Uchaguzi 2020 Charles Hilary chukua fomu ya Ubunge Jimbo la Kibamba hakika utashinda kwa kishindo

Aisee baada ya ile kauli ya "wewe gombea tu ukishindwa tutaangalia nafasi nyingine" naona kila mtu anataka kutupa ndoano baharini.
Kumbe umegundua huyu ndo Charles Hilary mwenyewe?
 
Hapana sio kwamba ni ujinga ila inaonekana tu Kuna kitu binafsi ambacho wewe hukipendi hapo.
Kwamba simpendi Charles? kanikosea nini? Hoja yangu Bungeni sio kijiwe na wastaafu ni mahali akili zinatakiwa kuchemka sasa mkijaza wastaafu kuna lipi la maana litatokea maana wastaafu hawatakuwa na chakupoteza hata wakigonga meza kwao inatosha
 
Na ukurugenzi wa radio Azam fm amuachie Nani?
Unacheza na ukurugenzi kwa bahresa?
Mkwanja mrefu anavuta pale.
Anataka aache kazi ya taaluma yake akaunge juhudi akaishi kwa huruma ya jiwe kwamba inategemea atakavyoamka
 
Na Mimi pia nimeshauri agombee yule kwasababu ya utu uzima wake na busara alizo nazo pia amefanya kazi mashirika mengi hivyo ana weledi wa kutosha, kama kustaafu ni huko sekta binafsi ili kwenye siasa bado anaweza kuendelea.
Kwanini usiwe wewe
 
Kwamba simpendi Charles? kanikosea nini? Hoja yangu Bungeni sio kijiwe na wastaafu ni mahali akili zinatakiwa kuchemka sasa mkijaza wastaafu kuna lipi la maana litatokea maana wastaafu hawatakuwa na chakupoteza hata wakigonga meza kwao inatosha
Kwahiyo huyo akili haichemki? Kwa umri gani alio nao hadi ashindwe kuwa bungeni.
 
Bado hujanielewa tu mkuu unakwama wapi? Hizo siasa za kuitana nyumbu na kondoo ni wewe na wenzako ndo mnaziweza, Mimi sizijui mkuu.

Basi umeingia kwenye siasa kwa bahati mbaya.
 
Anataka aache kazi ya taaluma yake akaunge juhudi akaishi kwa huruma ya jiwe kwamba inategemea atakavyoamka
Hiki ndicho ulichoacha kuongea mkuu, wewe sema tu sio kwamba huyu hafai kuwa mbunge eti kwasababu mstaafu ila sema hupendi agombee kwa kupitia ccm bila shaka ningeshauri agombee kwa kupitia Chadema au chama chochote cha upinzani usinge kuja kusema haya unayoyasema hapa.
 
ana umri gani ?
 
Akitaka kuharibikiwa aingie ccm kusaka vyeo...awaulize kina bashiru
 
Vijembe ni sehemu ya siasa.
Sasa kama vijembe ni sehemu ya siasa kwanini sasa wewe ukatae na uone haifai yeye kujiingiza kwenye hiyo siasa unayo iita ya kikondoo?
 
Huyu katumwa apime upepo.
Inaonekana unamuogopa sana huyo jamaa akigombea hilo jimbo mkuu, mshawishini ajiunge Chadema mtaongeza kiti cha Ubunge na sio kuja na chuki za ovyo hapa.
 
Charles Hilary akitaka kudhalilika ajaribu kujiunga na mambo ya ccm , hatutakuwa na mswalie mtume
Ewaa hiki ndicho kitu amlisahau kukiweka wazi sio kuja hapa kusingizia ustaafu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…