Charles Kitwanga atajwa kuhusika na kashfa ya ufisadi katika Jeshi la Polisi ya sh. bilioni 34

Charles Kitwanga atajwa kuhusika na kashfa ya ufisadi katika Jeshi la Polisi ya sh. bilioni 34

Status
Not open for further replies.
Yaani vituo 14 tu kati ya vyote vile,hii si madharau jamani?,
watumbuliwe wote bila kuangalia nyago ya mtu,

washaniudhi sasa,bilion 34 za burebure wanajichotea tu
 
Mhe Rais, amekuwa akieleza mara kwa mara kuwa hatawavumilia wateule wake ambao watashiriki ktk ufisadi
Naomba kushauri kuwa Mhe huyu anatakiwa awajibishwe haraka sana, vinginevyo tutaamini kuwa ile Kauli yetu ya Kizaramo "UKIWAONA KAMA WATU".
Mhe Rais Jipu kubwa hilo, unachotakiwa si kulitumbua bali ni kulikamua.
 
Tumeshindwa kwny Uchaguzi Mkuu kutokana na kukithiri vitendo cha Rushwa ndani ya Chama pamoja na ukosefu wa nidhamu-Freeman Aikael Mbowe Mwenyekit wa Chadema Taifa.


unajipoza machungu.
 
Hakuna namna wote waende kisutu wakapishane na kina Kitilya mlangoni, hakuna sababu ya kuendelea kumuita Mh. wakati ni mwizi, kumbe ndio maana watu wanahonga hela nyingi kuingia bungeni ili wapate nafasi ya kulinda uovu wao eeee, halafuu huyu DG. ana mahela tele kwenda kushindisha watoto wa watu barabarani bila kuwalipa mafao yao ni laana kweli kweli. wao ndio wanajua matumizi ya hela upuuzi mtupu.
 
Swali hapa ni je:
Wakati ameteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani ame-declare interest ya hizo kampuni (Lugumi enterprises, Infosys...etc.) na hata kabla ya hapo alipo apishwa bungeni amejaza fomu ya maadili ikionyesha vyanzo vyake vyote vya mapato. Je amefanya hivyo?.

Prof. Anna Tibaijuka alitiwa hatiani kwa arguments kama hizi.

.......Na tusubiri.
 
Huyu jamaa si ndie jina lake sijui lilikuwa kwenye payroll ya BOT ? leo tena anatajwa kwenye ufisadi wa bilioni 30 na ushee ??

Haya ngoja tumsubirie msemaji w wizara yake aje kukanusha badala ya Kitwanga ,
 
Waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga na Dk Modestus Kipilimba mkurugenzi wa NIDA? Hapa kuna jambo!

Tunzeni hii formula; ufisadi(mashine za alama za vidole+Vitambulisho vya Taifa)=wizara ya Kitwanga.

Iliwahi kuandikwa humu hata kabla JPM hajatangaza baraza lake la mawaziri, kwamba Kitwanga alikuwa akijitangaza kwamba atapewa uwaziri na kweli akaupata.

Iliwahi kuandikwa humu pia kwamba Kitwanga na Magufuli ni marafiki wa kutupwa (rejea urafiki wa Kikwete na Lowassa) akakanusha.

Kwa sababu wakati anaingia mkataba huo wa mabilioni na jeshi la polisi hakuwa waziri wa mambo ya ndani lakini baadaye akapewa wizara hiyo hiyo itupe picha gani? Kwamba aliiomba kwa rafiki yake ili asimamie kuuficha ufisadi wake.

Na kama ndivyo, alimdokeza rafikie kwa nini anautaka uwaziri wa mambo ya ndani? Wizara ambayo nina uhakika haiwezi na hataiweza na niliwahi kuandika humu kwamba, Rais anampaje mfanyakazi wa benki kusimamia wizara ya mambo ya ndani.

Ngoja tusubiri yaliyo njiani.
 
Kama Bunge lisipokubali kupiga vigelegele na likafuatilia, hakuna mtu atapona.
Kazi ya Bunge ni kuishauri na KUISIMAMIA serikali. Likitimiza wajibu hizo mbili nchi itarudi kwenye mstari
 
Aisee ...hii ni hatari..sana hivi huyo kipilimba si ndo aliwafukuza wale vijana wa nida bila kuwalipa stahiki zao na uzi umeshatolewa humu ....au ndo hela na jasho la hao vijana ndo alikua anaendeshea kampun yake hio na mwenzie..Chozi la mnyonge haliendi bure.
Huyo Waziri na Mchungaji lao moja
 
Waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga na Dk Modestus Kipilimba mkurugenzi wa NIDA? Hapa kuna jambo!

