Chapa ya Mpinga Kristo nyuma ya Worldcoin na Crypto currency, AI robot

Kristo hatapingwa kama kweli alikuwa mwana wa Mungu, kama ni wa mchongo kupingwa ni wajibu.
 
Hata cm unayo tumia imetengenezwa na mpinga kristo
 
Imani za kidini ni shambulio la akili
 
Tena watakupenda na kukupa cheo Kanisani, sadaka za dollar?!
 
Wasabato mmeanza mambo yenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi ishu ndo sasa zinakuwa fast tracked na kina Webb wa World Economic Forum (WEF) kwenye ile wanayoita agenda 2030 kwamba hutamiliki chochote na utakuwa na furaha na pia tutakula wadudu.

Kwenye agenda zao naona wanatilia mkazo sana hiyo wanayoita 4th revolution ambayo itaendeshwa sana na matumizi ya kimtandao, mambo kama hayo ya digital ID, carbon footprint na pia wanajenga hoja zao kwenye majanga ya dunia kama covid, climate change na kuna janga la kimtandao ambalo wametabiri litatokea hivi karibuni (global cyber-event) ambapo mitandao duniani itashambuliwa na kupelekea janga kubwa sana la kijamii maana kwa sasa huduma mbalimbali mfano za kibenki, kiutumishi zinaendeshwa kupitia mifumo ya kimtandao.

Kuhusu kuihusianisha hiyo digital ID na alama ya mnyama iliyotabiriwa kwenye maandiko nakubaliana na wewe.
Mpinga kristo.
Ufunuo wa Yohana 13:16-17
[16]Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao;

[17]tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.

Maana yake ni kwamba digital ID itawaondoa wasiokuwa nayo kwenye mfumo wa kiuchumi na kijamii (economical and social sanctions).....unakuwa huna tofauti na marehemu. Huwezi kupata huduma benki au kulipwa malipo yoyote au kufanya manunuzi yoyote maana hivyo vyote vitafanyika kupitia digital ID. Tulizoea kwamba nchi ndo inawekewa vikwazo, sasa hapa mtu binafsi ndo atawekewa vikwazo (individual sanctions) au kwamba kukataa kuwa na hiyo chip ni kujiondolea mwenyewe uhai (suicide).

Kwa hiyo kutiwa chapa kwenye mkono wa kuume ni kukubalina na masharti, ambayo kimsingi yana mlengo wa kumwabudu ibilisi, ili yakuwezeshe wewe kupata huduma za kiuchumi na kijamii kwa ajili ya kukuwezesha kuishi.

Na kutiwa chapa kwenye paji la uso ni swala la kubadilishwa fikra, badala ya kuwa na fikra za kumwabudu au kufanya matendo yanayoendana na kumwabudu au kumtumikia Mungu Mwenyezi utafanya kinyume chake ambazo ni fikra za kumwabudu na kumtumikia ibilisi.

Haya uliyosema hapa chini ni katika jitihada za kuweza kumwekea binadamu chapa kwenye paji la uso, yaani kumbadilisha fikra ziwe za kumwabudu na kumtukuza ibilisi.
AI robot ataweza kumjua au kuingiliana zaidi na binadamu, ataongoza hisia na maamuzi ya binadamu kwa binadamu kuwekewa chip.
Inasemekana chip hiyo itamsaidi binadamu kuondokana na msongo wa mawazo kabisa na kutokujitambua.
Fikra za binadamu zitaweza kuongozwa na AI (your will, Action and Emotion ambazo hutoka nafsini mwa mtu).

Kongole sana kwa kuja na bandiko kama hili tunapoelekea kwenye zama za kujidhihirisha kwa mpinga Kristo na ujio wa alama ya mnyama na mateso ya dhiki kuu.
 
Kenya kuna ambushi imetokea watu wakikua wanakesha siku tatu kusajiliwa kitambulisho cha dunia wapata bonus ya Crypto currency za bure.
 
Kenya kuna ambushi imetokea watu wakikua wanakesha siku tatu kusajiliwa kitambulisho cha dunia wapata bonus ya Crypto currency za bure.
Watu wanalilia chapa, hatari sana..
 
Unaogopa Chapa? Vipi kuhusu maneno, matendo na lufestyle ya Mpinga Kristo?
Mnawekeza nguvu katika kupambana na Chapa huku mnaishi maneno na vitendo.
Dunia ya kuogopa chapa?
Huo uhanithi
 
Biblia bhana Kwa hiyo Moto wa mbinguni utawashwa Kwa kiberiti sasa ni Cha Mo au kangoroo au cha gesi??Ngoja Nile jani Korofi Kwanza!!
 
Unaogopa Chapa? Vipi kuhusu maneno, matendo na lufestyle ya Mpinga Kristo?
Mnawekeza nguvu katika kupambana na Chapa huku mnaishi maneno na vitendo.
Dunia ya kuogopa chapa?
Huo uhanithi
acha kunidhani na hunijui.
 
acha kunidhani na hunijui.
Sasa nani ametaka kukujua hapa? Si umej8tambulisha mwenyewe kupitia maandishi yako ya kipuuzi? Kama hautaki watu wakujue ungeficha upumbavu wako.
Mnakumbatia Matendo ya hovyo halafu mpo busy kuhubiri habari za Chapa, Mnachapwa nini...ebwoo!
 
Sasa nani ametaka kukujua hapa? Si umej8tambulisha mwenyewe kupitia maandishi yako ya kipuuzi? Kama hautaki watu wakujue ungeficha upumbavu wako.
Mnakumbatia Matendo ya hovyo halafu mpo busy kuhubiri habari za Chapa, Mnachapwa nini...ebwoo!
mambo gani ya hovyo hayo ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…