara Yako ya kwanza kusafiri". Kwa ujumla huwa Wana maneno flani ya dharau.
Tatizo lingine ni uharaka wa baadhi ya abiria na kushindwa kukumbuka misemo ya wahenga isemayo "haraka haraka haina baraka au polepole ndiyo mwendo au heri kuchelewa kuliko kutokufika kabisa". Mkiwa safarini akitokea abiria anakemea speed utawaskia wale wanaojifanya wana haraka wanamjibu "kama unaoona speed ni kubwa shuka, wengine tunawahi mambo yetu au wengine tuna wagonjwa humu tuna wawahisha hospitali au watasema, 'wengine tunawahi msibani/tuanawahi biashara zetu".
Ili kudhihirisha wana haraka utaskia wanamwambia dreva, "dreva ongeza speed wengine tunachelewa mambo yetu, km umechoka pisha hapo tukusaidie". Abiria wa namna hii hufikiri yule/wale wanaokemea speed kubwa wao wamepanda km kujionesha au wanatalii tu. Dreva nae aksikia anapata backup ndiyo kwanza anaongeza speed.
Mwisho kuna wale abiria wanaoingiwa na uoga kwa kupigwa mkwara na dreva au kondakta pale abiria wanapoona speed Kali. Abiria wakikemea speed utaskia dreva anajibu "usinifundishe kazi km unaoona speed kubwa shuka". Kwa uoga mkubwa tena fikiria anakuambia ushuke sehemu yenyewe ni porini hakuna huduma yoyote au huenda ni usiku na eneo analokuambia kushuka hakuna hata nyumba, ili kuepuka hili abiria huamua kuufyata na kumuuacha dreva na konda wake wafanye watakavyo. Very sad.
Haya yote hupelekea dreva kujiona yeye ndiyo mmiliki wa gari na Mnyazimungu ni baba yake.
NB:
1) Pamoja na madhaifu haya yote ya abiria, dreva wote wa basi za abiria watambue wamebeba roho za watu, siyo mizigo hiyo au makreti ya soda/bia kwamba basi likianguka wananchi wengine wataburudika. Bali wajue basi likianguka na kuua au kuwaacha vilema familia ndiyo zinapata pigo na uchungu usiomithilika na Taifa hupoteza nguvu kazi ktk ulinzi na uzalishaji mali. Vipi km kwenye hayo mabasi wangekuwa wanabeba na ndugu zao mathalani wake/baba/mama zao wangekuwa wanajibu hovyo hovyo hivyo na kuwa na speed km hiyo?
2) Abiria tuache ushawishii na ujuaji kwa dreva unaoweza kumsababisha aongeze speed na hatimae kusababisha ajali.
3) Abiria tuitumie vyema elimu inayotolewa na jeshi la police na kuachana na tabia ya ouga.
Mimi binafsi kwa kutokuwa na tabia ya ouga na kuitumia vyema Elimu inayotolewa na jeshi la police vilishaniwezesha kuepusha mabalaa mengi ktk safari zangu. Nitolee mfano mmoja tu hapa, Kuna siku nilikuwa nasafiri tena safari ya masafa marefu, kumbe yule dreva alikuwa kalewa baadhi ya abiria tukamshitukia tukamwambia asimamishe gari ili tuletewe dreva mwingine, kichotokea ni baadhi ya abiria waliojiona wana haraka na kuanza kupaza sauti zao kuwa "anaetaka kusubiri dreva mwingine au anaogopa speed ashuke". Pasina uoga kati ya abiria wote tulijikuta tumebaki 2 tu tuliokerwa na majibu ya abiria wenzetu.
Tuliungana na yule mwenzangu kuwaelimisha abiria wenzetu juu ya kuendeshwa na dreva mlevi pasipo mafanikio.Na bahati nzuri yule mwenzangua alikuwa askari "kipenyo". Ikabaki mimi na mwenzangu bila kujuana kila mmoja akiwa anafanya awezalo ili kuepusha balaa. Kumbuka hapa huyo mlevi bado anaendeha kwa kubahatisha, mimi nilifikisha taarifa fasta kwa maafisa usalama waliokuwa kituo kinachofuata, kumbe mwenzangu nae keshawaliana na wenzake. Wakati huo dreva na kondakta wake walisha shitukia. Tulipofika tu kituo kilickokuwa kinafuata yule mlevi fasta alijichanganya na abiria akatokomea wakati tunashuka kujisaidia na ghafla aliingia dreva mwingine. Tukapanda na kuendelea na safari.
Abiria tuzitumie namba za makamanda wa police wa kila mkoa, na hata za makao makuu ya police inapoonekana hatua hazichukuliwi kwa wakati muafaka kuepusha ajali zisizo za lazima. Pia Kuna namba za Bure za maafisa wa Tarura kwa kila mkoa. Kizuri zaidi karibu kila basi la Abiria ndani kuna namba za kutolea taarifa kwa matukio ambayo siyo ya kawaida ktk safari, Mfano speed kubwa nk.
Nawatakia kila heri abiria wenzangu, tuchukue tahadhari ajali zinaua na kuziacha familia zetu kwenye huzuni mkubwa na pengo lisilo zibika.🙏🙏