Tunzeni hii formula; ufisadi(mashine za alama za vidole+Vitambulisho vya Taifa)=wizara ya Kitwanga.

Iliwahi kuandikwa humu hata kabla JPM hajatangaza baraza lake la mawaziri, kwamba Kitwanga alikuwa akijitangaza kwamba atapewa uwaziri na kweli akaupata.

Iliwahi kuandikwa humu pia kwamba Kitwanga na Magufuli ni marafiki wa kutupwa (rejea urafiki wa Kikwete na Lowassa)

Kwa sababu wakati anaingia mkataba huo wa mabilioni na jeshi la polisi hakuwa waziri wa mambo ya ndani lakini baadaye akapewa wizara hiyo hiyo itupe picha gani? Kwamba aliiomba kwa rafiki yake ili asimamie kuuficha ufisadi wake.

Na kama ndivyo, alimdokeza rafikie kwa nini anautaka uwaziri wa mambo ya ndani? Wizara ambayo nina uhakika haiwezi na hataiweza na niliwahi kuandika humu kwamba, Rais anampaje mfanyakazi wa benki kusimamia wizara ya mambo ya ndani.

Ngoja tusubiri yaliyo njiani.
 
Tena eti naskia Skia ni mchungaji wa kanisa moja Hv pale external linaitwa City Harvest! Kwel mtumishi wa Mungu unaweza kufanya haya yote jaman tumuogopen Mungu! Anaona yote tunayoyafanya hapa duniani!
 
  • Huyu Dr kapilimba si ameletwa hapo kukaimu nafasi,, kumbe nae jipu!!!! Alaf nasikia ni mchungaji wa kanisa flani ubungo!! Bilion 34 kwa kweli ni pesa ndefu sana!! Sheria uchukue mkondo wake ikiwezekana wasimamishwe kazi waachie ofisi,,waridishe pesa na wafilisiwe Mali zao zote then wafikishwe mahakamani
 
Vita dhidi ya rushwa,ufisadi,madawa ya kulevya,wizi etc ni vita endelevu.
As long as mwanadamu bado yupo juu ya uso wa hii dunia...
 
Nina uhakaika asilimia 100% Mkurugenzi wa NIDA siyo mmoja ya wamiliki wa infosys. Ndiyo, Kitwanga ni mmoja ya shareholder wa infosys IPS Ltd. Kampuni ya infosys IPS Ltd ni moja ya kampuni chache za IT zenye ufanisi mkubwa na uadilifu ktk utendaji. Ni kampuni ambayo hutimiza ahadi siku zote. Infosys IPS Ltd imewahi kufanya miradi mikubwa sana na wateja kama wizara ya fedha, TRA etc, na kote huko haikuwahi kuchelewesha kazi. Tusubiri naamini kukatakuwa na sababu za kwa nini Lugumi walichelewa au wamechelewa kutekeleza mradi. Hivyo infosys IPS Ltd na Charles Kitwanga ni kampuni safi na Mh. Charles Kitwanga ni muadilifu na mchapa kazi.
 
Hao watu ni wabaya sana.. Huyo mkurugenzi wa nida kaenda kufukuza vijana wasio na hatia watendani wa chini kabisa huku akiendelea kula na waovu wenzake meza moja eti ili ajisafishe tumuone mtu mwema kumbe na yy ni jipu..
Hawa wanasiasa wanaturubuni sana akili zetu. Ingekuwa amri yng hao ni wakunyongwa kabisa
 
Yaani hao Siyo majipu ni vidonda nduguu hao viongozi Kabisa haiwezekani unakuwa hodari kuwafukuza vijana kazini bila Kuwapa Stahiki zao ulijiona mwema ubaya umewarudia wenyewe. Wapeni vyao
 
Tumewapa wapinzani.hoja za kuinuka nazo bungeni kwa ajili ya kulindana lindana,serikali ingekuwa safi kabisa sasa imekuwa chafu kupita ile,waziri wa mapolisi unakuwa kibaka nani atakuwa msafi....Namuona Magufuli kuzeeka ghafla kabla ya muda,nampa mwaka na nusu mvi tele kichwani
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom