Yaani waende kisutu kabisa hata kesho nyie papaz mnajiona wasafi kumbe wachafu kabisaHao watu ni wabaya sana.. Huyo mkurugenzi wa nida kaenda kufukuza vijana wasio na hatia watendani wa chini kabisa huku akiendelea kula na waovu wenzake meza moja eti ili ajisafishe tumuone mtu mwema kumbe na yy ni jipu..
Hawa wanasiasa wanaturubuni sana akili zetu. Ingekuwa amri yng hao ni wakunyongwa kabisa
Basi huo upepo utaondoka na watu...Ni upepo tu
Kanda yetu sasa..mkuu yule jamaa atakuwa aliupata uwaziri kwa kigezo cha ong'wise
Nani anayehusika sasa kma huyo aliyetajwa unakataa..Nina uhakaika asilimia 100% Mkurugenzi wa NIDA siyo mmoja ya wamiliki wa infosys. Ndiyo, Kitwanga ni mmoja ya shareholder wa infosys IPS Ltd. Kampuni ya infosys IPS Ltd ni moja ya kampuni chache za IT zenye ufanisi mkubwa na uadilifu ktk utendaji. Ni kampuni ambayo hutimiza ahadi siku zote. Infosys IPS Ltd imewahi kufanya miradi mikubwa sana na wateja kama wizara ya fedha, TRA etc, na kote huko haikuwahi kuchelewesha kazi. Tusubiri naamini kukatakuwa na sababu za kwa nini Lugumi walichelewa au wamechelewa kutekeleza mradi. Hivyo infosys IPS Ltd na Charles Kitwanga ni kampuni safi na Mh. Charles Kitwanga ni muadilifu na mchapa kazi.
Kwa hiyo Waziri na DG wa Nida Ni maparter ndio maana Rahisi kaenda Kupumzika maana DG wa Nida na Waziri wa mambo ya ndani Wote majipu makubwa yaliyo hiva. Da masifa yote kumbe amnna lolote. Magazeti haliyo yatumia kuwachafua wafanyakazi wa Nida waliofukuzwa kama mbwa na kutopewa stahiki zao yamemchafua yeye. Da amakweli malipo hapa hapa Duniani mbinguni esabu.
unataka kusema,aliingia mambo ya ndani ili akafiche hiyo scandal?Waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga na Dk Modestus Kipilimba mkurugenzi wa NIDA? Hapa kuna jambo!
Tunzeni hii formula; ufisadi(mashine za alama za vidole+Vitambulisho vya Taifa)=wizara ya Kitwanga.
Iliwahi kuandikwa humu hata kabla JPM hajatangaza baraza lake la mawaziri, kwamba Kitwanga alikuwa akijitangaza kwamba atapewa uwaziri na kweli akaupata.
Iliwahi kuandikwa humu pia kwamba Kitwanga na Magufuli ni marafiki wa kutupwa (rejea urafiki wa Kikwete na Lowassa) akakanusha.
Kwa sababu wakati anaingia mkataba huo wa mabilioni na jeshi la polisi hakuwa waziri wa mambo ya ndani lakini baadaye akapewa wizara hiyo hiyo itupe picha gani? Kwamba aliiomba kwa rafiki yake ili asimamie kuuficha ufisadi wake.
Na kama ndivyo, alimdokeza rafikie kwa nini anautaka uwaziri wa mambo ya ndani? Wizara ambayo nina uhakika haiwezi na hataiweza na niliwahi kuandika humu kwamba, Rais anampaje mfanyakazi wa benki kusimamia wizara ya mambo ya ndani.
Ngoja tusubiri yaliyo njiani.
WAZIRI WA MAGUFULI KTK KASHFA YA UFISADI NA POLISI
- Kampuni inayohusishwa naye ya Infosys ilikuwa mkandarasi
Yadaiwa Infosys inamilikiwa na Kitwanga na Mkurugenzi Mkuu NIDA
Ni mdau wa LUGUMI enterprises
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga atajwa kuhusika na kashfa ya ufisadi katika Jeshi la Polisi ya sh. bilioni 34, imeelezwa.
Kuhusika huko kwa Waziri Kitwanga imekuja siku moja, baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali(PAC) kueleza kuwa kuna ufisadi mkubwa kwenye mkataba ulioingia kati ya Jeshi la Polisi Nchini na Kampuni ya Lugumi Enterprises.
Taarifa za kuaminika ilizozipata gazeti hili, zimeeleza kuwa Waziri Kitwanga anahusika kupitia kampuni yake ya Infosys anayomiliki pamoja na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), iliyo chini ya Wizara hiyo hiyo.
Jeshi la Polisi limekumbwa na kashfa kubwa ya manunuzi ya vifaa vya kuhifadhi alama za vidole ambapo Kamati ya PAC imegundua kuwa kampuni ya Lugumi Enterprises haikutekeleza mkataba ipasavyo.
Kampuni hiyo ililipwa sh. bilioni 34 na jeshi la polisi ili kusambaza vifaa hivyo nchi nzima katika vituo 138 vya polisi lakini ni vituo 14 vilivyopata vifaa hivyo.
Gazeti hili limegundua kuwa moja ya kampuni iliyopewa kazi hiyo ni Infsosys ambayo nakala za msajili wa makampuni inaonyesha kuwa inamilikiwa na Charles Kitwanga na Dk. Modestus Francis Kipilimba, ambaye ni Mkurugenzi wa NIDA.
Nyaraka za uchunguzi ikiwemo mkataba kati ya kampuni ya Lugumi na Infosys ambazo gazeti hili imeziona inaonyesha kuwa Kampuni hiyo ya Waziri Kitwanga ilifanya kazi ya kuunganisha internet kati ya vituo vya polisi na mkonga wa taifa.
Kazi ambayo haikufanyika kabisa kwani mpaka sasa ni vituo 14 tu vya polisi viliunganishwa, ambapo baadhi ya taarifa ilizozipata gazeti hili zilionyesha kuwa moja ya taarifa ya ukaguzi inaonekana Marijani Saleh alisaini kufikisha vifaa vya Infosys.
Vifaa hivyo, vinaelezwa vilifikishwa Machi 2, 2012. Katika Nyaraka hiyo upande wa Jeshi la Polisi alisaini ofisa mmoja wa Polisi aliyejulikana kwa jina la Nestory Tagaya na mdau mwingine kutoka kampuni ya BioLink alikuwa Pierson J.
Taarifa iliyotolewa na PAC hivi karibuni ilionyesha kuwa kampuni ya Lugumi ilingia mkataba na Jeshi la Polisi mwaka 2011, kwa kazi hiyo ya kufunga mitambo hiyo kwenye vituo vya Polisi vya wilaya nchi nzima na kulipwa fedha zote huku kazi ikiwa haijafanyika.
asee hizo bilioni 34 lazima watazitapika asee,,Tumewapa wapinzani.hoja za kuinuka nazo bungeni kwa ajili ya kulindana lindana,serikali ingekuwa safi kabisa sasa imekuwa chafu kupita ile,waziri wa mapolisi unakuwa kibaka nani atakuwa msafi....Namuona Magufuli kuzeeka ghafla kabla ya muda,nampa mwaka na nusu mvi tele kichwani