Katika thread ambazo niliamini kuwa kuna watu ni wabishi lakini hawapendi kujifunza bali wanataka ubishi ni hii mada. Nakumbuka nilichangia mwanzoni sana lakini niliona hakuna anayependa tujifunze bali ni ubishi.
Anyway, kwa kutoa mchango na mawazo yangu, Charles Darwin sio muanzilishi wa concept ya Evolution. Mwanzoni hii idea ya evolution ilikwepo kwenye baadhi ya Imani kama vile Buddhism na Induism. Buddha alisema ulimwengu unachange, viumbe vinachange nothing stay the same as it is, everything change from one form to another. Pia kwa upande wa wanafalsafa idea hii ilitolewa mawazo na Lucretius mwanafalsafa wa kigiri aliyeamini ulimwengu, viumbe na ufahamu umeanzia kutoka simple to complex. Miaka 600 kabla ya Darwin uarabuni alikwepo mtafiti na explorer aitwaye Nasir al-Din Tusi ambaye naye alizungumzia evolution ya viumbe kwa kina na hakukosea ila tu hakuwa na tafiti. Wapo watafiti kabla ya Darwin kama vile Russel Walace, Thomas Malthus, Erasmus Darwin aliyekuwa mlezi na babu wa Darwing ndiye aliyemfundisha Darwin kuhusiana na evolution kwa kusafiri na, kuchunguza nyani wa Africa na waka watu wa kwanza kuamini kuwa Nyani, masokwe na binadamu wametoka katika aina moja ya kumbe kilichoishi zamani sana ambacho kutokana na mageuzi kwa muda mrefu wa miaka na miaka zikatoka species mbalimbali wakaziita primates. Hivyo evolution sio idea ya Darwin tu, kuna imani za kale ziliiamini, kuna wanafalsafa wa kale walisema hivyo hivyo ila contribution ya Darwin ni alipoifanya iwe kisayansi kwa kutafuta ushahidi wa Mabaki ya mifupa ya kale, kuangalia sifa za viumbe na classification.
Evolution haizungumzii mwanadamu tu, ni kila kiumbe dunia. Kupitia evolution farasi, punda na pundamilia waligunduliwa hapo kale walikuwa trait moja na species moja.
Evolution inajibu kuhusiana na kwanini simba, paka, chui, puma wanafanana.
Evolution inajibu kwanini nyangumi ana mapafu, ni mnyama na ana nywele badala ya magamba, kwanini nyangumi ananyonyesha na kuzaa. Ni kwasababu aliwahi kuwa mnyama wa nchi kavu aliyetemea kuwinda vyakula vya kwenye bahari na hatimaye maisha yake yakazoea na sasa anaishi majini, pia sawa kwa kasa, na Sea Lion.
Evolution inajibu jinsi Penguin waliwahi kuwa ndege
Evolution inajibu jinsi viumbe vilipoacha kutaga na kuanza kuzaa
Evolution inajibu kwanini kuna mchina, mwafrika, mzungu na wote wanatofautiana. Mwafrika hawezi kuzaa na mwafrika wakapata mchina hata siku moja, then kama bila evolution tutasema wachina na races zilitoka wapi?
Evolution inajibu kwanini ukikunja kiganja chako mishipa ya mkono unautumia sana inayounganisha muscles na movement ya vidole inatofautiana katika mkono ulioutumia zaidi.
Evolution inajibu kwanini watoto wako hawawezi kufanana na wewe completely, na jinsi genes zinavyofanya shuffling na mutation.
Evolution inajibu mutation inavyofanya kazi
Evolution inaelezea kwanini Olduvai na sehemu nyingi kuna mabaki ya Homins wana sifa za nyani katika muonekano lakini walikuwa watembea miguu miwili na wamekutwa mifupa yako kwenye mabaki ya mawe na mifupa. Mifupa ina alama za meno na mawe katika kufunjwa na mawe yanaonekana yamechongwa kwa nia na madhumuni ya matumizi.
Evolution inajibu jinsi mwanadamu alivyosambaa kutoka afrika kuenea mpaka mabara mengine
Evolution inajibu kwanini huwezi kupata mabaki ya kale ya mwanadamu yanayozidi miaka milion 1.5 nje ya Africa.
Evolution inajibu mabaki ya viumbe wa kale ambao hawapo leo mfano farasi mwenye kwato tatu mifupa yake ipo olduvai, twiga wa shingo fupi, vifaru wafupi, tembo mammoths, dinasours waliokuwa wanapaa.
So why shouldn't I believe in Evolution? It make sense to me.
NB: Mimi ni archaeologist ninachukua masters ya Pili (Masters in Archaeology) University of Dar es Salaam. Katika fields zangu nimechimba sana, nimechunguza mifupa sana for 5 years now na siwezi kupinga. Kuna concepts kwenye evolution unaziona kabisa kwenye remains za kale.
Kama huamini evolution its okay, kama unaona ni illuminati ni mawazo na fikra zako. Sio lazima kila mtu awe na mtazamo huo. Sio kila mtu ni mkristu au muislam. Wengine imani zetu zinaunga mkono evolution na hatuwezi kusema ni uongo au ni ushetani as some perceive kutokana na imani zao.