GE2025 Charles Gabriel: Jitokeze mapema kuhakiki majina yako kabla ya kufika siku ya kupiga kura Oktoba 29

GE2025 Charles Gabriel: Jitokeze mapema kuhakiki majina yako kabla ya kufika siku ya kupiga kura Oktoba 29

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Wananchi wa Jimbo la Ushetu, wilayani Kahama, mkoani Shinyanga, wametakiwa kujitokeza mapema kuhakiki majina yao katika vituo 565 vya kupigia kura vilivyoandaliwa, huku waliopoteza vitambulisho vya kura wakiruhusiwa kutumia hati za kusafiria, leseni za udereva au vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Akizungumza ofisini kwake, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo, Charles Gabriel, amesema siku ya kupiga kura itakuwa Jumatano, Oktoba 29, ambapo vituo vyote vitafunguliwa saa 1:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni.

“Katika vituo hivyo, kutakuwa na mfano wa karatasi za kupigia kura za wagombea wa urais, ubunge na udiwani. Ni muhimu kila mpiga kura azione mapema ili ajue namna ya kuzitofautisha,” amesema Gabriel.

Screenshot 2025-10-23 001831.png
 
Back
Top Bottom