Kuna mahali nimeandika unachokisema? In case unekuja speed sana karudie kusoma tena. Sio sawa kila mtu kujifanya ni mtangazaji wa misiba ya watu na kusema amefariki kwa ugonjwa gani ilhali si msemaji wa familia wala hajaona death certificate inayoonesha marehemu amefariki kwa sababu gani.
Huu ni udaku unaopaswa kukoma. Inatosha kutoa taarifa za tanzia na mahali alipofia. Mambo ya ndani iachwe familia itangaze kama itapenda.
Mbowe alitangaza ndugu zake wamefariki kwa Corona na ilikuwa sawa. Ila sio random people kujifanya wasemaji wa familia.
Kumalizia hebu fikiria umefiwa na baba yako (Mungu aepushie mbali) halafu unakuta watu kama 100 hivi JF wanasema mzee kafariki kwa hiki ama kile. Unadhani utajisikiaje? Misiba ni faragha, tuwafariji wafiwa bila kuingilia faragha zao. Kama hatuwezi kuwafariji heri tukae kimya