Waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga na Dk Modestus Kipilimba mkurugenzi wa NIDA? Hapa kuna jambo!
Tunzeni hii formula; ufisadi(mashine za alama za vidole+Vitambulisho vya Taifa)=wizara ya Kitwanga.
Iliwahi kuandikwa humu hata kabla JPM hajatangaza baraza lake la mawaziri, kwamba Kitwanga alikuwa akijitangaza kwamba atapewa uwaziri na kweli akaupata.
Iliwahi kuandikwa humu pia kwamba Kitwanga na Magufuli ni marafiki wa kutupwa (rejea urafiki wa Kikwete na Lowassa)
Kwa sababu wakati anaingia mkataba huo wa mabilioni na jeshi la polisi hakuwa waziri wa mambo ya ndani lakini baadaye akapewa wizara hiyo hiyo itupe picha gani? Kwamba aliiomba kwa rafiki yake ili asimamie kuuficha ufisadi wake.
Na kama ndivyo, alimdokeza rafikie kwa nini anautaka uwaziri wa mambo ya ndani? Wizara ambayo nina uhakika haiwezi na hataiweza na niliwahi kuandika humu kwamba, Rais anampaje mfanyakazi wa benki kusimamia wizara ya mambo ya ndani.
Ngoja tusubiri yaliyo njiani.